Rais Samia amewezaje kufanya haya yaliyowashinda Marais wote?

1.Mi nipo Buswelu kona. Wameondoa vibanda vya mboga mboga wamepeleka Wilayani.
Nauli ya kutoka hapa mpaka wilayani ni elfu 1 kwenda na kurudi.

2.Machinga wa Makoroboi wamepelekwa Igogo. Toka mjini mpaka Igogo ni mia nane kwenda na kurudi.
Huoni hiyo?
Kwahiyo huko kote sio karibu na makazi ya watu?
 
Nipo jijini mwanza kiukweli mji unapendeza. Nimepita maeneo karibia yote makoroboi, nyasaka, nyamhongolo, buhongwa. Dah!

Siamini machinga wote wamehama tena wenyewe kwa mikono Yao, wamebomoa wenyewe bila vurugu zozote.

Mama Samia amewezaje ilihali watangulizi wake wote walishindwa na walipojaribu lilikuwa ni bomu hatari Sana...#raissamiaisaluteyou

Hizi ni picha nilizopiga maeneo ya buhongwa ambapo lilikuwa ni eneo hatari Sana kuwaondoa machinga!

View attachment 2002214

View attachment 2002215
Siri ya mafanikio ya Rais Samia ni moja tu

1. Tumia akili zaidi kuliko nguvu

2. Tumia nguvu pale tu zinapohitajika
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom