Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Sabaya amesimamishwa kazi sababu ya tuhuma. Na wanaofurahia kusimamishwa kwake kazi ni wanachama wa CHADEMA. Watu wenye upeo wa kufikiri tunajiuliza maswali mengi na machache kati ya hayo ni haya :
1- tuhuma zinazomkabili Sabaya sio za leo wala jana, ni tuhuma za kuanzia mwaka jana kurudi nyuma. Sasa je, wakati Sabaya anatuhumiwa, huyu Madam SSH yeye hakuwa Makamu wa Rais? Alichukua hatua zipi dhidi ya Sabaya kwa nafasi aliyokuwa nayo?
2- Madam SSH akisema kipindi hicho hakuwa na sauti, Je, sasa hivi akiwa kama Rais yuko tayari kuchukua hatua dhidi ya kila tuhuma zilizokuwa zikielekezwa kwa viongozi au Serikali anayoiongoza sasa hivi?
Hata chama chake CCM kinatuhumiwa sana kwa udanganyifu na wizi wa kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Je, Madam SSH yuko tayari kufanyia kazi hizo tuhuma kwa kuruhusu uchunguzi huru dhidi ya chama chake na ikiwa itathibitika kuwa kweli waliiba kura, Je, atakuwa tayari kujiuzulu na kupisha uchaguzi mwingine ufanyike?
3- Spika wa Bunge, Job Ndugai anatuhumiwa sana kuisigina katiba ya nchi, Je, Madam SSH yuko tayari kulivunja Bunge na kuitisha uchaguzi mwingine maana mamlaka hayo anayo.
4- Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatuhumiwa kudhulumu haki za kuishi za baadhi ya watu, Je, Madam SSH yupo tayari kupisha uchunguzi huru dhidi ya Makonda?
5- Usalama wa Taifa wanatuhumiwa kuhusika na tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu, Je, Madam SSH yupo tayari kuruhu FBI wafanye uchunguzi wao kama walivyotaka kufanya baada ya tukio na kuzuiliwa?
Ikiwa Madam anasikiliza tuhuma za mitandaoni, Je, sio sahihi kwa yeye kusikiliza na kuchukua maamuzi dhidi ya tuhuma hizo nilizoziainisha hapo juu??

Na hapo sijataja tuhuma za utekaji watu, kupotea kwa baadhi ya watu kama Azory n.k.
Au Watanzania mnapenda sana kushabikia vitu pasipo kufikiri kwa kina? Hamjui kwamba wanasiasa wote wamejaa unafiki?
Madam SSH yeye siyo MALAIKA, yeye ni Mwanadamu tena mwanasiasa. Hana tofauti na aina za wanasiasa tuwajuao.
Huna ujualo mkuu kaa kwa kutulia mjomba wa sabaya wewe

Huna akili hata kidogo.kwani samia anaishi ndani ya kibuyu kiasi kwamba hana analosikia au kuona kwa macho yake? Hilo bichwa tumia kufikiri siyo kufugia nywele.

Acha useng. e wewe
Kwahiyo unaona huu ni umbea
Kumbuka serikali ni kwa ajili ya watu

Unahisi kakosea kukutoa

Kasimamishwa kazi kupisha uchunguzi kama hana hatia siatarudishwa kwenyekiti chake? Nchi hii ni yetu wote hakuna mwenye uhuru wa kufanya atakalo. Haki itendeke.

Kuna clip toka hotel ya Mbowe akiwa na mabunduki akitesa wafanyakazi na kufanya uahlifu.
By the way source yoyote ya information kama wewe ni kiongozi mzuri ifanyie kazi. Mitandaoni mbona mnawafunga watu kwa taarifa za mitandaoni?

Genge la chato akili zenu bana
Kwa hiyo unasema rais hana vyanzo vya habari kuyajua majambazi?

Hadi lile genge lote la kabila letu pendwa lisambaratike lote. Kwani hamjijui?

CCM wanajua Watanzania wengi wamejeruhiwa na Mwendazake, kilichopo saizi wanawaponya majeraha...2025 wanakuja na gia nyingine.

