Rais Samia anavyotekeleza kwa vitendo sera ya Diplomasia ya Uchumi

Monica Mgeni

Member
Oct 7, 2021
82
134
WhatsApp Image 2022-08-02 at 2.28.00 PM (3).jpeg

Na Chacha Wangwe Jr

Ujio wa Rais wa Zambia nchini Mh.Hakainde Hichelema ni muendelezo wa uthibitisho wa kazi kubwa iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na Rais Samia Suluhu katika kuhakikisha sera ya mambo ya nje ya Tanzania inakuwa yenye tija kwa uchumi na ustawi wa Taifa letu lakini pia katika kumarisha umajumui wa Afrika.

Uhusiano wa Tanzania na Zambia ni aina ya ushirika wa kipekee wenye utajiri wa historia ya udugu halisi wa Kiafrika. Uhusiano uliochochewa na ujasiri wa harakati za kulikomboa Bara la Afrika na sasa wabia imara wa kibiashara; Kwanini Zambia ?

1. uhusiano wa kibiashara- Tanzania na Zambia ni kati ya mataifa yenye Uhusiano imara wa kibiashara wa muda mrefu. Mwaka 2021, Tanzania iliuza bidhaa zenye thamani ya zaidi ya USD Mil 68 nchini Zambia.

2. Miundombinu ya Reli- Tanzania na Zambia ni wabia muhimu katika miundombinu ambapo reli ya TAZARA yenye urefu wa takribani KM 1860 imekuwa kati ya chachu namba moja ya maendeleo na mahusiano ya mataifa haya mawili tangu kipindi cha harakati za kupinga ukoloni.

3. Nishati ya Mafuta - Tanzania na Zambia ni wamiliki wa Bomba la mafuta la TAZAMA linaloanzia katika mitambo ya TIPPER Jijini Dar es salaam hadi Mjini Ndola katika mitambo ya Indeni. Mradi huu ni rasilimali nyingine inayothibitisha umuhimu wa uhusiano wa Tanzania na Zambia.

4. Bandari ya Dar es Salaam - Geografia ya Zambia na mahusiano kati ya nchi hizi mbili imeifanya Bandari ya Dar es salaam kuendelea kuwa mlango wa Taifa hilo linapokuja suala la kusafirisha mizigo na kupokea kupitia bahari ya Hindi. Uhusiano katika eneo hili muhimu kwa manufaa ya Tanzania na Zambia.

5. Uhusiano wa kindugu - Wananchi wa mataifa haya mawili wana muingiliano mkubwa katika nyanja zote za kijamii, kitamaduni na kiuchumi. Mpaka sasa, huhitaji kuwa Visa kusafiri kati ya Tanzania na Zambia, uhusiano huu ni muhimu kwa ustawi wa mataifa haya.

Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kuonyesha uwezo na weledi mkubwa katika kuongoza Taifa hili. Shime watanzania tumuunge mkono na kumpa moyo kwa kazi kubwa anayoifanya.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MMBARIKI RAIS WETU

#SisiTumekubali #Kaziinafanyika
 
Hiyo diplomasia ya uchumi imesaidia nini wakati huu wa mfumuko wa Bei. Nini cha maana kwa watanzania walio wengi na hiyo diplomasia ya uchumi. UJINGA UJINGA TU
 
Na Chacha Wangwe Jr

Ujio wa Rais wa Zambia nchini Mh.Hakainde Hichelema ni muendelezo wa uthibitisho wa kazi kubwa iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na Rais Samia Suluhu katika kuhakikisha sera ya mambo ya nje ya Tanzania inakuwa yenye tija kwa uchumi na ustawi wa Taifa letu lakini pia katika kumarisha umajumui wa Afrika.

Uhusiano wa Tanzania na Zambia ni aina ya ushirika wa kipekee wenye utajiri wa historia ya udugu halisi wa Kiafrika. Uhusiano uliochochewa na ujasiri wa harakati za kulikomboa Bara la Afrika na sasa wabia imara wa kibiashara; Kwanini Zambia ?

1. Uhusiano wa kibiashara- Tanzania na Zambia ni kati ya mataifa yenye Uhusiano imara wa kibiashara wa muda mrefu. Mwaka 2021, Tanzania iliuza bidhaa zenye thamani ya zaidi ya USD Mil 68 nchini Zambia.

2. Miundombinu ya Reli- Tanzania na Zambia ni wabia muhimu katika miundombinu ambapo reli ya TAZARA yenye urefu wa takribani KM 1860 imekuwa kati ya chachu namba moja ya maendeleo na mahusiano ya mataifa haya mawili tangu kipindi cha harakati za kupinga ukoloni.

3. Nishati ya Mafuta - Tanzania na Zambia ni wamiliki wa Bomba la mafuta la TAZAMA linaloanzia katika mitambo ya TIPPER Jijini Dar es salaam hadi Mjini Ndola katika mitambo ya Indeni. Mradi huu ni rasilimali nyingine inayothibitisha umuhimu wa uhusiano wa Tanzania na Zambia.

4. Bandari ya Dar es salaam - Geografia ya Zambia na mahusiano kati ya nchi hizi mbili imeifanya Bandari ya Dar es salaam kuendelea kuwa mlango wa Taifa hilo linapokuja suala la kusafirisha mizigo na kupokea kupitia bahari ya Hindi. Uhusiano katika eneo hili muhimu kwa manufaa ya Tanzania na Zambia.

5. Uhusiano wa kindugu - Wananchi wa mataifa haya mawili wana muingiliano mkubwa katika nyanja zote za kijamii, kitamaduni na kiuchumi. Mpaka sasa, huhitaji kuwa Visa kusafiri kati ya Tanzania na Zambia, uhusiano huu ni muhimu kwa ustawi wa mataifa haya.

Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kuonyesha uwezo na weledi mkubwa katika kuongoza Taifa hili. Shime watanzania tumuunge mkono na kumpa moyo kwa kazi kubwa anayoifanya.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MMBARIKI RAIS WETU

#SisiTumekubali #Kaziinafanyika
 
Sijui ameandika nn, badala kueleza lengo kuu la ujio wa mh. Hichilema yeye analeta historia, jinga sana
 
Huu utaratibu wa fake id unatuharibia sana JF, mtu anapost kwa account moja, ana logout ana post kwa account nyingine...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom