Rais Samia amteua Mavere Tukai kuwa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD)

Kwanza ni mpongeze kwa uteuzi!
Lakini lazima watu wajue kuwa tatizo kubwa la MSD si kupeleka dawa bali kuna shida kubwa kwenye upatikanaji wa dawa na kuna shida kubwa kwenye ma hospitali yetu mengi hayana uwezo wa kununua dawa kwa wakati maana hawana pesa!

Lazima tujue kuwa MSD haipeleki dawa bure kabisa kwa hiyo lazima hospitali inunue dawa kutoka MSD ndio wapeleke tena kwa order...kwa hiyo kwanza lazima tujue shida kubwa ya mahospitali yetu hawan uwezo wa kununua dawa ndio maana kelele nyingi za ukosefu wa dawa mahopitalini unazisikia maana nyingi zinakuwa hazina hela ya kutoa order ya dawa kwa wakati!

Pia hata MSD yenyewe haina budget ya kutosha kabisa kwa hiyo wanaweza kuwa na order nyingi sana kutoka kwenye mahospitali lakini mfumo unaonesha hakuna dawa husika..na shida inakuwa ni pesa za kuagiza dawa kwa wakati lazima serikali ihakikishe MSD inajitosheleza kabisa ki budget kusiwepo na delay ya kupata dawa!

Kinyume haya tutakuwa watu wa kubadilisha watu tuu bila kujua tatizo ni nini! Hata akiwekwa malaika hapo MSD kama hakuna dawa za kutosha na Mahospitali kama hayana pesa za kununua dawa lazima ataonekana hafanyi kazi maana matokeo yatakuwa tofauti na matarajio yetu!

Kwa hiyo lazima tujue tatizo ni nini kwenye swala la dawa ...je mahospitali yetu yasiyo na uwezo wa kununua dawa kwa wakati kutokana na kipato chao tutawafanya nini? Au mwisho wa siku watu wakikosa dawa lawama kwa MSD wakati MSD hawatoi dawa bure......

Pia lazima tujiulize hawa MSD wanapewa pesa zote kwa wakati? Ni kweli dawa zote zinakuwepo na zote zimeagizwa? MSD wanapewa hela yote kwa wakati?

Ni lazima tujue tatizo liko wapi na tumelitatua vipi?
 
Huu ni uchawa mwingine. Unashauri O/S notification badala ya kushauri kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya. Yaani aboreshe kuonesha tatizo na si kutatua tatizo. Acheni wizi basi.
Wewe ndo unadhani tunaishi kwenye perfect world siyo leo hata angekuja malaika MSD haiwezi ku-attain 100% Fill Rate kwa wateja wake.Uki-Refer recent CAG report,Business Plan ya MSD ili-target stock availability ya 75%,na wakaweza ku-attain only 34% ambayo CAG amei-query.Sasa hata MSD inge-perform to its maximum target ya 75% unategemea hiyo balance ya 25% ingekuwa complemented vipi?
 
Kama MSD ingeattain hiyo 75% fill rate, kelele za OS zingepotea mno. Shida kubwa ni kwenye tertiary hospitals na maoteo ya nchi hayapo realistic. Tuki quantify vizuri na procurement process zikaboreshwa OS itakuwa ni kidogo mno.
Juzi tumeona wabunge wakiongea uongo juu ya utaalamu.
Wanasahau MSD ilinyimwa fedha for 18 months kwahiyo HFs zikawa zinapewa buffer stock, then covid19 ikaibuka.
Sasa siasa za kijinga pia zijitenge na MSD
 
Huyu ndugu Mavere Tukai ni "kichwa" haswaa.....

Ni "pharmaceutical management specialist"....

Jamaa yuko FOCUSED na DETERMINED sana.....

Alikuwa pale USAID....wamarekani wanamfahamu kwa uwezo mkubwa alionao....watammiss sana.....

Imefika muda atutumikie katika MSD.....

Kila la heri kwake kamarada Mavere Tukai ,amen🙏

#Siempre JMT🙏
#YetzerHatov🙏
Wewe jamaa umesomea uchawa? Wewe ni kichwa wa uchawa na Hakika kazi ya uchawa unaitendea haki kabisa
 
Ni mtaalamu anatokea USAID kule waajiri vichwa tu tena vikali vyenye uwezo mkubwa wa creativity innovation nk

Professional certification yake umeiona ?ni ya kimataifa siyo ya Tanzania .Tanzania wapo wachache sana professionals wenye international certification
Mkuu, nani alikudanganya USAID wanaajiri vichwa? Nina ndugu zangu kibao wanafanya kazi USAID na international organization nyingine. Hakuna cha kichwa wala nini.
 
Huyu ndugu Mavere Tukai ni "kichwa" haswaa.....

Ni "pharmaceutical management specialist"....

Jamaa yuko FOCUSED na DETERMINED sana.....

Alikuwa pale USAID....wamarekani wanamfahamu kwa uwezo mkubwa alionao....watammiss sana.....

Imefika muda atutumikie katika MSD.....

Kila la heri kwake kamarada Mavere Tukai ,amen

#Siempre JMT
#YetzerHatov
What is kichwa?
 
Raymond Mndolwa aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Operesheni za Mikoa pale NHC. Kumbukumbu zinaonyesha alisimamishwa kazi kwa tuhuma za ufisadi na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Mhe Lukuvi.

Sasa leo tunaona amepata uteuzi wa Rais. Je zile tuhuma zilikuwa ni malicious!?
Kusimamishwa sio dhambi isiyofutika boss, aliyemsimamisha hakuwa Mungu ni binadamu. Kwa Mungu kwenye dhambi anazifuta
 
Wewe ndo unadhani tunaishi kwenye perfect world siyo leo hata angekuja malaika MSD haiwezi ku-attain 100% Fill Rate kwa wateja wake.Uki-Refer recent CAG report,Business Plan ya MSD ili-target stock availability ya 75%,na wakaweza ku-attain only 34% ambayo CAG amei-query.Sasa hata MSD inge-perform to its maximum target ya 75% unategemea hiyo balance ya 25% ingekuwa complemented vipi?
CAG naye awe anaimulika serikali je ilipeleka msd pesa ya kununua dawa Kama ilivyopitishwa bajeti ya dawa bungeni? Sio unampima ili umdhalilishe ikiwa unaelewa serikali imepeleka pesa 40% na madeni ya nyuma kibao hujalipa alafu unataka matokeo yawe 100 kwa 100.
CAG nao huwa vilaza msiwashabikie muda wote Kuna baadhi ya maeneo hawasaidii nchi zaidi ya sifa za kijinga na mbwembwe kwenye ripoti zao
 
Back
Top Bottom