Rais Samia anaweza kuanzisha mkoa mpya wa Chato endapo haya yatazingatiwa…

Hongera sana mtoa mada kwa andiko lililo sheheni madini na uchambuzi mpana. Ningekuwa mwalimu wako wa Public Administration, hakika ningekupa 98/💯 sawa na A+.

Hoja za kuanzisha mkowa Chato ni za kipumbafu sana hizi, na yeyote anayeziunga mkono ana akili ndogo kama PIRITONI.

Yaani yule DIKTETA ali- misuse raslimali za nchi kwa kwenda kujenga miundombinu mikubwa kuliko mahitaji halisi ya kitongoji cha Chato, isitoshe kila alichofanya hakikuwa na approval ya Bunge, bado wanataka watushawishi TUBARIKI MAKOSA yake kwa kuipa Chato hadhi ya Mkoa?? They are not serious.

Mungu ametuepushia hiyo DHAHMA kwa kuchukua roho ya mtu mwongo, mwizi na katili na mbinafsi ili tujipange vizuri, kama tutaupa Chato hadhi ya mkoa itakuwa ni KUFURU kwa Mungu wetu.

Ile Chato ni ya kubaki hivyo hivyo kama ilivyobaki GBADOLITE ya Mobutu, ili vizazi vijavyo vije vitambue kuwa tuliwahi tawaliwa na mtu KICHAA kwa miaka 5 na siku 131.
 
Mama Amon,
Unajitaidi sana lakini nafikiri ungefupisha zaidi andiko lako, hakuna mtu mwenye muda was kusoma ‘kitabu’!
 
Jamaa yuko sawa na ameeleza maelezo ya kitalaam. Kwa kifupi sioni haja ya kuanzisha Mkoa wa Chato yale yalikuwa mawazo ya ubinafsi ya huyo mtu aliyetaka kuanzisha Wilaya ya Chato. Hata Wilaya za Katoro na Kisesa ni uharibifu mkubwa wa rasilmali za Serikali.
 
Kwa hiyo kuwepo Wanyonge ndiyo uhalali wa kuwepo Serikali!!!!!

Haswa! Hoja inayoanzia kwenye ibara ya 9(i) iko hivi:

The family is demanded by the natural law. But the state is a natural outgrowth of the family, and becomes necessary for human living when a number of families realize the need of cooperation for their common good. Therefore in these circumstances the state is demanded by the natural law, and is therefore a natural society. This argument can be expressed under the following points:

  1. The most elementary form of society is the family. The family is here taken in the broader sense to mean all blood relatives living together and any servants or others adopted into the household. It can provide for its own welfare in mere daily wants, but it cannot provide for a broader human life. The arts and appliances of civilization could never be developed within one family; for these there is needed the cooperation of many minds and many hands through accumulated generations.
  2. As the family grows, the end it can attain also grows. The children reach maturity and found new families, usually nearby. In several generations a group of families all interrelated live close to one another. Division of labor comes in; people begin to specialize in different kinds of work and to exchange their products.
  3. The interrelated group has become a clan or tribe. A clan is a smaller group with a tradition of descent from a common ancestor. A tribe is a larger group and may be an amalgamation of several clans; at least the blood relationship is not so clear. Some tribes never get beyond the tribal condition, either because of nomadic habits, or because they are wholly occupied in war, or because they show no ingenuity in developing the earth's resources. To form a state a peaceful industrious settlement is necessary: a central village where the people trade.
  4. The village community can supply more of its wants than a single family, but it is not yet self-sufficing. Military organization against enemies from without, economic organization against famine and want, legal organization for settling internal disputes, are still wanting. These things are handled rather arbitrarily by the tribal chief with his council of elders. This chief may be the patriarch or founder of the whole family, or his eldest son, or one of his descendants appointed by him, or one elected by the tribe to be their leader, or one who simply assumes leadership and keeps it by his ability.
  5. From the village community or an aggregate of such villages the state is formed. One village composed of people all descended from the same common ancestor may expand to such a size in such a favorable location, that it is now able to take care of all its needs and has become self-sufficing. More probably several such villages would aggregate together, organize for common defense, mutual trade, and a common legal system. As soon as these things have been determined upon and an authority has been established to enforce them, the state has come into existence.
 
Yani na ukubwa wa Teknolojia bado tunawaza kuongeza watawala ili kutawaliana!?
Nazani tunawaza kinyume, kwa sasa tunatakiwa kupunguza idadi ya watawala na kuongeza viwanda, masoko, shule, nk
 
Unajua lakini kuanzia Mzee RUKHSA hadi dhalimu magufuli ufisadi na wizi wa miaka 36 uliofanywa na hao watu na subordinates wao wa trillions za walipa kodi na hakuna hata mmoja aliyepandishwa kizimbani hivyo wakiendelea kuwa mamilionea na mabilionea huku hao wanyonge wanaojidai kuwatetea wakiishi maisha yaliyojaa ufukara wa kutisha ikiwemo elimu ya hovyo, huduma za afya za hovyo, ajira hakuna, hawana mitaji ya kuanzisha biashara za maana etc hivyo circle ya umaskini wa kutisha kuendelea miaka hadi miaka.
Fungua macho yako uone hali halisi ya nchi yetu na kuelewa hizi sera za KIPUUZI kurudiwa miaka nenda miaka rudi huku kukiwa hakuna TATHMINI yoyote kama sera hizo zina tija yoyote kwa nchi.
Nasubiri TATHMINI kuhusu sera hizo za KIPUUZI kuonyesha mafanikio yake.

Haswa! Hoja inayoanzia kwenye ibara ya 9(i) iko hivi:

The family is demanded by the natural law. But the state is a natural outgrowth of the family, and becomes necessary for human living when a number of families realize the need of cooperation for their common good. Therefore in these circumstances the state is demanded by the natural law, and is therefore a natural society. This argument can be expressed under the following points:

  1. The most elementary form of society is the family. The family is here taken in the broader sense to mean all blood relatives living together and any servants or others adopted into the household. It can provide for its own welfare in mere daily wants, but it cannot provide for a broader human life. The arts and appliances of civilization could never be developed within one family; for these there is needed the cooperation of many minds and many hands through accumulated generations.
  2. As the family grows, the end it can attain also grows. The children reach maturity and found new families, usually nearby. In several generations a group of families all interrelated live close to one another. Division of labor comes in; people begin to specialize in different kinds of work and to exchange their products.
  3. The interrelated group has become a clan or tribe. A clan is a smaller group with a tradition of descent from a common ancestor. A tribe is a larger group and may be an amalgamation of several clans; at least the blood relationship is not so clear. Some tribes never get beyond the tribal condition, either because of nomadic habits, or because they are wholly occupied in war, or because they show no ingenuity in developing the earth's resources. To form a state a peaceful industrious settlement is necessary: a central village where the people trade.
  4. The village community can supply more of its wants than a single family, but it is not yet self-sufficing. Military organization against enemies from without, economic organization against famine and want, legal organization for settling internal disputes, are still wanting. These things are handled rather arbitrarily by the tribal chief with his council of elders. This chief may be the patriarch or founder of the whole family, or his eldest son, or one of his descendants appointed by him, or one elected by the tribe to be their leader, or one who simply assumes leadership and keeps it by his ability.
  5. From the village community or an aggregate of such villages the state is formed. One village composed of people all descended from the same common ancestor may expand to such a size in such a favorable location, that it is now able to take care of all its needs and has become self-sufficing. More probably several such villages would aggregate together, organize for common defense, mutual trade, and a common legal system. As soon as these things have been determined upon and an authority has been established to enforce them, the state has come into existence.
 
View attachment 1807456
Ummy Mwalimu, Waziri wa TAMISEMI akiwa anaangalia muundo wa serilkali ya Tanzania kuanzia Ikulu hadi Vitongojini.

Usuli

Andiko lifuatalo linalo umbo lifuatalo: utangulizi; hoja za kutea pendekezo la kuwepo kwa mkoa mpya wa Chato, wenye kujumisha wilaya za Chato, Bukombe, Kakonko, Biharamulo na Ngara; mapingamizi dhidi ya pendekezo; usanisi wa hoja husika; na hitimisho.

Utangulizi

Kwa mujibu wa tovuti ya Wizara ya TAMISEMI inayoongozwa na Waziri Ummy Mwalimu, Tanzania Bara inayo mikoa 26, wilaya 139, na Halmashauri 185.

Tovuti ya TAMISEMI haitaji idadi ya Kata, Tarafa, Vijiji, Vitongoji wala Mitaa. Hata tovuti za Halmashauri kadhaa zilizounganishwa kwenye tovuti hii hazitaji takwimu sahihi za Kata, Tarafa, Vijiji, Vitongoji.

Lakini, mwezi Oktoba mwaka 2014, Ofisi ya Waziri Mkuu ilitangaza ongezeko la idadi ya kata, vijiji, mitaa na vitongoji nchini vilivyotumika kwa ajili ya uchaguzi serikali za mitaa. Kwa mujibu wa tangazo hilo, Tanzania kuna Kata 3,337, vijiji 12,423, mitaa 3,741 na vitongoji 64,616. Mjadala wa sasa unafanyika katika mazingira haya.

Tangu mjadala kuhusu ombi la kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Chato uanze, tarehe 26 Mei 2021, kuna orodha ndefu ya hoja za kutetea ombi, hoja za kupinga ombi.

Hapa napendekeza kufanya usanisi ya hoja za pande zote mbili, katika mipaka ya taarifa nilizoziokota kutoka mitandao ya kijamii. Nafanya uchambuzi kwa kutumia mawazo ya
Profesa Tibaijuka, Askofu Bagonza, Askofu Niwemugizi, Baraza la Mashauriano la Mkoa wa Geita, Baraza la Madiwani la Geita, na mchambuzi wa masuala ya kisiasa aitwaye Charles Makakala.

Mapendekezo ya waleta hoja (thesis)

Nimebaini hoja nne mpaka sasa:

Mosi, Kuenzi legasia ya hayati Magufuli, kwa kutekeleza miradi ambayo alitamani kuitekeleza wakati wa uhai wake.

Pili, Kupeleka huduma za kiutawala karibu na wananchi wa wilaya za Chato, Bukombe, Kakonko, Biharamulo, Ngara, na baadhi ya Kata za Muleba, zitakazounda mkoa mpya wa Chato.

Tatu, Kuundwa kwa mkoa mpya wa Chato wenye wilaya za Chato, Bukombe, Kakonko, Biharamulo na Ngara utawasaidia wananchi wa wilaya husika kupata nguvu ya pamoja ya kiuchumi wasiyoweza kuwa nayo kwa sasa; tena, bila kuumiza sana mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma itakayomegwa.

Na nne, Kuundwa kwa mkoa mpya wa Chato wenye kumega mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita, kunatokana na matakwa ya kanuni ya utawala kuhusu ukubwa wa wigo wa majukumu ya usimamizi unaoweza kuleta kasi na tija; kwani, uamuzi huu utawatua mzigo mzito wa kusimamia watu wengi na eneo kubwa ulio mikononi mwa ma-RC wa Kagera, Kigoma na Geita.

Mapingamizi dhidi ya mapendekezo (antithesis)

Kama ambavyo kuna mapendekezo manne, kuna mapingamizi manne pia:

Mosi, hoja ya kuenzi legasia ya hayati Magufuli, inapingwa kwa njia hii: Magufuli alikuwa ni binadamu; kila binadamu anayo mapungufu yake; kwa hiyo, matakwa yake yanaweza kuwa na dosari; matakwa yenye dosari hubainika kwa kuchambuliwa moja baada ya jingine; hivyo kila takwa la Magufuli linapaswa kuchunguzwa kivyake kabla ya kutekelezwa.

Pili, hoja ya kupeleka huduma za kiutawala karibu na wananchi wa wilaya za mkoa mpya inapingwa namna hii:

Kwa upande mmoja, Wilaya za Ngara, Biharamulo, na Kakonko ziko umbali wa 300km, 173km na 284km, mtawalia, kutoka makao makuu ya mikoa yake ya sasa.

Na kwa upande mwingine, wilaya ya Chato ambayo inapigiwa chepuo kuwa Makao Makuu ya Mkoa Mpya, iko umbali wa 218km na 130km kutoka Kakonko na Ngara, mtawalia.

