Rais Samia apewa ujumbe kuelekea mwaka mmoja wa uongozi wake

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
Na Maziku Jr

Mapema leo hii wadau mbalimbali wa Sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wameshiriki mjadala ulioendeshwa na Taasisi ya Watch Tanzania kwa njia ya mtandao. Mjadala huo ulioshirikisha wadau kutoka ndani na nje ya nchi ulihudhuriwa na Mh. Nape Nnauye.

Mjadala huo ulijikita katika mambo yaliyofanyika kwa kipindi cha karibuni mwaka mmoja sasa tangu Rais Samia aingie madarakani. Baadhi ya mambo yaliyoelezwa na kuwavutia washiriki ni pamoja na;

1. Serikali kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari na kutoa ruhusa kwa vyombo binafsi kupewa matangazo kutoka Taasisi za serikali.

2. Serikali kujipanga kisekta kuhakikisha Tanzania inanufaika na mapinduzi ya nne ya viwanda.

3. Serikali kuchukua hatua katika kusimamia maslahi ya wanahabari katika Tasnia nzima.

4. Mamlaka za serikali kama vile TCRA kuweka mazingira wezeshi kwa biashara zinazochipukia kwenye maeneo ya ubunifu.

5. Serikali kuunda Bodi ya Tume ya TEHAMA na kuiwezesha katika kiutendaji katika kutekeleza majukumu yake hususani kusaidia utekelezaji wa adhma ya Rais kuona TEHAMA inanufaisha watanzania.

6. Serikali kuweka ukaribu na watoaji huduma za mawasiliano ili kutatua changamoto za walaji ambao ni wananchi.

7. Mh. Rais kuwezesha upatikanaji wa fedha kwaajili ya kuimarisha mifumo ya kidijitali na mazingira mazuri ya Kuchochea ubunifu.

8. Serikali kuimarisha huduma ya Mawasiliano nchi nzima kupitia mfuko wa UCSAF.

Kwa mjadala huu ni hakika Rais Samia amefanya mapinduzi makubwa katika wizara hii inayojihusisha na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Kama mwanahabari napenda kuungana na wanahabari wote kumpongeza kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya.
 
Back
Top Bottom