Serikali yaongeza mara mbili zaidi mzunguko wa fedha (M3) kutoka 6.5% hadi 12.7%

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
4,984
4,083

Rais Samia Suluhu Hassan tayari ameongeza mara mbili zaidi mzunguko wa fedha yaani (M3) kutoka 6.5% hadi 12.7%​


===
Katika kipindi cha miezi tisa sasa tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani Uchumi wa Tanzania umeendelea kuwa imara siku hata siku ambapo ulikuwa kwa wastani wa asilimia 5.2 kutoka asilimia 2.1 katika kipindi kama hicho FY2020.

Ukuaji huu wa Pato la Taifa ( GDP ) unachagizwa zaidi na kuimarishwa kwa Sekta ya Utalii iliyochangia kwa asilimia 18.,Kilimo kilichochangia kwa asilimia 15.1 lakini pia kuimarishwa kwa miundombinu ya Usafirishaji,Mawasiliano na kuimarisha sekta ya fedha nchini,

Mfumuko wa bei umeendelea kusalia katika urari wa tarakimu moja ya kati ya asilimia 3 na 5 hali iliyosababishwa naupatikanaji wa Chakula cha kutosha cha zaidi ya tani laki mbili kwa mujibu wa ripoti za BOT huku ukiyumbishwa kidogo na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kulikosababishwa na janga la COVID 19.

Sote tunafahamu,Kabla ya Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan na katika mwaka wa fedha 2019|2020 Ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi ( M3 ) kwa mujibu wa BOT ulikuwa na kufikia asilimia 6.5,

Majaabu ni ripoti za robo ya tatu za Benki Kuu ya Tanzania zinaonesha ujazi huo huo wa fedha zinazomiminika ( liquid money-M3 ) umefikia asilimia 12.7 kutoka asilimia 6.5 sawa na ongezeko la karibu asilimia 100 yaani mara mbili zaidi kwa kipindi hiki kifupi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan,

Kwa maana nyepesi sasa hivi unaweza kuiandika noti ya Shilingi elfu 10 jina lako na baada ya muda mfupi ikakupata tena ikiwa na jina lako Natoa mfano tu sisemi tuchafue noti zetu tufanyeni kazi vipimo vya kitaalamu vinaonesha pesa tayari iko mtaani inamiminika ila lazima tufanye kazi kwa bidii na maarifa kwani hakuna pesa ya bure Tanzania,

Wakati huohuo Ujazi wa fedha kwa tafsiri finyu yaani ( M2 ) nayo imeongezeka kutoka asilimia 9.1 FY2019|2020 hadi asilimia 14.9 hivi sasa huku akiba|Ukwasi yaani ( M0 ) nayo ikikua kutoka asilimia 5.7 hadi asilimia 6.3 yaani kila Sekta mambo ni bambam na Rais Samia Suluhu Hassan,

Ukuaji huu wa Ujazi wa pesa yaani M3, M2 na M0 umechagizwa zaidi na Sera rafiki na madhubuti za Kiuchumi zinazosimamiwa na Rais wa awamu hii ya Sita Mhe Samia Suluhu Hassan anayesimamia kwa Vitendo Ukuaji wa Uchumi akiufungamanisha na Maendeleo ya Watu na Maendeleo ya Vitu,

==================================
photo_2022-01-06_02-51-12.jpg


photo_2022-01-06_02-51-47.jpg
 
Wewe mchambuzi mpumbafu tu, Huna hoja kabisa,


Mimi nafanya vitu serious wewe unaleta UCHADEMA kwenye vitu serious,
Ha ha ha sijafika huku muda mrefu, nimejichimbia kusoma updates za kula ki masihara tu. Haya mambo mengine serious tueaachie wahusika maana hatuna uwezo wa kubadilisha watakalo, uwezo wetu unaishia kusifu au kupiga kelele tu
 
mambo za Multi ID yanajidhihiri hapa.
Unaandika halafu unakuja kujijibu mwenyewe. Huku unachungulia post yangu imesomwa mara ngapi?

Frankly speaking mambo serious sana nimeyapa kisogo. Ni kujitia stress tu. MMU kuzuri bana, stress freee
 
Unaandika halafu unakuja kujijibu mwenyewe. Huku unachungulia post yangu imesomwa mara ngapi?

Frankly speaking mambo serious sana nimeyapa kisogo. Ni kujitia stress tu. MMU kuzuri bana, stress freee
Soma vizuri comment yako na ya jamaa yako,
 
Back
Top Bottom