Hivyo, kama umbali kati ya makao makuu ya mkoa na wilaya zake ndilo tatizo, basi, Biharamulo au Nyakanazi inapaswa kuwa makao makuu ya mkoa mpya.

Tatu, hoja ya kuwasaidia wananchi wa wilaya za mkoa mpya kupata nguvu ya pamoja ya kiuchumi, ambayo hawawezi kuwa nayo pasipo muungano kama huu, inapingwa kwa njia mbili.

Njia ya kwanza ni ya Bagonza anayesema kuwa mikoa itakayomegwa inaweza kufa kama ambavyo wanawake wenye mimbo iliyotungiwa nje ya mji wa mimba (ectopic pregnancy) hufa. Anaongelea uchumi. Hata hivyo, hoja hii haijaambatana na data za mimba ya kiuchumi inayoongelewa ili tujue ina miezi mingapi. Ni hoja inayoanzia kwenye hisia zaidi na kusahau kukunjua mkeka wa ushahidi.

Njia ya pili, ambayo naiona ikijitokeza kwa njia ya mzunguko katika maandiko ya Tibaijuka, ni kwamba kumega mikoa tajwa kutawafanya baadhi ya watu wanaomiliki ardhi katika mikoa ya sasa kuwa raia wa mikoa miwili. Yeye anayo ardhi kubwa kata ya Kimwani inayotaka kumegwa. Kwa hiyo sehemu ya ardhi yake itakwenda mkoa mpya wa Chato wakati ardhi yake baki itabaki mkoa wa Kagera.

Na nne, hoja kwamba kuundwa kwa mkoa mpya wa Chato kwa kumega mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita, kunatokana na matakwa ya kanuni ya utawala kuhusu ukubwa wa wigo wa majukumu ya usimamizi unaoweza kuleta kasi na tija huko Kagera, Kigoma na Geita, inapingwa kwa kuwa inasahau kuwa inaongeza mzigo wa usimamizi kwa Rais kwa kuongeza mikoa kutoka 26 hadi 27.

Majumuisho ya hoja husika (synthesis)

Baada ya kupitia mapendekezo na mapingamizi hapo juu nimejiuliza swali moja la haraka: Hivi, hayati Magufuli alikuwa anasukumwa na sababu gani nzuri mpaka akaibuka na wazo la kuanzisha mkoa mpya wa Chato?

Hapa tunalazimika kuanzia kwenye hitimisho/pendekezo ili kutafuta sababu za kuhalalisha hitimisho/pendekezo hilo.

Kwa maoni yangu, ili tuweze kugundua sababu iliyoamsukuma hayati Magufuli kuja na wazo hili, tunapaswa kufanya jambo moja:

Ni kuhakikisha kuwa mjadala kuhusu uwezekano wa kuundwa kwa mkoa mpya wa Chato unapaswa kuendelezwa kwa kutumia darubini inayoturuhusu kuona urefu na upana wa majukumu ya ujasiriadola katika ofisi ya Rais.

Kwa hiyo, kama ningekuwa naandika makala hii kwa Kiingereza ningeipa kichwa cha maneno kifuatacho: “On the feasibility of the proposed Chato Region: Framing the debate in terms of vertical and horizontal spans of control in state governance.”

Katika muktadha huu, mpaka sasa, kuna mambo manne ya haraka ambayo nimeyaona.

Kwanza, hoja ya kuenzi legasia ya hayati Magufuli imenyongwa hadi kufa.

Pili, hoja ya kupeleka huduma za kiutawala karibu na wananchi wa wilaya za mkoa mpya imenyongwa hadi kufa.

Tatu, hoja ya kuwasaidia wananchi wa wilaya za mkoa mpya kupata nguvu ya pamoja ya kiuchumi, imenyongwa na inakaribia kufa, na hivyo hakuna haja ya kushughulika nayo.

Na nne, hoja kuhusu madai kwamba mapendekezo ya mkoa mpya wa Chato yanakidhi matakwa ya kanuni ya utawala kuhusu ukubwa wa wigo wa majukumu ya usimamizi unaoweza kuleta kasi na tija, imechinjwa vibaya kwa kutumia kisu butu, na mpaka sasa bado inapumua.

