Rais Samia anafungua Uhuru wa habari Spika Ndugai anaziba mdomo watoa habari. Hii nchi ina Marais wangapi?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Spika wa Bunge anapotumia Bunge kunyamazisha wanannchi nikinyume kabisa na Katiba. Anapoingilia Uhuru wa vyombo vya habari ni kinyume kabisa na sheria za nchi. Kitendo cha spika kuanza kuvifunga mdomo vyombo vya habari kwa kisingizio kwamba wanaandika na kuripoti habari zakupotosha Ni kinyume kabisa na mamlaka ya kibunge.

Leo spika anapotuhumiwa au Bunge linapokosolewa haiwezi kuingia akilini kwamba Bunge ndipo litakalojipima na kuona linakosolewa na likiona hivyo litawaita wakosoaji nakuwahoji Kisha litatoa maamuzi. Najiuliza haki itapatikana?

Lakini pia zipo mahakama ambazo kazi yake nikusikiliza na kutoa maamuzi kwa mujibu wa sheria. Je Bunge linaweza kutoa adhabu kwa vyombo vya habari au watu binafsi? Hiyo adhabu ni ya aina gani?

Lakini pia, kwanini spika anatumia nguvu kubwa sana kumkwamisha Mhe. Rais kinyume na Rais aliyepita ambaye Spika hajawahi kwa namna yoyote ile kufanya Jambo lenye kiashiria cha kupingana?

Je, ana hasira kwa sababu safari za kuambatana na Rais kila sehemu zimefutwa? Je, leo ndipo ameanza kuwa na wivu na muhimili anaoungoza? Au anampima Mhe. Rais kuona Kama ana nguvu kiasi gani? Au amejiona yeye ni super more than others?

Tukimruhusu Ndugai akalitumia Bunge Kama chombo binafsi nikuruhusu kumkwamisha kwa makusudi Rais aliyepo kinyume kabisa na matendo yake kwa Rais aliyepita.

Tusiogope kukosoa, Bunge aliwezi kutoa adhabu kwa watu au taasisi nyingine. Atumie wanasheria wake kufungua mashauri mahakamani ili atakiwe kuwasilisha ushahidi.
 
Ivi hakuna namna mama Samia anaweza fanya huyo Nduugay akaondolewa kwenye iyo nafasi, then nafasi yake ikachukuliwa na Naibu wake, maana naona kabisa Nduugay anataka kuuchafua utawala wa Rais aliyepo, maana ye bado yupo na fikra za tawala ya kiimla iliyopita,

Mama inabidi afanye umafia fulani uyu mtu apigwe chini
 
Ivi hakuna namna mama Samia anaweza fanya huyo Nduugay akaondolewa kwenye iyo nafasi, then nafasi yake ikachukuliwa na Naibu wake, maana naona kabisa Nduugay anataka kuuchafua utawala wa Rais aliyepo, maana ye bado yupo na fikra za tawala ya kiimla iliyopita,

Mama inabidi afanye umafia fulani uyu mtu apigwe chini
Wabunge wenyewe hawawezi kumuondoa?
 
Hapo ni kuanzisha vuguvugu kupitia wabunge wenyewe (sauti itoke ikulu wademkaji wawe bungeni) hapo atakua kamaliza kazi kama polepole alivyokua ananunua na kuuza watu kama bidhaa ila deep down unaona huo uwezo ni wa juu sana dhidi yake😂😂
 
Nyie walevi mnachekesha kweli.

Vyombo vya habari vinapaswa kuwa na mipaka.

Hauwezi ukawa unapotosha watu na kuzua taharuki halafu uchekewe tu. Kwanza ni utovu wa maadili ya uandishi.

Na huku kwenye mitandao ndio hatari zaidi. Kumejaa walevi na wajuaji wa kila kitu.

Kudhalilisha tu watu, kuchonganisha, kuchochea ghasia, matusi na kila kitu..... ati ndio UHURU!

Uhuru gani wa kilevi namna hiyo?

Unahara tu hovyo mitandaoni, unachafua watu na kuwatweza utu wao! — Ukishughulikiwa unaanza kulia liaa.... oooh nanyanyaswa!!
 
Theoretically separations of power ipo ila deep down mihimili imezidiana “kujichimbia chini”
Executive ina executive orders (rejea maamuzi ya Trump)
Hakuna muhimili zaidi ya mwenzake,ukiona mmoja umezidiwa nguvu ujue top gun wa huo muhimili hajitambui au hajui nguvu aliyokua nayo...executive orders zina mipaka yake na ni almost ineffective on the long run...
 
Kuna maredio wakati mchina anaibuka kwenye teknolojia aliyatengeneza meengi yaakiitwa Supersonic. Radio lina Spika kuuubwa halafu bendi 1.
 
Back
Top Bottom