Rais Samia apokea Ndege ya Mizigo, aeleza nia ya Serikali kuboresha Sekta ya Anga kwa miaka mitano ijayo

Kwahiyo kwenye mapokezi ya ndege mikusanyiko inaruhusiwa?

Au waliokusanyika washadungwa kitu cha Johnson?

Msamaria mmoja aniangalizie kama spika wetu Job Ndugai kahudhuria mapokezi.... huwa hakosagi yule kwenye haya mambo...

Otherwise tuanzishe kampeni yetu pendwa "Where is our beloved Speaker?"
Anamuda gani hajaonekana aiseee baada ya kuwataka mje na hoja mbadala?!
 
#NUKUU: RAIS SAMIA AKIPOKEA NDEGE MPYA DASH 8- Q400

Baadhi ya nukuu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Ndg. Samia Suluhu Hassan akizungumza leo Julai 30, 2021 wakati wa kupokea ndege mpya aina ya DASH 8-Q400 katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

#twendePamoja
#kwaMatokeoYaHaraka
#KaziIendelee

IMG-20210730-WA0062.jpg

IMG-20210730-WA0063.jpg

IMG-20210730-WA0064.jpg

IMG-20210730-WA0065.jpg

IMG-20210730-WA0066.jpg

IMG-20210730-WA0067.jpg
 
Hahah...

Jamaa huwa wanafungua wapo vizuri sana kwenye kuzichapa ndege maji...

Mimaji inaruka juu haswa, wakati siku ile pale K'koo ilichukua muda kweli kuweza kurusha maji kupitia ule uwazi wa juu wa soko
Magari ya fire yaliyoko uwanja wa ndege na pale fire makao makuu ni tofauti na hata siku moja magari ya uwanja wa ndege hauwezi kuyakuta fire makao makuu
 
Hivi JNIA haikuwa na taa mpaka mama yetu alijikwaa kwa msaidizi wake Jana na kusimama kwa mshangao kama vile alikwazika yaani hii haikuwa poa kabisa jamani ndege 2 zilizosalia wahusika mkiona muda umekwenda Bora zilale Nairobi na kuanza safari mchana siku inayofuata siyo aibu ya Jana.
Povu na utoporo ruksa
 
Mama umesema uchumi unakua ? Hongera kwa kurekebisha mambo ya uchumi, Unaonaje tukarudi kwenye suala la katiba mpya ? 🤣🤸🐒
 
Magari ya fire yaliyoko uwanja wa ndege na pale fire makao makuu ni tofauti na hata siku moja magari ya uwanja wa ndege hauwezi kuyakuta fire makao makuu

Mkuu wakati wa emergency kubwa hayo ya Airport huwa walau gari moja hutolewa na kwenda kupambana na moto nje ya Airport kama moto ni mkubwa sana unaohitaji zile gari...

Hata Kariakoo walipeleka lakini ni baada ya muda mrefu kupita...

Screenshot_20210731-090943~2.png
 
Nyerere amefanya maendeleo gani mkuu! Hata ki-TV kumiliki ilikua ishu! Katika marais watano waliopita plus mama samia wanaafazali kuliko nyerere.
Wakati Nyerere anapigania uhuru babu yako alikuwa anafanya nini?

Kana hujui alichafanya Nyerere basi hapa sio mahali sahihi kwako rudi shule usome historia na literature mbalimbali ili uelewe alichofanya Nyerere.
 
Kama ni ya mizigo basi ni vema...., ila mizigo kwenda wapi mbona nimesikia kama ni masafa mafupi...., kwenye mizigo ya ndani kwa ndani si tungeboresha treni na kuongeza mabehewa au upembuzi yakinifu umefanyika na kuona kuna demand ya mizigo mingi ya wadau nchini wenye uwezo wa kulipia kwa ndege ambayo haipati huduma
 
Mkuu wakati wa emergency kubwa hayo ya Airport huwa walau gari moja hutolewa na kwenda kupambana na moto nje ya Airport kama moto ni mkubwa sana unaohitaji zile gari...

Hata Kariakoo walipeleka lakini ni baada ya muda mrefu kupita...

View attachment 1874955
Ni sawa na ni kwa vile ilikuwa usiku kama ni mchana sidhani kama hilo gari unaweza kuliona huko
 
Wakati Nyerere anapigania uhuru babu yako alikuwa anafanya nini?

Kana hujui alichafanya Nyerere basi hapa sio mahali sahihi kwako rudi shule usome historia na literature mbalimbali ili uelewe alichofanya Nyerere.

Bila wazee wa kiislamu angekuwepo pale!!!! Navyojua waislamu ndio wamemuweka pale, pamoja na hayo yote bado aliendelea na ushenzi na kuwachukia waislamu + na mauwaji ya waislamu/waarabu katika mapinduzi ya zanzibar akishirikiana na yule kafiri mwenzie okello, na abeid karume na kuuwa waislamu/waarabu. Acha kuwatetea magaidi wewe.

Mohamed Said
 
Ni sawa na ni kwa vile ilikuwa usiku kama ni mchana sidhani kama hilo gari unaweza kuliona huko

Huwa yanatoka kwa dharura (hadi waombwe) na kutegemea moto huo unawaka wapi...

Hiyo ya Kariakoo sio mara ya kwanza
 
Bila wazee wa kiislamu angekuwepo pale!!!! Navyojua waislamu ndio wamemuweka pale, pamoja na hayo yote bado aliendelea na ushenzi na kuwachukia waislamu + na mauwaji ya waislamu/waarabu katika mapinduzi ya zanzibar akishirikiana na yule kafiri mwenzie okello, na abeid karume na kuuwa waislamu/waarabu. Acha kuwatetea magaidi wewe.

Mohamed Said
Ndio maana nikasema rudi usome historia. TAA ilianzishwa na nani? Nyerere aligombea uongozi wa TAA na alichaguliwa kwa mujibu wa katiba ya TAA. Yeye ndiye aliyeshawishi wenzie wabadilishe TAA ili ipiganie uhuru wa Tanganyika na kuunda TANU ; Rupia alikuwa muislamu?

Hao waislamu unaodai walimpisha kwa nini wampishe? Kwanza sio kweli .

Watu walioshiriki kudai uhuru walikuwa na dini zao lakini waliungana kwa lengo moja tu lla kupigania uhuru. Dini haikuwa kigezo. Nyerere ndiye aliyeongoza harakati hizo huo ndio ukweli upende au usiupende na itafundishwa hivyo daima hadi mwisho wa dunia.

Bila Nyerere uhuru usingepatikana ndani ya miaka saba tena bila kumwaga damu. Nani alienda UN kudai uhuru? Kama Nyerere hakufanya kitu nani aliyefanya kitu na unakipimaje? Nyerere hakuna kiongozi baada yake atakayemfikia kwa mambo aliyoifanyia nchi hii. Nina hakika babu yako alikuwepo wakati wa harakati za kudai uhuru lakini alikwepa kushiriki.
 
Kwahiyo kwenye mapokezi ya ndege mikusanyiko inaruhusiwa?

Au waliokusanyika washadungwa kitu cha Johnson?

Msamaria mmoja aniangalizie kama spika wetu Job Ndugai kahudhuria mapokezi.... huwa hakosagi yule kwenye haya mambo...

Otherwise tuanzishe kampeni yetu pendwa "Where is our beloved Speaker?"
Tayari?
 
Back
Top Bottom