Hoja hii isiposhughulikiwa inaweza kufufuka na kuhalalisha ujio wa mkoa mpya wa Chato. Kwa hiyo, natumia sehemu hii kuichunguza kwa kina.

Maneno “wigo wa majukumu ya usimamizi” yanamaanisha “span of control” kwa Kiingereza. Na kuna aina mbili za wigo wa majukumu ya usimamizi.

Kwanza kuna wigo wa majukumu ya usimamizi kuanzia juu kwenda chini, yaani “vertical span of control.” Hapa tunajiuliza, matakwa ya kanuni ya utawala kuhusu ukubwa wa wigo wa majukumu ya usimamizi unaoweza kuleta kasi na tija, ni kwamba mtendaji awe na ngazi ngapi za utawala chini yake?

Na pili, kuna wigo wa majukumu ya usimamizi kuanzia kushoto kwenda kulia, yaani “horizontal span of control.” Hapa tunajiuliza, matakwa ya kanuni ya utawala kuhusu ukubwa wa wigo wa majukumu ya usimamizi unaoweza kuleta kasi na tija, ni kwamba mtawala awe na watu wangapi chini yake na wenye kuripoti kwake?

Mkuu wa Mkoa ni mteule wa Rais na anamwakilisha Rais. Hivyo, hapa, neno “mtawala” linapaswa kumaanisha Rais, mkuu wa mkoa (RC), mkuu wa wilaya (DC), Mtendaji wa Kata (WEO), Mtendaji wa Kijiji (VEO), na Mtendaji wa Kitongoji (KEO).

Kwa hiyo, maswali makuu mawili yanaibuka: Mosi, Matakwa ya kanuni ya utawala kuhusu umuhimu wa wigo wa majukumu ya usimamizi unaoweza kuleta kasi na tija, ni kwamba RAIS au RC au DC au WEO au VEO au MEO au KEO awe na ngazi ngapi za utawala chini yake?

Na pili, Matakwa ya kanuni ya utawala kuhusu umuhimu wa wigo wa majukumu ya usimamizi unaoweza kuleta kasi na tija, ni kwamba RAIS au RC au DC au WEO au VEO au KEO awe na watu wangapi chini yake na wenye kuripoti kwake?

Maswali haya yanaweza kujibika kwa kutumia ushahidi wa kinadharia (theoretical evidence) au ushahidi mbashara (empirical evidence), au vyote kwa pamoja.

Kwa mujibu wa matini niliyopewa na mwalimu wangu wa somo la Utawala na Uongozi maswali mawili hapo juu yanaweza kujibiwa kwa kutumia fomula za kinadharia zilizobuniwa na kina V.A. Graicunas pamoja na Ralph C. Davis.

Wataalam hawa wanasema kuwa, kwa wastani, ukubwa wa wigo wa majukumu ya usimamizi kuanzia juu kwenda chini ni 5-10. Ni vivyo hivyo kwa ukubwa wa wigo wa majukumu ya usimamizi kuanzia kushoto kwenda kulia.

Kuanzia Ikulu hadi kwa mtendaji wa mtaa ni kama kuna ngazi saba za utawala, yaani: Rais, mkuu wa mkoa (RC), mkuu wa wilaya (DC), Afisa Tarafa (DEO), Mtendaji wa Kata (WEO), Mtendaji wa Kijiji (VEO), Mtendaji wa Mtaa (MEO)/Mtendaji wa Kitongoji (KEO).

Ukubwa wa wigo wa majukumu ya usimamizi kuanzia juu kwenda chini unategemea mambo kadhaa kama vile: umahili wa wasaidizi wa bosi; kiwango cha mahitaji ya weledi wa kupanga kazi kuhusiana na nafasi husika; kiwango cha kasma ya madaraka inayotolewa kwa ngazi za chini na kueleweka katika ngazi hizo; uwepo wa miongozo, miiko na viwango rasmi ya utendaji wa kazi kwa watendaji husika, uwepo wa mazingira yanayoruhusu mawasiliano yenye kasi na tija, na kiwango cha mgawanyo wa majukumu unaohitajika kulingana na utofauti wa kazi zinazofanyika.

Kwa sasa Tanzania Bara inao ma-RC 26, ma-DC 139, ma-WEO 3,337, ma-VEO 12,423, ma-MEO 3,741 na ma-KEO 64,616.

Mchoro: Muundo wa Uongozi wa Serikali ya Tanzania ukionyesha mfumo wa mawasiliano

Kwa hiyo, wigo wa majukumu ya usimamizi uko kama ifuatavyo: Ngazi ya Taifa inasimamia watu 26; kila mkoa unasimamia wastani wa watu 6; kila wilaya inasimamia wastani wa watu 24; kila kata inasimamia wastani wa watu 4; na kila kijiji inasimamia wastani wa watu 6.

Je, kwa mujibu wa takwimu hizi, kanuni ya wigo wa majukumu ya usimamizi kuanzia juu kwenda chini inazingatiwa? Kwa maoni yangu, jawabu ni “ndiyo.”

Na je, kanuni ya wigo wa majukumu ya usimamizi kuanzia kushoto kwenda kulia inazingatiwa? Kwa maoni yangu, jawabu ni “ndiyo” kwa ngazi za mkoa, kata na kijiji. Lakini, jawabu ni “hapana” kwa ngazi za Taifa na wilaya.

Katika ngazi ya wilaya, jawabu laweza kuwa ni kupunguza wigo wa usimamizi kutoka watu 24 hadi tuseme watu 10 kwa kuongeza idadi ya wilaya hadi 350. Wilaya 350 zinamaanisha kuwa wigo wa usimamizi katika ngazi ya mkoa umekuwa watu 14, ambayo ni zaidi ya wastani.

Hii maana yake ni kwamba katika ngazi ya mkoa, tunalazimika kupunguza wigo wa usimamizi uliojitokeza kutoka watu 14 hadi tuseme watu 10 kwa kuongeza mikoa 9, na hivyo kuwa na mikoa 35.

Na katika ngazi ya Taifa tutalazimika kupunguza wigo wa usimamizi uliojitokeza kutoka watu 35 hadi tuseme watu 7 kwa kuunda Kanda 5 za kiserikali.

Kanda hizi tano zinaweza kusimamiwa na Wakuu wa Kanda Watano au Makatibu Wakuu Watano ndani ya TAMISEMI. Nimewahi kusema kuwa TAMISEMI ni dude kubwa lenye kuhitaji makatibu wakuu wengi.

Hitimisho

Kwa mantiki hii basi, Rais Samia anayo hiari katika kuamua kuunda mikoa mipya, ukiwemo mkoa mpya wa Chato, kama ataamua kuzingatia umantiki wa hoja iliyojengwa katika andiko hili.

Kanuni za utawala na uongozi ninazozifahamu zinamruhusu kufanya hivyo. Hata hivyo, kulingana na hoja za wadau nilizoziona, kama mkoa mpya wa Chato utaundwa haiytakuwa sawa kuweka makao yake makuu wilayani Chato.
Siku Magufuli akifufuka anzisheni mkoa wa Chato!
 
Mama Amon,
Unajitaidi sana lakini nafikiri ungefupisha zaidi andiko lako, hakuna mtu mwenye muda was kusoma ‘kitabu’!
Mama Amon umewakomesha vichwa panzi maana umeandika kitaalamu. Kwa mtu professional umavutiwa kusoma mpaka ujue mwishoni conclusion itakuwaje.

Pole santesandy,. hii ndiyo JF nyumbani kwa great thinkers
 
Mtu ambaye amewahi kufanya kampeni za ubunge katika majimbo ya mikoani kama kule Tabora na Shinyanga hatakubaliana na hoja yako ya kupunguza wabunge.

Mtu ambaye amesafiri kwa gari na kuizunguka Tanzania hatakubaliana nawe kuhusu habari ya kupunguza mikoa na wilaya.

Pia, wazo la kupunguza Wizara linahotaji kujengewa hoja. Kwa sababu ya ukubwa wa nchi, muundo wa serikali umeunganisha geographical, functional and matrix departmentation principles.