Kwa Hali hii ccm itatawala miaka mingi ijayo, maana wanajua kula na vipofu.

Ni Jambo kua na rais anayesikiliza,

Mama katumia busara Sana, kasema kasimamishwa kupisha uchunguzi.

Hajafukuzwa, atafukuzwa zikithibitishwa tuhuma zake.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni Jambo zuri Sana mama anafanya, kiongozi ni kusikiliza...
 
Dc sabaya ni mwiba kwa ufisadi na kada mzuri wa ccm. Kutokana na uongozi wake hai ccm iliweza kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi uliyopita ubunge na udiwani.
Kumsimamisha eti kwa uchunguzi ni kufanyia kazi madai ya uzushi ya wapinzani. Hili linaleta wasiwadi mkubwa kama kweli mama anafuata njia ya kimapinduzi ya jpm au anasikiliza kelele na uzushi wa maliberali vibaraka wa ubeberu.
uyo jpmm ni keng.e mmoja Kama wewe
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili kuanzia leo, Mei 13, 2021

Aidha, Rais Samia amefanya teuzi za Viongozi mbalimbali ambao uteuzi wao unaanza leo

Habari ndo hiyo

Nawatakia Eid Njema.

====
Alizaliwa mwaka 1980 katika mkoa wa Arusha

Hayati John Pombe Magufuli tarehe 28 Julai, 2018 alimteua Sabaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai

CHAMA: CCM

#NA SASA KAZI IMEANZA#


TAARIFA ZA ELIMU YAKE


SVISC. MASSACHUSET UNIVERSITY USA

BSC.ED ST JOHN UNIVERSITY DODOMA

UNED: SINIOUR SIX –BUGEMA HIGH SCHOOL-UGANDA.

FORM IV: IKIZU SEC SCHOOL

STD VII: SAMBASHA PRIMARY SCHOOL.

OTHERS: IST: PRESIDENT ST. JOHN’S UNIVERSITY DODOMA 2007.

CHAPEL PREFECT BUGEMA HIGH SCHOOL UGANDA.

CEO: TANZANIA YOUTH DEVELOPMENT CENTRE

SEMINARS BSYMPOSIUM: S. KOREA YOUTH CONFERENCE ,SOUL

YOUTH SUMMIT COMMISSIONED BY HON. PINDA TYDC:2010

CAPRIPOINT YOUTH EMPOWERMENT 2014

CV nyepesi kama uji HALAFU kwa taarifa St.Johns University of Tanzania hakumaliza alikamatwa na sups aka DJ. Get that fact loud and clear. Hiyo ya juu yake ni uchafu gani hapo Massachusetts?
 
What a beautiful news!!!!
Mungu anaendelea kusafisha SUKUMA GANG
Hapo kwenye Sukuma Gang unakosea.

Wasukuma wengi ninaowafahamu hawana fikra za kudhuru. Hivyo neno hilo ni kama blanket linawapa picha isiyo yao.
 
Halafu nyie mnaojifanya ooh sijui subirin mbele Rais sijui atamuweka tena banaa weee tusidiscuss ya huko cha muhimu for now He is no longer DC hayo mengine yakifika tutajua...acheni kujitia utabiri mwingi 🚮🚮
 
Hopeless kabisa wewe. unafikiri wanaotoa taarifa mitandaoni ni ghost ama? mbona wewe unamshauri Mh Rais kwa kutumia mtandao?
huyo kiongozi zaidi kachukiwa na wapinzani kwa sehemu kubwa na wapinzani siku zote hawajawahi mkubali mtu ambae ni mwiba kwao hata kama anasimamia sheria
 
Ukizingua Mama anakuzingua, haya ndo masalia ya Bwana yule yaliyozidi kujimwambafai hata katika awamu ya sita! Mama Hongera, hii inaonesha jinsi ulivyo msikivu tofauti na Bwana Yule!

Mama Samia Suluhu Hassan, Mungu akupe maisha marefu
Bei wetu mama Samia
 
Back
Top Bottom