Rais Samia anafanya kazi kwa weledi sioni upinzani kama una tija kwa sasa

goodlif1600

JF-Expert Member
Jun 1, 2016
794
865
Habari ndugu Wana JF

Nimekua nikifuatilia habari na matukio yanayoendelea hapa nchini kiukweli nimpongeze Rais wetu Samia kwa kuamua kuongoza nchi kwa kutumia Sheria na utawala bora.

Wote tumeshuhudia akijenga mahusiano mazuri na nchi nyingi huko duniani lakini ameonyesha njia katika kutatua changamoto mbali mbali zilizokua zikiwakibili wafanya biashara nchini pia ameonyesha nia kwenye swala la watumishi wa umma wamepandishwa vyeo wale wanaokidhi vigezo na ameahidi mwakani atawaongeza mishahara, posho na marurupu mengine.

Mpaka hapa ametuonyesha mwanga watanzania yeye ni kiongozi wa namba gani nilichokiona hata wapinzani wamekua washabiki wazuri wa mama yetu mh.Rais kwaio nimeona ni vyema nikawaomba watulie waachane na haya Mambo ya KATIBA ili mama afanye kazi.

Lengo ni kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi ili Taifa liwe na maendeleo katika nyanja zote kwa manufaa ya watu wote na sio chadema kushika dola.
 
Shida ya kuishi kwa shemeji kula kulala ndiyo hii unaamua kuanzisha thread hata ya kijinga sababu mtu unakuwa umeshiba sn pasipo kufanya kazi.
 
Sawa Mkuu nimepunguza.

Ila mkuu wakati unaandika usiigize kama hakuna wpinzani.
Wapinzani ni kama hewa lazima wawepo piga ua
Nakubali wapinzani wanatakiwa wawepo lakini wapinge pale Mambo yanapokua yanaenda ndivyo sivyo.lkn kwa Sasa naona mama anafanya kazi yake vizuri sioni haja ya kuja na agenda za kumyumbisha Kama KATIBA MPYA mwacheni Kwanza.

Watanzania kwa sasa tunaitaji maji Safi na salama, Usafiri wa uhakika kwa maana ya miundo mbinu ,elimu Bora, vituo vya afya na hospital za wilaya.kazi iendelee !
 
Nakubali wapinzani wanatakiwa wawepo lakini wapinge pale Mambo yanapokua yanaenda ndivyo sivyo.lkn kwa Sasa naona mama anafanya kazi yake vizuri sioni haja ya kuja na agenda za kumyumbisha Kama KATIBA MPYA mwacheni Kwanza.Watanzania kwa sasa tunaitaji maji Safi na salama, Usafiri wa uhakika kwa maana ya miundo mbinu ,elimu Bora, vituo vya afya na hospital za wilaya.kazi iendelee !
Mama hana muda na hayo ya maji safi, elimu bora, sijui afya mara umeme. Mama ye anataka muwe na hela mfukoni ndo kilikuwa kilio chenu.
 
Marekani ina kila kitu lakini upinzani bado upo tena una nguvu haswa
Upinzani wa marekani usiufananishe na huu wa nchi yetu ule upo strategically na impact yake kwenye nchi yao inaonekana.Sio huu wetu wa kijinga Sana watu wapo kubeza kila kitu kinachofanyika na kupandikiza chuki dhidi ya watu wengine.
 
Upinzani wa marekani usiufananishe na huu wa nchi yetu ule upo strategically na impact yake kwenye nchi yao inaonekana.Sio huu wetu wa kijinga Sana watu wapo kubeza kila kitu kinachofanyika na kupandikiza chuki dhidi ya watu wengine.
Mpuuzi wewe, kama unafanya maendeleo watu si wataona au hawaoni?
 
Mpuuzi wewe, kama unafanya maendeleo watu si wataona au hawaoni?
Binafsi nimetoa ushauri ambao utatusaidia kulijenga taifa letu.Rais ameonyesha nia ya kutatua Kero nyingi ambazo hata hao wapinzani walikua wakizipigia kelele sasa kwanini tena apingwe?
 
Back
Top Bottom