Rais Samia anaupiga mwingi, ameenda kuzindua maghala ya kisasa ya kuhifadhi chakula

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,604
3,846
Uzinduzi wa maghala ya chakula si suluhishi ya kutatua matatizo yanayokumba nchi hivi sasa mfumuko wa bei wa bidhaa mbalimbali ndiyo kitu pekee mama ambacho hivi sasa angekaa na viongozi wake nini wafanye kwa wananchi ili kupunguza ukali wa maisha.

Changamoto ya umeme na maji imekuwa shida kubwa kwa wananchi nachojiuliza serikali baada ya kutangaza kina cha maji kimeshuka kwa hiyo hakuna mbadala wa suluhisho la tatizo hilo, je ni wazi wananchi tunaendelea kuisoma namba

Mama kwa sasa ilitakuwa ajue ni kero zipi wananchi wanalalamikia ndiyo aanze nazo uzinduzi wa maghala hayo ni ziada kwa hali iliyopo nchini nachojiuliza wasaidizi wake sijui huwa wabamwambia nini ! pamoja na miradi mingi kuendelea kutekelezwa angeangalia kero zilizopo hivi sasa.

Huduma mbovu kwenye ofisi za umma vimeshamili kwa sasa kitu kinachoitwa haki katika mahakama zetu ni ndoto ya mchana kweupe, Mama panga mda angalau ukae hata miezi mitatu nchini na kufanya mukoa mbslimbali utajionea madudu yanayoendelea nchini.

Kwa sasa aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa, hadi kupata barua yoyote ya utambulisho kutoka kwa wenye viti wa mitaa ni hela zaidi ya hapo utazungushwa mda wote na kinachofuata nikuchukiwa.
 
Usimlaumu mama, kwa sasa hajui ashike lipi aache lipi. Maana akikaa nchale, akiinuka nchale, akiinama nchale. Imebaki kuwa zumbukuku ulimwengu uko huku.
 
Ninachochukia nikumuita Rais Mama huyo sio mama Yako mbona hamsikii woiii usitafute hela wewe Kaa na ulie ulie hapa
 
Usimlaumu Mama yetu, nyuma yake Kuna watu wameamua au kwa makusudi au ndipo akili zao zinapokomea kumfanya kichekesho!

Hata JPM walimfanya hivi hivi ila kwasababu ya mazingira alimokulia (kushinda polini unachunga n'gombe si mchezo) akaamua kuwa na chanzo kingine cha taarifa na yeye pia akawa anafika mwenyewe!

Kuna wakati hata hotuba zao waliyokuwa wanamuandikia alikataa kuzisoma akawa anaflow na yaliyomo kichwani mwake. Jiulize huyu Waziri wa Nishati ambaye aliwahi kuwa muandishi wa hotuba za rais kwa akili zake hizi utasoma hotuba zake kweli? Mwingine yupo anagoogle picha za viroboto naye unategemea amuelekeze rais kweli.
 
Kuzindua maghala ya kisasa ya hifadhi ya chakula na lenyewe ni jambo muhimu, ingawaje hakutakiwi kupunguza spidi ya kushughulikia na hayo mengine.
 
Baada ya hapo ngonjera za anaupiga mwingi zitaendelea na wakati huo njaa inazidi kunukia kwa wananchi wa kipato cha kawaida
 
Hayo maghala ya chakula yatakuwa na matumizi kweli na hii kampeni ya kuhamasisha wakulima kuuza mazao yao nje ya nchi?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom