Rais Samia ameua Mhimili wa Bunge, bado kumalizia wa Mahakama. Haya si ya kushangilia

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,373
73,975
Haya yote yanayotokea na kushangiliwa hayana lolote katika ustawi wa Taifa hili.

Tunakwenda kuangamia. Jana/Juzi kitendo cha kumkemea Ndugai hadharani akajiuzulu, maana yake Bunge limesalimu amri kwa Executive. Kinachofuata ni kumalizia Mahakama maana alishaianza kuiua.

Matokeao yake unaweza usiyaone leo, lakini inaweza kuleta hata vita ya wenyewe kwa wenyewe baada ya kuwepo makundi ya KUONEA na KUONEWA.

Kuna makundi yatakataa kuonewa na yataungwa mkono na mataifa yanayo-advocate HAKI.

Tumkemee mtawala huyu! Tupaze sauti kuua Muhimili wa Bunge! Pamoja na kuwa Ndugai alikuwa shetani, nunda mla watu.
 
Ndugai alishakubali hilo bunge kuchezewa, na tayari limeshutumiwa sana na kuwa dhaifu. Ila alipotaka kuhoji sasa ndio akaulizwa toka lini amekuwa wa kuhoji?

Kwenye hili lilitokea sasa, wa kulaumiwa kabisa ni Ndugai mwenyewe, kwani tayari alishalimaliza bunge mbele ya serikali. Kibaya zaidi hata hayo maoni yake hakitatolea bungeni ambako angeweza kukaa na hizo kinga azitakazo. Kinga ya spika au mbunge ni ndani ya bunge.
 
Kama madai yako yana hata chembe ya ukweli basi angalau ungesema labda mama anamalizia yaliaoanzishwa na mwengine.

Kidogo tungetafakari,

Lakini kusema straight kwamba mama ni hivi naona kama ni kumuonea tu

Coz hayo angefanya yeyote yule awaye

Kwa kuwa yale maneno yenyewe yalikuwa ni vita tosha,

Kuhusu kupigana wenyewe kwa wenyewe Tanzania sahau,

Labda walioonja asali watake kuchonga mzinga
 
Haya yote yanayotokea na kushangiliwa hayana lolote katika ustawi wa Taifa hili.

Tunakwenda kuangamia. Jana/Juzi kitendo cha kumkemea Ndugai hadharani akajiuzulu, maana yake Bunge limesalimu amri kwa Executive. Kinachofuata ni kumalizia Mahakama maana alishaianza kuiua.

Matokeao yake unaweza usiyaone leo, lakini inaweza kuleta hata vita ya wenyewe kwa wenyewe baada ya kuwepo makundi ya KUONEA na KUONEWKun

Kuna makundi yatakataa kuonewa na yataungwa mkono na mataifa yanayo-advocate HAKI.

Tumkemee mtawala huyu! Tupaze sauti kuua Muhumili wa Bunge! pamoja na kuwa Ndugai alkuwa shetani, nunda mla watu.
Mkuu . Katiba tulionayo hii ya 1977 ni mbaya kabisa. Katiba Imemfanya Rais kuwa mungumutu , ambaye huwezi kuhoji wala kupishana naye mawazo.

Hoja ya Ndugai ilikuwa na mashiko ukilinganisha na msimamo wa mama. Lakini Tanzania hii , Rais ni mungumutu huwezi kuhoji hatua zake. KATIBA MBAYA
 
Haya yote yanayotokea na kushangiliwa hayana lolote katika ustawi wa Taifa hili.

Tunakwenda kuangamia. Jana/Juzi kitendo cha kumkemea Ndugai hadharani akajiuzulu, maana yake Bunge limesalimu amri kwa Executive. Kinachofuata ni kumalizia Mahakama maana alishaianza kuiua.

Matokeao yake unaweza usiyaone leo, lakini inaweza kuleta hata vita ya wenyewe kwa wenyewe baada ya kuwepo makundi ya KUONEA na KUONEWKun

Kuna makundi yatakataa kuonewa na yataungwa mkono na mataifa yanayo-advocate HAKI.

Tumkemee mtawala huyu! Tupaze sauti kuua Muhumili wa Bunge! pamoja na kuwa Ndugai alkuwa shetani, nunda mla watu.
Ndugai kakosa hekima na kutanguliza makasiriko mbele na hofu pia.. Kasemwa kidogo kajiuzulu ANGEKOMAA
 
Kwa aliyoyasema gwajima jana huyo ndugai wenu mnafiq na fitina tu. Kama suala lililetwa bungeni kwako ukalipitisha then unaenda kwenye media unamponda rais lengo lako nini? Alafu unashupaza shingo kwa sababu ya kukopa kwani huyo mama ndio wa kwanza? Ndugai kafanya mangapi ya kulimaliza bunge kabla hata huyo mama hajawa rais? Mbona mnachuki sana na mama nyie watu.?
 
Back
Top Bottom