Ni katika mazingira haya unapaswa uonyeshe ni wapi kupunguzwe na kwa vipi. Kutamka tu hakuna msaada.
Wingi wa viongozi sii utendaji.
 
Mama Amon umewakomesha vichwa panzi maana umeandika kitaalamu. Kwa mtu professional umavutiwa kusoma mpaka ujue mwishoni conclusion itakuwaje.

Pole santesandy,. hii ndiyo JF nyumbani kwa great thinkers
Yeah, mimi sikatai! Ila kama unaweza kuwafikia hata hao vichwa panzi, Kwanini usisamarize ukawafikia?! Kumbuka umeme ule ule wa grid ya taifa unaweza ‘kuu-summarize’ ukachajia simu!
 
Kwa hiyo serikali ya ccm hamuwezi kuwapelekea maendeleo wananchi mpaka muwagawe kimaeneo?!
This is utter nonsense!kama mmeishiwa hivi hebu tuachieni nchi yetu tutafute viongozi wenye kuwaza kidijitali zaidi.
Kama mnatafuta majimbo mapya ya kiuchaguzi si mseme tu!
Mtaigawanyagawanya nchi hadi lini?!mimi nashauri kuanzia mshahara wa rais hadi wabunge ikatwe kodi na mambo yote kama sisi wa chini huku ili huu mzigo wa kodi tubebe wote,mtaacha kuongea mambo ya ajabu ajabu!
...na huko chato hiviiii..mna tunguli yenuu au?!mimi suala la chato(na maeneo ya jirani yake) kupewa mamlaka ya kimkoa silipendi sababu ya uwingi wa warundi na wanyarwanda kule.kwa mantiki za kitamaduni na kiusalama acha chato ibaki Geita..na hata hiyo Geita ingebaki Mwanza tu.Tungerudisha mikoa 25 tu.
Warundi na wanyarwanda ni watu wa kuwa nao makini.Wasipewe nafasi ya kufika ikulu.anayeijua vizuri Afrika ya kati atanielewa.
 
Mh! Msomaji wa kawaida anasoma maneno 200kwa dakika. Hata hivyo Watu wengi si wa somaji wazuri, kasi yao ni ndogo
Na watu Wengine, wengi, siyo wasomaji! Unahitaji uwe na ushawishi mkubwa kumfanya Mtu asome bandiko refu!! Anyway, Mama Amon, amefanya kazi nzuri sana!
 
Mh! Msomaji wa kawaida anasoma maneno 200kwa dakika. Hata hivyo Watu wengi si wa somaji wazuri, kasi yao ni ndogo

Msomaji wa kawaida anayesoma maneno 200 ni yupi huyo?
Uandishi una kanuni zake.
Kubwa ni sita:

  • Audience Analysis
  • Purpose Analysis
  • Content Analysis
  • Organization Analysis
  • Style/Tone Analysis
  • Approach analysis
Baada ya kuziangalizi kanuni hizi ndio urefu wa andiko huamuliwa.
Na urefu wa andiko unamaanisha kuwabagua baadhi ya watu katika hadhira kwa makusudi.
Nimezingatia yote haya.
 
Tatizo la wasomi wengi, hamuwezi kushuka ngazi mje kwenye maisha ya kawaida, Hiyo ni kufeli kuitafsiri elimu iguse watu wa kawaida! Mtu wa kawaida akiangalia tu urefu wa bandiko, anapita!
Hata hao magreat thinkers, anapitia juu juu tu! Nafikiri bado inawezekana kufanya short analysis kwa kupigilia point! Lakini nakubali kwamba Una point ya muhimu!
 
Ma Great thinker wamemuelewa mama amon Ila wale wa la 7 lazima wapate shida
 
Ma Great thinker wamemuelewa mama D Ila wale wa la 7 lazima wapate shida
Mkuu unamuelewa Mama Amon, huku ukimuwaza Mama D!? Kwa taarifa yako mama Amon ni ☝️ of Covid-19, mama d ni CCM vitu maalumu, watu wawili tofauti!
Pia challenge yangu kwa Mama Amon, natamani awafikie na hao wa la 7 ambao ndo majority Tiizii!
 
Back
Top Bottom