SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 43,707
- 60,756
Kwa Hangaya tumepigwa big timeIpo tofauti nimeiona ndani ya miezi saba tangu JPM aage dunia na Rais Samia apewe nchi. Tofauti ya uwezo wa kusikiliza na kufanya maamuzi yenye mizania sahihi. JPM hakubarikiwa busara za utatuzi wa matatizo mengi ya kiutekelezaji japokuwa alikuwa na sifa ya utatuzi huo. Hayati JPM alipenda kuamua suala pale pale jukwaani yaani muda ule ule alipokuwa ndio kwanza kalifahamu.
Rais Samia anaukwepa huu mzigo wa lawama ya wananchi. Hana pupa ya maamuzi na hutumia busara ya kusema 'mimi na wasaidizi wangu hili tunalichukua na tunakwenda kulifanyia kazi'. JPM aliamua muda ule ule, matokeo yake baada ya siku kadhaa kupita yale maamuzi yanakuwa yakifahamika kuwapendelea baadhi ya watu na kuwaumiza wengine. Baada ya siku kadhaa kupita inakuja kujulikana kuwa maamuzi yameegemea upande mmoja badala ya kuwa ni ya haki. Hulka hii ilisababisha baadhi ya watendaji serikalini kumuogopa Hayati JPM.
Na wengine hawakumuogopa bali walianzisha tabia ya kuharibu kazi makusudi ili wamuachie ofisi ateue watu wengine anaoona wanafaa kupewa ofisi. Rais Samia anakubali kutumia muda mrefu kupata utatuzi wa matatizo akijiridhisha na maamuzi yatakayofikiwa baada ya kulitazama suala husika kwa pande zote mbili. Unaweza kudhan ni udhaifu kumbe ni sifa ya uongozi, kuepuka kuleta mifarakano miongoni mwa watu wako wa karibu.
Kwani udhaifu wa tabia ya maamuzi ya jukwaani ni kiongozi kuwa wapendwa zaidi wanaoaminiwa na yeye na wapendwa wa kawaida tu. Watu wasioogopa wala kuona aibu ya kuwaharibia wenzao walio wengi kwa sifa ya muda mfupi tu.
Rais Samia ameonyesha utulivu wa kufanya maamuzi. Hajaonyesha pupa wala hasira pale anapochokozwa, mfano alichokifanya Baba Mchungaji Gwajima kingeweza kabisa kuiamsha hasira ya Samia lakini akatulia kama hakuna linalotokea. Aliweza kuonyesha ukomavu wa kiuongozi kwa kuweza kuistahimili misukosuko ya kisiasa kwa utulivu mkubwa.
Hayati JPM alipendwa kwa kusimamia haki za wananchi lakini upande mwingine wa sifa hiyo ulimpatia maadui haswa miongoni mwa wale waliokwazwa. Rais Samia ameweza kueleweka pale anaposema 'hili tunalichukua'. Hataki kufanya maamuzi halafu yakaleta msingi mbaya (precedent) wa siku zijazo.