Poppy Hatonn
JF-Expert Member
- Apr 9, 2021
- 2,080
- 2,688
Mpaka sasa sijaona kosa alilofanya. Mambo yote aliyofanya ni sahihi.
Ni muhimu kwamba usimkejeli rais kwa sababu ya maneno aliyosema huyu au yule.
WEWE ndio uwe mwamuzi. Usikubali mtu akuambie rais hafai. Wasikilize watu wengine lakini uamuzi lazima uwe wako.
Matatizo ya Katiba nadhani rais anaongea kuhusu GHARAMA ya kutengeneza Katiba. Lakini kwa nini watu wasiruhusiwe kuijadili Katiba hayo Mambo ya gharama yakafikiriwa baadaye? Kwa sababu rais amezungumza maneno dhidi ya mjadala wa Katiba. Kwa hiyo analeta taharuki, mpaka abadili usemi wake. Kwa sababu sasa hivi watu wakitaka kuijadili Katiba,P olisi watatafuta kisingizio kuwazuia, kwa sababu rais amekataza.
Kuhusu Mbowe kupelekwa mahakamani, haionekani kama kuna Jambo lolote la maana wanalotaka kulijadili huko mahakamani. Ingekuwa bora kama Mbowe angeachiwa huru sasa hivi. Kama mimi ndio ningekuwa namshauri rais, ningemshauri amwachie huru Mbowe.
Mwisho, ningependa kulaani kile kitendo kilichofanyika Tanga wiki iliyopita. Nimeona ile video. Watu wamemkamata mwizi wa bodaboda, wakamfunga na kamba kwenye miguu, wakamburuza kwenye barabara ya vumbi. Nalaani kile kitendo kwamba ni kibaya sana, siyo kwamba nawaombea dua mbaya waliotenda.
Pia nimpongeze Kamanda Sirro kwa kukemea ubakaji na udhalilishaji alipokwenda Unguja juzi. Kukemea ubakaji na udhalilishaji siyo tu Unguja Ila Tanzania kote.