Rais Samia anao uhalali wa kisiasa, kisheria na kikatiba kushika wadhifa wa Urais

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
✓Wapo wanaopotosha Rais Samia hakupigiwa Kura

✓Wapo wanaopotosha hastahili kugombea tena Urais

✓Wapo wanaopotosha hana uhalali wa kushika wadhifa huo wa Urais hivyo;

SASA TUELEWANE
Kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa tano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli mnamo tarehe 17 Machi, 2021 kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 37(5) Aliyekuwa Makamu wa Rais kwa wakati huo Mheshimiwa SAMIA SULUHU HASSAN ndiye aliyeapa kuongoza nchi kwa nafasi ya Rais na hivyo atakuwa Rais wa sita wa Tanzania.

Ibara hiyo ya 37(5) inasema, "Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano..."

Aidha Ukomo wa madaraka pia umeelekezwa kwa mujibu wa katiba hiyo katika mazingira kama haya ambayo Makamu wa Rais hulazimika kuchukua madaraka ya Urais,

"Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu."

Hivyo, kwa kuzingatia matakwa ya katiba ni wazi Mheshimiwa Samia kwa kuwa ameshika madaraka haya ikiwa ni miezi mitano tu toka awamu ya pili ya Magufuli kuanza, ataongoza nchi kwa takribani miaka minne unusu, hivyo ataruhusiwa kugombea urais mara moja tu kwa maana ya kipindi cha miaka mitano tu.

Kisiasa: Wakati wa Uchaguzi Mkuu karatasi za kura kwa nafasi ya urais zilikuwa na jina na picha za Mgombea Urais na Mgombea Mwenza pamoja na jina na nembo ya Chama Cha siasa kilichodhamini. Kwa mantiki hiyo dhana ya katiba kumpa kipaumbele makamu wa Rais kwenye kuchukua madaraka ya Rais kama ilivyoelezwa kwenye katiba ibara hiyo ya 37(5) ni kwa sababu alifanya kampeni za kuomba kura na wananchi walishiriki kumpigia kura kumuweka madarakani kwa hiyo dhana ya demokrasia ilionekana.


Darasa Huru.
Screenshot_20211212-092754_1.jpg
 
Madudu ni Mengi. Kuongoza watu siyo kazi ndogo. Mama Samia ni mzuri wa sura na roho. Ukiyajua yaliyoko nyuma ya pazia, utampenda tu, kama ambavyo nimeamua kumpenda kwa dhati mama huyu.
 
Hii katiba ina matobo mengi mnoo. Hata huyo alie fariki hakuchaguliwa na wananchi. Alipewa nafasi kwa kuiba. Kusaidiwa na vyombo vya usalama na tume aliyo iweka yeye.

Kama Samia alikuwa mgombea mwenza wa mwizi ina maana na yeye ni mwizi.

Tuna taka katiba mpya. Katiba iliyo halalishwa na wananchi.
 
✓Wapo wanaopotosha Rais Samia hakupigiwa Kura

✓Wapo wanaopotosha hastahili kugombea tena Urais
Sie watanzania wenye uelewa hatuna shida na madaraka yake, mnao pandikiza matatizo ni nyie KWa nyie CCM A,B,C na D

Tunataka katiba mpya itakayozaa Time huru ya uchaguzi, nani mtasimamisha Kama mgombea pitia chama chenu CCM ,hayakuhusu,
 
Back
Top Bottom