#COVID19 Rais Samia amewataka viongozi wa dini kutoa elimu kwa waumini juu ya umuhimu wa kupata chanjo ya uviko19

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa dini kutoa elimu kwa waumini juu ya umuhimu wa kupata chanjo ya uviko – 19 pamoja na kushiriki katika sensa inayotarajiwa kuanza mwaka 2022.

“Niwaombe viongozi wa dini kujumuisha masuala ya sensa kwenye mahubiri yenu, kawaida serikali ikitoa matamko ya sera anatokea kiongozi wa dini kwenda kupinga na bado maamrisho kwenye kitabu chake hayamtumi hivyo, pia mpige kampeni ya kutosha kwenye suala la corona,”

“Ukweli ni kwamba chanjo zinapunguza vifo lakini pia inapunguza makali ya maumivu ya ugonjwa wa corona, wale wambao hamjawahi kupata maumivu ya lile gonjwa hamuwezi kuelewa lakini wale ambao yameshawafika wanaelewa,”

“Niwaombe viongozi wa dini muwaelimishi waumini ili wakubali kupata chanjo ya corona, tumesema sio lazima kuchanja lakini wengine hawajui akichanja anapata nini na asipofanya hivyo anakosa nini,”
 
Mungu anawaona!! Namshukuru sana Mungu kwa kuwa hii chanjo ni hiari!! Afadhari nife kuliko kuchanjwa kwa lazima!! Ila angalizo ni kwamba kinachoagizwa hadharani kuwa chanjo ni hiari iwe hivyo kweli!! Isije ikawa huko nyuma ya pazia viongozi wanaagizwa kulazimisha watu chanjo!! Na viongozi wasitishwe kuwa nafasi zao ziko hatarini kama maeneo yao watu wengi wataamua kutumia hiari yao kutokuchanja!! Wafanyakazi wa serikali wasitishiwe nafasi zao kama wataamua kutumia hiari yao na kuchagua kutokuchanja!! Mungu anawaona!! Niwashukuru sana viongozi wa kitaifa kuamua kufanya jambo hili kuwa la hiari.
 
Chanjo ya CORONA itakukinga na ugonjwa, kulazwa na hatari ya kifo. Fanya uamuzi wa kupata chanjo. Wahi sasa, okoa maisha. Kwa msaada zaidi piga 199 bila malipo.
 
Chanjo ya CORONA itakukinga na ugonjwa, kulazwa na hatari ya kifo. Fanya uamuzi wa kupata chanjo. Wahi sasa, okoa maisha. Kwa msaada zaidi piga 199 bila malipo.
Nilijua ni TIGO wamenitumia huo ujinga.

Nikawapandia hewan, Nmewatapikiaaa


Akaanza kuniambia, sio sisi. Ni serikali wenyeweee, sisi jumbe zetu lazima ziwe na neno TIGO.
 
Mungu anawaona!! Namshukuru sana Mungu kwa kuwa hii chanjo ni hiari!! Afadhari nife kuliko kuchanjwa kwa lazima!! Ila angalizo ni kwamba kinachoagizwa hadharani kuwa chanjo ni hiari iwe hivyo kweli!...
sawa tu hata kuvaa kondomu ni hiyari yako.

ila kazi kwako, ukiukwaa ukimwi utalia wewe na familia yako.

chanja kwa uhai wako.
 
Hiyo ni ngumu!! Kilicho rahisi ni kuwaambia waumini kuwa chanjo ni hiari!! Ukikubali nenda kachanje! Na hilo viongozi wote wa dini wamekuwa waaminifu kulisema!!

Viongozi wa djni hawawezi kuwa wadhamini wa usalama wa chanjo kitu ambacho hata watengenezaji wa chanjo wamegoma kudhamini usalama wa chanjo!!

Hata serikali imegoma kudhamini usalama wa chanjo!! Kilichopo ni "chanja at your own risk"!!! Tena unaambiwa unasaini kabisa kana kwamba unaingia kwenye chumba cha upasuaji mkubwa !!
 
Amesahau kuwaambia wahubiri haki za wauminiwao ambazo zinavunjwa na genge la polisi
 
"wale ambao hamjawahi kupata maumivu ya lile gonjwa hamuwezi kuelewa lakini wale ambao yameshawafika wanaelewa"Hapa ameongea vizuri sana...
 
Chanjo ya CORONA itakukinga na ugonjwa, kulazwa na hatari ya kifo. Fanya uamuzi wa kupata chanjo. Wahi sasa, okoa maisha. Kwa msaada zaidi piga 199 bila malipo.
Huo ndio ushauri mzuri!! Tatizo lake tu ni kuwa hausemi chochote juu ya usalama wa chanjo na madhara ya chanjo ya muda mrefu! Ungekuwa mkweli/honest ungesema:

Tunaamini ni salama japo haujafanyika utafiti wa muda mrefu kuthibitisha usalama wa chanjo au athari za chanjo za muda mrefu.

Hii taarifa ni muhimu ili mtu anapoamua kuchanja ajue kuwa kuna kiasi cha risk fulani anachochukua akiamua kuchanja!!
 
Iwe hivi,
Wasiotaka kuchanja watengwe mbali ili wasiendelee kuukomaza huu ugonjwa,
Lengo ni kuutokomeza wote, sasa kama wengine wanaulea kweli utaisha?
 
Back
Top Bottom