Rais Samia ana viwango vya kimataifa, ni zawadi maalum kwa Watanzania

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,434
12,803
Kama una afya njema ya mwili na akili hebu chukuwa muda wako kumuangalia usoni Mama Samia kwa kutumia macho yako ya nyama na ya rohoni. Bila shaka utagundua kuwa Tanzania na watu wema wote wako salama chini ya uongozi wake. Uhakika wa kuiona kesho yao na hata kuwaona wajukuu wako kabla hujafa umeongezeka sana kwa kila Mtanzania.

Utagundua kuwa Rais Samia anajisikia fedheha kuongoza watu wenye shida zinazozuilika na zinazotatulika. Anajisikia vibaya kuongoza watu wanaolalamika na wasio na matumaini ndani ya nchi yao wenyewe kwa visingizio vya kijinga kabisa (historia, we used to do this, ni dini ile ni kabila lile ni chama kile)

Utamgundua kuwa anataka Tanzania ifananefanane na Ulaya kwenye viwango vya kiuchumi, elimu, afya, huduma za jamii na hata kidemokrasia.

Utamgundua kuwa yeye hataona tabu kuona CCM ikipokezana na Chama kingine kuiongoza Tanzania kwa njia za kidemokrasia za wazi, salama na amani.

Mungu amemleta huyu mama kwa njia zake mwenyewe (kisulisuli) kama zawadi kwetu. Nchi imetulia tuliiii ukiondoa kiangazi, mabadiliko ya hali ya hewa, na athali za vita ya Ukraine na covid 19 ambayo viko juu ya uwezo wake.

Mtamgundua kuwa ni mtu mwenye Nia njema kwa Watanzania WA pande zote za muungano.

Kama tutakuwa na subra na uvumilivu Tanzania itageuka Ulaya ya Africa kidemokrasia, kiuchumi, kimiundombinu, na ustawi wa jamii.

Binafsi Kuna wakati namuangalia na kumsikiliza hadi natokwa machozi. Kinachonitoa machozi ni namna alivyoupata uraisi bila jasho, kukurika, kuiba kura, kudanganya mtu na bila kutarajia na mambo anayoyafanya kama Rais wa ghafla na majaribio kama mwanamke. Sikijua kama atafika miaka 2 bila Tanzania na muungano kutetereka kwakuwa kuna watu wengi wenye uzoefu wa kuongozwa. Wako watu walikuwepo tangu utawala wa wakoloni, Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli, hivyo walitaka Rais ajae afananefanane na hawa kwa hotuba, kwa mavazi, kwa kufoka, kwa kutukana watu, na hata kwa jinsia. Lakini bana kumbe sio hivyo, kila zama na kitabu chake, nchi inasonga mbele kwa kasi kimyakimya.

Nimegundua Sasa kuwa kumbe kiongozi imara sio kufokafoka hadharani, hotuba nyingi na ndefu, vitisho au kuchekacheka kila wakati. Kumbe kiongozi mzuri ni yule mwenye exposures, asiye na makundi, asiye na makambi, mzalendo, mwenye haya, anaejisikia aibu, mwenye hofu ya Mungu, anaeogopa kuchekwa, mzalendo na anaewapanda watu wake na taifa lake na anayependa kuacha alama nzuri kwa taifa lake na duniani. Uongozi sio mbwembwe.

Walah kila mtu atamshangaa kama akifanikiwa kuwa Rais tena 2025-2030.
 
Nakubali, ila kwa Mwigulu kuwa pale ni kikwazo.
Mama amefanya mabadiliko mengi sana kwenye barasa lake, kama Mwigulu angekuwa kikwazo angeshambadilisha. Jamani chukueni muda kumsoma huyu mama. Adui yake namba atatoka CCM TU baaasi. Mama amedharia kuifanya Tanzania iwe mahali ambapo kila mtu mwenye uwezo, hoja na Nia safi aweze kuiongoza Tanzania bila kujali dini, jinsia, Kanda Wala upande gani wa jamhuri. Anayo gundi special ya kuiunganisha nchi. She think globally and acting locally. Nadhani anataka Rais wa Tanzania awe na hadhi sawa na Rais wa ufaransa, Hispania, Uingereza, Italy, Japan au Marekani wanapokutana kwenye majukwaa ya kimataifa. Ni aibu Rais mwizi, corrupt, mwizi wa kura, unaeua watu wako mwenyewe, unaeziba midomo watu wako wasiongee kukaa kwenye meza moja na Rais mwenye heshima kwa watu wake.
 
Nakubaliana na wewe
 
pale kazini siku mkimpata mkurugenzi mpya mzuri ndio mtajua kumbe mlikuwa na mkurugenzi mbaya ila mlikuwa hamjui.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom