Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Bwana mdogo Sabaya Hakujifunza kwa pacha mwenzake Paul Makonda Baada ya kutumbuliwa kwake namna gani jamii ilimpokea.
Nilishangaa sana Juzi alipokuwa akihojiwa kwenye tawi la ccm ( clouds media) alikuwa anaongea mpaka anawapindukia watangazaji kama yuko sitting room alitamba zaid kiasi cha kum stopisha Kija kuwa asiwe na haraka yaani alikuwa na confidence ya hovyo sana.
Na ili nililitegemea maana malalamiko yalikuwa mengi mno juu yake.
Swala la kupisha uchunguzi dhidi yake ni kumtafutia sababu ya kumbananisha kwenye kona.


Mungu ni mwema siku zote.
Sema hivi sio kumtafutia sababu,sababu zipo tena zakutosha Sana.
 
Miaka 35 ni sahihi ,kipind anasoma Ikizu sekondari akiwa form four mi nilikuwa form one mwaka 2006...jamaa alikuwa mbabe Sana , alikuwa na kundi la wannyanyua vyuma , yeye alikuwa wa mwisho kuingia dining hall na kundi lake na haiwezekani kuruhusiwa Kula bila yeye na kundi lake hawajafika , ni mtu wa system pia , Baba yake by that time alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Serengeti kama sikosei
Kumbe huu UJINGA wake aliuanza muda mrefu toka akiwa shule. Sijafaham Vetting ya kuwapata viongozi wa Umma inakuwa vipi mpaka watu kama hawa wanapenya
 
Haya.
Ndo maana nimewaambia bakisheni akiba ya maneno..
Kusimamishwa.
Kutenguliwa haya NI MANENO mawili tofauti.
Muwe mnaelewa.
Mama anasoma comments zoteeee KWA furaha hii ya wananchi hawez mrudisha
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili kuanzia leo, Mei 13, 2021

Aidha, Rais Samia amefanya teuzi za Viongozi mbalimbali ambao uteuzi wao unaanza leo

Habari ndo hiyo

Nawatakia Eid Njema.

====
Alizaliwa mwaka 1980 katika mkoa wa Arusha

Hayati John Pombe Magufuli tarehe 28 Julai, 2018 alimteua Sabaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai

CHAMA: CCM

#NA SASA KAZI IMEANZA#


TAARIFA ZA ELIMU YAKE


SVISC. MASSACHUSET UNIVERSITY USA

BSC.ED ST JOHN UNIVERSITY DODOMA

UNED: SINIOUR SIX –BUGEMA HIGH SCHOOL-UGANDA.

FORM IV: IKIZU SEC SCHOOL

STD VII: SAMBASHA PRIMARY SCHOOL.

OTHERS: IST: PRESIDENT ST. JOHN’S UNIVERSITY DODOMA 2007.

CHAPEL PREFECT BUGEMA HIGH SCHOOL UGANDA.

CEO: TANZANIA YOUTH DEVELOPMENT CENTRE

SEMINARS BSYMPOSIUM: S. KOREA YOUTH CONFERENCE ,SOUL

YOUTH SUMMIT COMMISSIONED BY HON. PINDA TYDC:2010

CAPRIPOINT YOUTH EMPOWERMENT 2014




 
Amemsimamisha kupisha uchunguzi, hajamfukuza kazi. Kuna ubaya kuchunguza tuhuma za kiongozi wa umma? Unadhani Rais hana vyanzo vyake vya taarifa?
Na wewe unadhani mpaka amsimamishe Rais hakuwa na hizo taarifa kutoka katika vyanzo vyake?hapo kamuweka pembeni jela inafuatia
 
Hii ni awamu ya 6 bwashee.

Mabadiliko makubwa yanakuja!
 
Wewe sio wa kutufundisha! Maisha ni haya haya! Tulia, anachunguzwa sio ametengukiwa tu, usitufanye wakinga

Jamani hivi yule wa Mbeya na yule wa Iringa wapo kweli !!!???

Maana tangu "MWANAKWENDA ZAKE na AENDE" alipoondoka kama siwasikii tena naona wana act low profile sana

... au ilikua nguvu ya Azam Cola gesi imeisha na wao chali pressure zinapanda na kushuka

Ama kweli kila zama na Nabii wake !!!
Wameufyataaaa thubutu walete ngebe watu wawasagie kunguni ....🤣🤣
 
88 Reactions
Reply
Back
Top Bottom