Rais Samia ana nia njema, tumuunge mkono tumtie nguvu mama yetu

AUGUSTINO CHIWINGA

JF-Expert Member
Apr 23, 2017
216
1,000
Kasi ya ustawi wa maendeleo na ujenzi wa Taifa imara imeendelea kuonekana katika uongozi huu madhubuti wa Serikali ya awamu ya Sita ya Mama yetu Mh. Rais Samia Suluhu.

Ujenzi wa miundombinu katika sekta za barabara,maji, nishati elimu na afya imeendelea kupamba moto kote nchini.

Kazi hiyo ni ngumu sana ukizingatia jiografia ya ukubwa wa nchi kama Tanzaniai ilivyo. Hivyo kinachohitajika ni watanzania kushikamana pamoja na kumuunga mkono na kumtia nguvu ili aendelee kukamilisha kazi nzuri aliyokwisha kuianza ya ujenzi wa Taifa imara la Tanzania.

Sisi tulio na wananchi huku katika ngazi za chini ni mashuhuda wa jinsi kero sugu za wananchi anavyozitatua kwa viwango na kwa kasi kubwa, anayo dhamira ya dhati na uchungu mkubwa wa kuzishugulikia kero za watanzania.

kazi iendelee hakika Wazalendo wote tunaithamini na kuiona kazi yake kubwa yenye tija na umakini ya kuipaisha juu nchi uetu kimaendeleo.
 

Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
8,178
2,000
Kikubwa awe na maono kama alivyoongea leo, katufurahisha sana. Aongeze kidogo tu ka ukali hizo hela zisije ibwa na wachache.
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,450
2,000
Wewe kumbe bado una hangover ya Mwendazake? Mapambo haya yalikuwa ya Mwendazake sasa unayaleta huku, Rubbish! Kamfuate umpe mapambio huko aliko.
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
35,177
2,000
Kiumbe mwenye sifa ya kuitwa 'Mama' hawezi kuiba kura na kubambikizia watu makesi ya uwongo ya ugaidi.

Yule ni Yezebeli wa Tanzania.Jina 'Mama' liheshimiwe tafadhali.
7654311.png
 

Shehullohi

JF-Expert Member
Jul 21, 2020
2,430
2,000
Leo nimeona glimpse ya hiyo dhamira njema. Sasa tuione kwenye miradi kama ya Bandari ya Bagamoyo kwa kuurejea Mkataba wake na kuondoa vile vipengele vya kishenzi kabisa na ikishindikana kufanya hivyo atafute wawekezaji wengine watakao kubali kuingia mkataba wakunufaisha pande zote ili mradi ule usife na fedha zilizotumika kufidia watu zisipotee bure
 

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
13,395
2,000
Kasi ya ustawi wa maendeleo na ujenzi wa Taifa imara imeendelea kuonekana katika uongozi huu madhubuti wa Serikali ya awamu ya Sita ya Mama yetu Mh. Rais Samiah Suluhu...
Nia peke yake haisaidii. Nafikiri wengi wana nia .... tatizo ni MEANS.....!!
 

Dp800

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,206
2,000
Tumuunge mkono bila kazi kuonekana acheni uduanzi uongozi sio kazi ya kuoneana huruma kama hawezi atoke.

Leo ameanza kujitambua sio lazima awalambe wahisani miguu tutaichangia nchi yetu kwa ajili yetu na sio kwa hisani yao.

Kwanza aachane na upuuzi wa corona maana mpango wake ni kutufanya kuwa wategemezi na sio vinginevyo then tukusanye Kodi kwa kuwawezesha vijana wetu kufanya kazi.

Wahisani ukiwaendekeza watakupaka mavi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom