Serikali yaongeza mara mbili zaidi mzunguko wa fedha (M3) kutoka 6.5% hadi 12.7%

Mimi nilikuwa mdau wa Upinzani kwa miaka mingi ila toka wapinzani wanunuliwe niliwapuuza rasmi,nimewahi tumia rasilimali zangu kwa ajili ya wapinzani hasa Silinde na Waitara.

Na kale kashonza kalikuwa kanatupangia majukumu tukiwa chuo kumbe ni kashenzi.From there nikaacha siasa rasmi nikawa mpinzani wa Magu hasa kwenye sera zake za kipuuzi za Uchumi.

Alivyoshika mama nikaona tunaenda sawa kwenye issues za management of economy,mambo ya siasa sihusiki nayo,namkubali mama kwenye sera za Uchumi za kiliberali.
Hizi ID za mwendokasi sio za kuaminika!ID mwezi uliopita,hizi ni ID za mapambio tu!
 
Umetaka kushawishi zitumike taarifa za nje au sikukuelewa?

Zitumike local data ambazo zinaonesha uhalisia sio za kuchachawa!! Unakumbuka zile figures mlizomchomekea Rais kuhusu status ya foreign reserve kwenye speech yake aliyoitoa mwisho wa mwaka? Namna hiyo mtaaminika vipi na nyie ndio wasemaji wa Serikali?
 
Zitumike local data ambazo zinaonesha uhalisia sio za kuchachawa!! Unakumbuka zile figures mlizomchomekea Rais kuhusu status ya foreign reserve kwenye speech yake aliyoitoa mwisho wa mwaka? Namna hiyo mtaaminika vipi na niye ndio wasemaji wa Serikali?
daaah
 
Hakika kuhusu money supply bado sana na Samia ashaambiwa ushauri wa bure na Shabiby bungeni mishahara ongeza, lipa madeni,lipa wazabuni, lipa wastaafu, lipa malimbikizo, weka bajeti ya taasis kufanya seminar na vikao, nunua mazao ya wakulima, pesa za tarura na madarasa zinaenda kwa wahuni wachache
Tangu lini Shabiby akajua Uchumi wewe jamaa
 
===
Katika kipindi cha miezi tisa sasa tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani Uchumi wa Tanzania umeendelea kuwa imara siku hata siku ambapo ulikuwa kwa wastani wa asilimia 5.2 kutoka asilimia 2.1 katika kipindi kama hicho FY2020.

Ukuaji huu wa Pato la Taifa ( GDP ) unachagizwa zaidi na kuimarishwa kwa Sekta ya Utalii iliyochangia kwa asilimia 18.,Kilimo kilichochangia kwa asilimia 15.1 lakini pia kuimarishwa kwa miundombinu ya Usafirishaji,Mawasiliano na kuimarisha sekta ya fedha nchini,

Mfumuko wa bei umeendelea kusalia katika urari wa tarakimu moja ya kati ya asilimia 3 na 5 hali iliyosababishwa naupatikanaji wa Chakula cha kutosha cha zaidi ya tani laki mbili kwa mujibu wa ripoti za BOT huku ukiyumbishwa kidogo na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kulikosababishwa na janga la COVID 19.

Sote tunafahamu,Kabla ya Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan na katika mwaka wa fedha 2019|2020 Ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi ( M3 ) kwa mujibu wa BOT ulikuwa na kufikia asilimia 6.5,

Majaabu ni ripoti za robo ya tatu za Benki Kuu ya Tanzania zinaonesha ujazi huo huo wa fedha zinazomiminika ( liquid money-M3 ) umefikia asilimia 12.7 kutoka asilimia 6.5 sawa na ongezeko la karibu asilimia 100 yaani mara mbili zaidi kwa kipindi hiki kifupi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan,

Kwa maana nyepesi sasa hivi unaweza kuiandika noti ya Shilingi elfu 10 jina lako na baada ya muda mfupi ikakupata tena ikiwa na jina lako Natoa mfano tu sisemi tuchafue noti zetu tufanyeni kazi vipimo vya kitaalamu vinaonesha pesa tayari iko mtaani inamiminika ila lazima tufanye kazi kwa bidii na maarifa kwani hakuna pesa ya bure Tanzania,

Wakati huohuo Ujazi wa fedha kwa tafsiri finyu yaani ( M2 ) nayo imeongezeka kutoka asilimia 9.1 FY2019|2020 hadi asilimia 14.9 hivi sasa huku akiba|Ukwasi yaani ( M0 ) nayo ikikua kutoka asilimia 5.7 hadi asilimia 6.3 yaani kila Sekta mambo ni bambam na Rais Samia Suluhu Hassan,

Ukuaji huu wa Ujazi wa pesa yaani M3, M2 na M0 umechagizwa zaidi na Sera rafiki na madhubuti za Kiuchumi zinazosimamiwa na Rais wa awamu hii ya Sita Mhe Samia Suluhu Hassan anayesimamia kwa Vitendo Ukuaji wa Uchumi akiufungamanisha na Maendeleo ya Watu na Maendeleo ya Vitu,

==================================
View attachment 2070665

View attachment 2070666
Nikweli pesa imerejea mtaani tufanye kazi kwa bidii,
 
Back
Top Bottom