Rais Samia anarudi zama za siasa za chuki au anawajibu wanaombipu?

Nilimuomba Mama awe mkali kidogo hili genge la hawa Chadema lina hitaji kwenda nalo kwa akili kubwa kadili wao wanavyoleta uhuni.

Tupo katika mapambano na Covid 19 na wao wamekuwa wakihimiza serikali kuchukua hatua za kupambana na ugonjwa, serikali inawapa maelekezo wanakaidi sasa uhuni unatakiwa kudhibitiwa kwa namna yake.

Safi Mama sana Mama ni mwendo wa long balls sasa hakuna cha mwingi tutapoteza mechi Watanzania.
Kwahiyo Mbowe ni gaidi?
 
Tatizo la msingi la siasa za afrika ni kutoelewa maana ya uchaguzi.ilan na agenda. kwamba kile chama kilichoshindwa ktk uchaguzi ndio kinageuka kuwakilisha umma na kutaka agenda zake zitekelezwe na serikali ya walioshinda. Kwenye kampeni umeahidi katiba ndani ya siku 100, haki, uhuru na demokrasi cha ajabu ilan hii imeshindwa hata kuvuta watu waje kituo cha kupiga kura.. kumbuka kwamba duniani kote dalili kubwa ya upinzan kuchukua dola ni wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
 
Tufute mfumo wa vyama vingi wabaki CCM maana ndo wenye hati miliki ya nchi
Bora wafanye hili, haiwezekani kongamano la masaa machache tu lizuiliwe kwa nguvu kubwa kiasi hiki hadi wengine kubambikiwa kesi za ugaidi.

Huenda kuna kikundi kinaamini hii nchi ni Mali yao hivyo wana haki ya kufanya lolote au wanadhani wao pekee tu ndio wenye uwezo wa kuongoza.
 
We Tanzanian are not ready to tollarate any plot or activities of terrorist under the cover of political freedom.
Mbowe and his fellow alleged to plot and conduct terrorist act, they are criminals like any other criminals, no one is above the laws, he used Political party as an umbrella, he used agenda of demanding new constitution as an umbrella. that man is dangerous.
 
Nilimuona SSH ni mtu wa hovyo tu kama JPM a moment alipoendeleza katazo la mikutano ya hadhara kwa vyama vya upinzani, wakati suala la mikutano ni haki ya kisheria.

Lakini kwa upande mwingine unatarajia nini kwa rais aliyezungukwa na timu ile ile?! Anapokuwa na kikao cha Baraza la Usalama wa Taifa, 99% ya Wajumbe ni wale wale waliokuwepo zama za JPM!!! Watamshauri nini hawa kama sio yale yaleyaliyokuwa yanafanyika zama za aliyemtangulia!!!
 
Asante sana Kwa kuniwakilisha.

Kwa kuongezea tu ni hv:

CHADEMA wanajitahidi sana kucheza generational politics ilhali CCM yangu inafanya siasa za wakati wa nyuma sana.

The fact ni kwamba, siasa za upinzani zitakuja kushinda huko mbele tuendako kwa sababu ndani ya CCM kutatokea hujuma za wenyewe kwa wenyewe as time goes on.

Nijuavyo deep state ni kwamba wana CCM wengi hawaridhishwi na muenendo wa siasa za CCM dhidi ya wapinzani.

Reference nzuri zaidi: The Rise of Kigogo2014 wa twitter
perfect
 
Nilimuona SSH ni mtu wa hovyo tu kama JPM a moment alipoendeleza katazo la mikutano ya hadhara kwa vyama vya upinzani, wakati suala la mikutano ni haki ya kisheria.

Lakini kwa upande mwingine unatarajia nini kwa rais aliyezungukwa na timu ile ile?! Anapokuwa na kikao cha Baraza la Usalama wa Taifa, 99% ya Wajumbe ni wale wale waliokuwepo zama za JPM!!!
hata mimi nikajua utopolo
 
Mama alianza vizuri sana kwa kutaka siasa safi na zenye kuheshimiana. Unfortunately, viongozi wa chadema wakaona kama mama ni mdhaifu na wakaanza kumchokonoa na manono mbovumbovu.
1. Alianza Mbowe kwa kumshurutisha Rais aitishe kikao na wapinzani mapema iwezekenavyo. Hili lilikiwa ni kosa na dharau kwa Rais maana alishasema ataitisha mkutano. Mbowe angeweza kumwambia Rais haja yake privately na siyo kama alivyosema.
2. Mdude baada ya kuachiwa mahakamani tunajua wote alichosema kuhusu Rais akitumia maneno ya kejeli. Hakuna kiongozi yeyote wa Chadema aliyekemea kali ile.
3. Kauli zilizokuwa zinatolewa na viongozi wa chadema akiwemo na Mbowe kwa viongozi wa serikali kabla ya Mkutano wa Mwanza hazikiwa na afya kwa wenye mamlaka.

Chadema bado wana nafasi ya kujisahihisha.
 
Kuna features kadhaa kuhusu matukio makubwa mawili yaliyojiri siku chache zilizopita, la kukamatwa Mheshimiwa Mbowe na viongozi wengine kadhaa wa Chadema, na kabla ya hapo, kukamatwa kwa wafuasi kadhaa wa chama hicho, matukio yaliyojiri huko Mwanza.

Kwanza, hoja za jeshi la polisi na mkuu wa mkoa Mwanza kuzuwia kongamano kwa kigezo cha korona ni utopolo. Hilo halina mjadala.

Pili, kuzuwia kongamano hilo pamoja na lile la awali ni ukiukwaji wa haki za kidemokrasia na kikatiba. Freedom of association sio fadhila bali haki ya msingi kwa kila Mtanzania. Polisi wanapaswa kutoa ulinzi kwenye matukio husika na sio kuwa waamuzi wa endapo shughuli ifanyike au la.

Tatu, kama ilivyokuwa utawala uliopita, kuna double standards, ambapo CCM "wanapeta" tu ilhali ni kosa la jinai kwa Wapinzani japo kijaribu hayohayo CCM wanaruhusiwa kuyafanya.

Nne, kukamatwa kwa Mheshimiwa Mbowe na viongozi wengine wa Chadema kunatia doa taswira nzuri iliyoanza kujengeka kuwa Mama Samia anataka siasa za maelewano badala ya siasa za chuki zilizotawala zama za Mwendazake. Kuachiwa kwa Mdude na kugeuzwa hukumu ya Mbowe ni miongoni mwa ishara zilizotupa matumaini wengi kuhusu Mama Samia.

Tano, siasa za Tanzania na zero-sum game: Unfortunately siasa za Tanzania ni aidha ishinde CCM na Wapinzani wafeli au wapinzani wafaulu na CCM washindwe. Ni vigumu mno kupata suluhu kwenye masuala muhimu ya mustakabali wa kitaifa yanayohitaji mshikamano wa pande zote mbili.

Na ndio maana kwa mazingira ya sasa ni vigumu mno kwa madai ya Katiba mpya kuwa na ufanisi kwa sababu CCM wanajiona washindi wakikwamisha mchakato huo (unfortunately kwa vile ni chama tawala wana uwezo wa kukwamisha) na wanatafsiri kuwa kukwamisha huko ni "kuwapiga bao" Wapinzani

Ufumbuzi: win-win. Katiba ni kwa ajili ya Watanzania wote. Washindi ni Watanzania, sio chama fulani. Ikishindikana, waliofeli ni Watanzania wote, sio kundi fulani.

Sita, Sambamba na hilo, confrontational politics ni ngumu japo wakati mwingine ndio only option. Katika mazingira ya sasa, sidhani kama mkutano kati ya Mama Samia na viongozi wa upinzani utakuwepo tena maana tayari "mstari umechorwa."

Saba, kwa upande mwingine, pengine Mama Samia hajatendewa haki kwenye hilo la mkutano na viongozi wa upinzani. Alikuwa na kila ruhusa ya kutamka kuwa "sihitaji kukutana na Wapinzani" na isingemuathiri kwa lolote, lakini akakubali.

Unfortunately, viongozi wa Chadema wanataka mkutano huo ufanyike mapema kadri iwezekanavyo, which is a valid point. However, kutokana na uzito wa mkutano huo, ni muhimu kuwe na maandalizi ya kutosha. On one side, hakutokuwa na tija endapo mkutano utaishia kuwa fursa ya Mama na wapinzani kunywa kahawa kisha kupiga picha pasipo kujadiliana masuala muhimu kwa taifa letu. On the other side, anayeombwa appointment, hapangiwi wala halazimishwi na mwomba appointment.

Ufumbuzi: kunahitajika ustahimilivu, assuming possibility ya mkutano huo bado ipo, though I highly doubt.

Nane, madai ya katiba mpya ni valid. Katiba Iliyopo ina mapungufu makubwa. Now, whether kinachohitajika ni katiba mpya au marekebisho kwenye katiba iliyopo, that's open to discussion.

However, approach ya kudai katiba ipo a bit flawed. Kws kuzingatia kuwa siasa zetu ni za zero-sum, it is virtually impossible kwa CCM kuridhia mchakato wa Katiba mpya, kwa sababu watakuwa wanajipiga bao. It essentially would fast-track safari ya wao kitoka madarakani.

Tisa, kuna kikwazo cha pili. Ni kwamba utamaduni wa siasa za Tanzania, na hata baadhi ya nchi kubwa, hutegemea sana utashi wa kiongozi aliyepo madarakani. Tumeona zama za Magufuli. Aliyotaka yawe yakawa. Aliyitaka yasiwe hayakuwa. Lakini hata Marekani, utashi wa Obama uliifanya Marekani kuwa "tofauti" na "Marekani ya Trump," na "ya Biden" ni tofauti pia. Na hili ni taifa lenye katiba imara na kongwe.

Ufumbuzi: pamoja na ugumu mwingi, only viable way ya kuwezesha mchakato wa Katiba ni kuhusisha utashi wa Mama Samia, kufanikiwa kuwavuta CCM waone kuwa ni win-win na sio zero-sum game, na suala la katiba kuwa la kitaifa zaidi kuliko "la chama kimoja."

Kumi, no si dhambi kwa Chadema kuongoza harakati za kudai Katiba mpya. However, on on side kuna kikwazo hicho cha CCM, lakini tatizo kubwa zaidi ni kwamba kuna watu watakaokwepa kuunga mkono katiba mpya kwa vile tu ni "sera ya chama flani." Ikumbukwe, zaidi ya nusu ya Watanzania si wafuasi wa chama chochote cha siasa.

Mwisho, ni jawabu la swali lililobeba kichwa cha habari. Je Mama Samia anairudisha Tanzania kwenye zama za siasa za chuki au huu ni utekelezaji wa kile alichotanabaisha mapema kuwa "ukinizingua nitakuzingua"?

Hilo moja, la pili, na linalohitaji tafakuri kubwa ni ukweli mchungu kuwa hata Mama Samia akiamua "kuachana na siasa za kistaarabu" na kuwa full tyrant, hakuna ww kumzuwia. Hakuna aliyeweza kumzuwia Mkapa kuukandamiza upinzani 1995 to 2005. Hakuna aliyeweza kumzuwia Jk kuuma na kupuliza ambapo hadharani alionekana mtu poa kwa wapinzani ilhali faraghani aliwahujumu. Na hakuna kilichoweza kumzuwia Shujaa Mwendazake kufanya siasa za chuki ambapo aliwanyanyasa wapinzani atakavyo.

Ukweli mwingine mchungu ni kwamba tangu jana ni "porojo" tu, Spaces, nk lakini hadi muda huu kinachosubiriwa ni "huruma ya serikali" kuwaachia Mheshimiwa Mbowe na wenzake. Katika mazingira haya ambayo watu ni mahiri sana wa kuongea na kujimwambafai kuliko kutenda, pengine ni muhimu kuwa na Plan B kabla ya kufanya jambo ambalo matokeo yake yanafahamika. Kwa tukio la Mwanza, ilifahamika bayana nini kingetokea, lakini ni wazi there was no plan B. Another zero-sum game?

Kuna video hapa chini inayoeleza hoja hizo zote kwa upana

Huwezi kumtisha rais kwa kisingizio cha demokrasia

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Unadhani armed struggle ndio solution?

La hasha, remember watakaobeba bunduki ni waafrika hawa hawa

Nothing will change except primitive way of solving problems itarudi
Solution ni kurudisha ukoloni tu maana tumeshindwa kujitawala
 
Tindo, binafsi sishabikii chama chochote cha siasa maana siamini katika fikra za wanasiasa oya oya....1995 sikupiga kura maana nilikuwa naijua sinema, 2000 sikupiga kura maana sikuona aliye serious na kuijua sinema, 2005 sikupiga kura, 2010 sikupiga kura, 2015 nilikwenda kupiga kura na kumchagua JPM baada ya kukubaliana na baadhi ya mitizamo yake hasa TZ ya viwanda na undava dhidi ya wapumbavu na wajinga... 2020 sikupiga kura, nilitofautiana mitazamo na JPM dhidi ya approach zake toward Tanzania ya viwanda na ujenzi wa mastructure hovyo hovyo bila kuwa strategically, nilikubaliana naye kw undava wake na ujeuri, maamuzi magumu na kutengeneza dola inayoogopwa na kuheshimika.. 2020 upinzania haukuwa na mgombea serious zaidi ya oya oya na makelele tu...naomba pia nikwambia hili " fanya research yako mwenyewe privately upate kumjua mbowe ni nani na ukirudi nyuma kidogo kwenye ule ugomvi wake na ZZK unaweza kusmell kitu na ukirudi nyuma kidogo ukazama katikati ya mistari ya hutaki unaacha utasmell kitu pia"..

Back to the topic, sio kila anayepingana mtazamo na CDM atakuwa CCM hapana anaweza kuwa chauma, anaweza kuwa ACT anaweza kuwa UDP....na sio kila harakati za CDM lazima ziungwe mkono na kila chama au kila mtu hapana pia...inaonekana pia hujui kwanini ACT walikubaliana na CCM na aliyekuwa nyuma ya makubaliano ni nani, jaribu pia kuunganisha historia ya Zanzibar vs siasa za Zanzibar....Kuna mengi sana bwana tunahitaji kuyafahamu pamoja na kuichukia kwetu CCM....kwa sasa naamini kwenye kuipa pressure CCM ikatuogopa wananchi kuliko kuamini agenda na harakati za wanasiasa..
Natumaini watasoma ili waelewe, nimependa msimamo wako mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom