Rais Samia ametangaza siku 7 za maombolezo Kitaifa kufuatia kifo cha Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt. Kenneth Kaunda

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pole kwa wanafamilia na Rais wa Zambia Edgar Lungu, kufuatia kifo cha Rais wa Kwanza na Muasisi wa Taifa hilo Kenneth Kaunda, kilichotokea jana Juni 17, 2021.

Kaunda amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 97, ambapo imeelezwa kwamba mauti yalimfika wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Jeshi ya Maina Soko iliyopo Lusaka, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, ameeleza kuwa Afrika imeondokewa na tunu na itaendelea kumkumbuka kwa yale aliyoyafanya katika nchi yake na Afrika kwa ujumla na kwamba ataendelea kumkumbuka kwa ushauri wake aliokuwa akimpatia wakati akiwa bado ni Rais hata baada ya kustaafu.

PIA SOMA:
- News Alert: - Kenneth Kaunda afariki dunia akiwa na miaka 97
 
Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, ameeleza kuwa Afrika imeondokewa na tunu na itaendelea kumkumbuka kwa yale aliyoyafanya katika nchi yake na Afrika kwa ujumla na kwamba ataendelea kumkumbuka kwa ushauri wake aliokuwa akimpatia wakati akiwa bado ni Rais hata baada ya kustaafu
Na Mwinyi anasemaje?
 
Apumzike kwa amani Mzee wetu KK, atufikishie salamu zetu kwa NYERERE, KENYATA, MANDELA, NKURUMAH na wapigania uhuru wengine wa Afrika. True Sons of Africa. Wapumzike kwa amani wote
Hivi unaachaje, kwa mfano, kwenye hii orodha kumtaja JPM, Anko Magu, Bulldozer, Tingatinga, Jembe, Chuma!??? Au akaunti yako imedukuliwa!??? Unajua JPM amefanya hata makaburi ya hao wazee wetu wapigania-uhuru, watetezi wa utu na rasilimali za Afrika, yasafishwe na kuonekana vizuri upya.
 
Back
Top Bottom