Rais Samia anafanya kazi kwa weledi sioni upinzani kama una tija kwa sasa

Binafsi nimetoa ushauri ambao utatusaidia kulijenga taifa letu.Rais ameonyesha nia ya kutatua Kero nyingi ambazo hata hao wapinzani walikua wakizipigia kelele sasa kwanini tena apingwe?
Kupingwa ni kawaida tu. Na ndio maana ya siasa za vyama vingi.
Asipingwe yeye nani
 
Habari ndugu Wana JF

Nimekua nikifuatilia habari na matukio yanayoendelea hapa nchini kiukweli nimpongeze Rais wetu Samia kwa kuamua kuongoza nchi kwa kutumia Sheria na utawala bora.

Wote tumeshuhudia akijenga mahusiano mazuri na nchi nyingi huko duniani lakini ameonyesha njia katika kutatua changamoto mbali mbali zilizokua zikiwakibili wafanya biashara nchini pia ameonyesha nia kwenye swala la watumishi wa umma wamepandishwa vyeo wale wanaokidhi vigezo na ameahidi mwakani atawaongeza mishahara, posho na marurupu mengine.

Mpaka hapa ametuonyesha mwanga watanzania yeye ni kiongozi wa namba gani nilichokiona hata wapinzani wamekua washabiki wazuri wa mama yetu mh.Rais kwaio nimeona ni vyema nikawaomba watulie waachane na haya Mambo ya KATIBA ili mama afanye kazi.

Lengo ni kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi ili Taifa liwe na maendeleo katika nyanja zote kwa manufaa ya watu wote na sio chadema kushika dola.

La msingi zaidi ni kuwa ni kwa maneno tu kuwa yeye na bwana yule ni wale wale ila si kwa vitendo!

Wasiojulikana wameyeyuka, shabaya yuko mahali salama, kondakta na wenziwe wanapumulia mashine, Ray C yuko njiani kurejea Njombe, nk nk.

Mola atupe nini tena? Labda katiba mpya!
 
Back
Top Bottom