Rais Samia anawezaje kujenga zahanati 564, Vituo vya Afya 304 na Hospitali 68?

View attachment 2197392
===
Kunawakati huwa nikimsikia mtu anamsema vibaya huyu Mama natamani kumpiga na kitu kizito kichwani,basi ni vile sheria tu hairuhusu na Mungu hataki,

Hebu jiulize,tangu tupate Uhuru ni lini umewahi kuona jumla ya Zahanati mpya 564 zinajengwa kwa mpigo tena nchi nzima?

Hebu jiulize tena,tangu tupate Uhuru ni lini umewahi kuona vituo vipya vya Afya 304 vinajengwa kwa Mpigo nchi nzima?

Hebu jiulize zaidi,tangu tupate Uhuru ni lini tuliwahi kujenga hospitali 68 ikiwemo ile ya Mbagala kwa mpigo?

Hebu pitia kwa utulivu hii taarifa toka TAMISEMI, then umsikie mtu anamsema vibaya mama kama hujatamani kufanya ninayotamani Mimi,

=====
HUDUMA ZA AFYA YA MSINGI-TAMISEMI

27. Mheshimiwa Spika
, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais - TAMISEMI iliidhinishiwa Shilingi bilioni 28.20 kupitia ruzuku ya Serikali Kuu,

Fedha hii ni kwaajili ukamilishaji wa ujenzi wa maboma 564 ya Zahanati katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Hadi kufikia Februari 2022, zimepokelewa Shilingi bilioni 23.32 sawa na asilimia 82.69 ya fedha zilizoidhinishwa.

28. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Shilingi bilioni 110.60 ziliidhinishwa kupitia ruzuku ya Serikali Kuu,

Fedha hii ni kwaajili ya kuendeleza na ujenzi wa Vituo vya Afya 304.

Kati ya hivyo, Vituo 52 vilianza kujengwa Mwaka wa Fedha 2019/20 ,

Jumla ya Vituo 252 vimeanza kujengwa Mwaka wa Fedha 2021/22,

Jumla ya Vituo 18 vimejengwa kwenye Halmashauri zenye Mapato madogo,

Vituo 234 vimejengwa katika Tarafa zisizo kuwa na Vituo vya Afya na Kata za Kimkakati kupitia tozo za miamala ya simu.

Hadi Februari, 2022 Shilingi bilioni 108.05 zimepokelewa sawa na asilimia 97.69 ya fedha zilizoidhinishwa na ujenzi unaendelea,

29. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Serikali ilitenga Shilingi bilioni 81.10,

Fedha hizi ni kwaajili ya kuendelea na ujenzi wa Hospitali 68 ,

Hadi Februari, 2022 Shilingi bilioni 66.80 sawa na asilimia 82.36 zilikuwa zimepokelewa na ujenzi upo katika hatua mbalimbali,

NB, Hizi Zahanati 564,Vituo vya Afya 304 na Hospitali 68 vyote hivi vinajengwa na TAMISEMI tu achili mbali vile vinavyojengwa na Wizara ya Afya sijaviorodhesha hapa,
unakosa subira acha kuwaza kumpiga mwenzako na kitu kizito kichwani atakufa.Pili nikukosowe siyo samia kajenga bali serikali.Huu ni mrejesho wa kodi zetu si hisani.
 
Naona una maaba makubwa na rais wako. Kwa hiyo mikopo ya Matirioni ya fedha yaliyokopwa huko Ulaya hujawahi kuyasikia?. Si ndivyo?. Hauishi Tz?. Hizo fedha za Matozo ya simu tunazikatwa tunapoenda kwa wakala kutoa visijenti vyetu kununulia nyanya na zile tunazotuma kwa bibi zetu wanunue mafuta ya taa nazo hukuwahi kusikia. ?. Acha ushabiki.
Kipi kizuri. Ufe kwa njaa kwa sababu ya ujeuri au uishi au uwe mjinga ili ule na uishi. Ukitaka kula lazima na wewe ukubali kuliwa .......by jk

Sasa jpm hakutaka kuliwa hata kidogo ndo Mana nchi ilikuwa haimuvu kabisa na ajira zote zimepotea wamebbaki machinga wanarandaranda barabarani tu
 
Chawa mmekuwa wengi halafu pia wajinga ni wengi.

Kodi yako ndio inamlipa mshahara huyo Mama pia kodi yako ndio inajenga hayo madarasa na vituo vya afya.

Bila wewe na mimi huyo Rais si kitu .

Chakula ,malazi , matibabu anapata bure kwa kodi zetu kwahiyo hakuna haja ya kusifiwa.

Man up we're not going to buy cheap propaganda and politics of deceit.
 
Wewe pia ni chawa wa Mbowe, Unanyoosheaje wenzio vidole?
 
Nadhani tujadili hoja wala sio Who we are,
Hoja ni kuwa hakuna Samia analoweza kufanya bila nguvu ya wananchi.

Msururu wa kodi na tozo ndio zinaendesha serikali.

Take it to the bank.

Sovereignty belongs to the people ,however supremacy belongs to the constitution so you must not confuse sovereignty with supremacy.
 
Hoja ni kuwa hakuna Samia analoweza kufanya bila nguvu ya wananchi.

Msururu wa kodi na tozo ndio zinaendesha serikali.

Take it to the bank.

Sovereignty belongs to the people ,however supremacy belong to the constitution so you must not confuse sovereignty with supremacy.
Rais ni mwakilishi wa wananchi,

Anachofanya ndicho wanachofanya wananchi and verse versa is true,

take it from me
 
Nikiwa nasoma hapa ndio nakumbuka hoja ya mbunge Manyanya kwamba tuone namna ya kuondoka na chawa kwenye nchi hii.
Nakumbuka pia taarifa ya kwamba hii nchi inakila kitu ila Haina watu sahihi.
 
View attachment 2197392
===
Kunawakati huwa nikimsikia mtu anamsema vibaya huyu Mama natamani kumpiga na kitu kizito kichwani,basi ni vile sheria tu hairuhusu na Mungu hataki,

Hebu jiulize,tangu tupate Uhuru ni lini umewahi kuona jumla ya Zahanati mpya 564 zinajengwa kwa mpigo tena nchi nzima?

Hebu jiulize tena,tangu tupate Uhuru ni lini umewahi kuona vituo vipya vya Afya 304 vinajengwa kwa Mpigo nchi nzima?

Hebu jiulize zaidi, tangu tupate Uhuru ni lini tuliwahi kujenga hospitali 68 ikiwemo ile ya Mbagala kwa mpigo?

Hebu pitia kwa utulivu hii taarifa toka TAMISEMI, then umsikie mtu anamsema vibaya mama kama hujatamani kufanya ninayotamani Mimi.

=====
HUDUMA ZA AFYA YA MSINGI-TAMISEMI

27. Mheshimiwa Spika
, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais - TAMISEMI iliidhinishiwa Shilingi bilioni 28.20 kupitia ruzuku ya Serikali Kuu.

Fedha hii ni kwaajili ukamilishaji wa ujenzi wa maboma 564 ya Zahanati katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Hadi kufikia Februari 2022, zimepokelewa Shilingi bilioni 23.32 sawa na asilimia 82.69 ya fedha zilizoidhinishwa.

28. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Shilingi bilioni 110.60 ziliidhinishwa kupitia ruzuku ya Serikali Kuu.

Fedha hii ni kwaajili ya kuendeleza na ujenzi wa Vituo vya Afya 304.

Kati ya hivyo, Vituo 52 vilianza kujengwa Mwaka wa Fedha 2019/20.

Jumla ya Vituo 252 vimeanza kujengwa Mwaka wa Fedha 2021/22.

Jumla ya Vituo 18 vimejengwa kwenye Halmashauri zenye Mapato madogo.

Vituo 234 vimejengwa katika Tarafa zisizo kuwa na Vituo vya Afya na Kata za Kimkakati kupitia tozo za miamala ya simu.

Hadi Februari, 2022 Shilingi bilioni 108.05 zimepokelewa sawa na asilimia 97.69 ya fedha zilizoidhinishwa na ujenzi unaendelea.

29. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Serikali ilitenga Shilingi bilioni 81.10.

Fedha hizi ni kwaajili ya kuendelea na ujenzi wa Hospitali 68 .

Hadi Februari, 2022 Shilingi bilioni 66.80 sawa na asilimia 82.36 zilikuwa zimepokelewa na ujenzi upo katika hatua mbalimbali.

NB, Hizi Zahanati 564,Vituo vya Afya 304 na Hospitali 68 vyote hivi vinajengwa na TAMISEMI tu achili mbali vile vinavyojengwa na Wizara ya Afya sijaviorodhesha hapa.
Tozo za kila mwezi hadi sasa ni kiasi gani wamekusanya
 
Rais ni mwakilishi wa wananchi,

Anachofanya ndicho wanachofanya wananchi and verse versa is true,

take it from me
Awamu ya 5 ilijaa propaganda ya 6 nayo inaelekea kule kule .

Awamu ya 5 walisema walifanikiwa kujenga viwanda 100 kila mkoa ila statistically walipobanwa waoneshe ndio tukaletewa hadi sewing na milling machines kuwa ni viwanda.

Awamu hii inajinasibu kuwa imejenga zahanati na madarasa na asifiwaye ni Samia lakini ni majuzi Samia huyo huyo alipokea mkopo wa Covid Relief Fund ndio zikatumika hapo na hatujui riba ya mkopo huo ni kiasi gani.

Sio ajabu kuona lumumba buku saba inaendelea maana imekuwa kila mtawala anaajiri genge la kumsifia mtandaoni .

Ipo siku mtakuja kumsifia humu anaoga mara 5 kwa siku.
 
Back
Top Bottom