Rais Samia amepambana kishujaa na kijasiri kulifikisha hapa taifa kimaendeleo

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,096
9,466
Ndugu zangu watanzania,

Kwa hakika Rais Samia Anastahili pongezi kutoka kwa kila mtanzania mzalendo, Rais wetu Ni mpambanaji na aliyepambana kishujaa na kijasiri Sana kwa ajili ya Taifa letu, Amepambana kwa nguvu zake zote kuhakikisha kuwa licha ya mdororo wa uchumi wa kidunia uliosababishwa na ugonjwa wa COVID 19 pamoja na Vita vya ukrein na kuathiri uchumi wa nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania ,alihakikisha ya kuwa watanzania hatuathiriki na kuelemewa na mzigo wa mfumuko wa Bei.

Rais wetu na serikali yake alihakikisha anatoa mabillioni ya Ruzuku katika Nishati ya mafuta pamoja na mbolea,mfano alitoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi katika mafuta pamoja na billion Mia moja hamsini katika mbolea, alipambana kwa kuhakikisha kuwa wakati wote bidhaa muhimu zinakuwepo nchini na zinapatikana kwa Bei nafuu na maeneo yote ya nchi zinakuwepo.

Rais wetu na serikali yake amepambana kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaofaulu wanapata nafasi ya kuripoti shuleni kwa wakati,kwa kujenga vyumba vya madarasa zaidi ya elfu 20, alihakikisha Elimu inakuwa bure Hadi kidato Cha sita ili kutoa fursa kwa watoto wanaotoka Kaya za kipato Cha chini wanapata Elimu na kutimiza Ndoto zao,Amejenga zahanani na vituo vya Afya kila mahali ,ametoa maelfu ya ajira kila mwaka ili kuchochea utolewaji wa huduma kwa watanzania.

Rais Samia alizunguka na kufanya ziara huku na huko ili kuzungumza na wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kuja kuwekeza Tanzania,matokeo yake tunaona kwa Sasa Tanzania limekuwa chaguo namba moja la wawekezaji, wafanyabiashara na watalii,mapato yameongezeka kufikia Trioni mbili kwa Mwezi,ajira zimeongezeka kupitia miradi mbalimbali ya kiuwekezaji, nchi imefunguka na Sasa Biashara zimeshamiri mitaani na kuchochea mzunguko wa fedha, soko la mazao Ni la uhakika kwa wakulima.

Rais Samia alihakikisha Taifa linakuwa moja,linazungumza lugha moja na Lina kuwa lenye umoja na mshikamano,haya yote yalitokana na maridhiano na mazungumzo mbalimbali aliyoyafanya na viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wa Dini,wanaharakati wa haki za binadamu,mashirika mbalimbali na Taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa,na Matokeo au matunda ya juhudi hizi za mh Rais Ni kuwa kwa Sasa tunaona Taifa likiwa na umoja wa kitaifa,amani na utulivu, upendo miongoni mwa watanzania na Imani kubwa imejengeka kwa wawekezaji ,watalii na wafanyabiashara.

Rais Samia alipambana kuhakikisha kuwa anajenga uchumi Unaogusa maisha ya watu,uchumi unaokua katika mifuko ya watu,uchumi unaomnufaisha mtanzania moja kwa moja,uchumi unaokua mikononi mwa mtanzania, alifanya haya kwa kutambua ukweli kuwa uchumi unakuwa hauna maana ikiwa unakuwa katika makaratasi lakini ukakosa uharisia katika maisha ya watanzania.

Rais Samia alipambana kuhakikisha kuwa anaiweka serikali Yake mikononi mwa watanzania,alifanya hivi kwa kuwa msikivu kwa watu,kuwa na ajenda na sera zinazogusa hisia za watu ,maisha ya wengi,maoni ya watu,ushauri wa watanzania,kiu ya wengi na mahitaji ya wote,ndio sababu serikali Yake Ina baraka ya watanzania wote,inakubarika na kuungwa mkono na watanzania wa Rika zote ,makundi yote, jinsia zote,Dini zote na inatetewa na watanzania wote kwa kuwa kila mtu anajiona ni mmiliki wa serikali na kuwa serikali ipo kwa ajili ya kuwatumikia watanzania.

Kwa hakika Rais Samia na serikali Yake Anastahili kupongezwa Sana kwa hapa alipotufikisha,Anastahili kuambiwa Asante mama yetu kwa kazi njema na ya kutukuka aliyoifanya ndani ya muda mfupi,Anastahili kupewa zawadi ya upendo kutoka kwa watanzania wote ,Anastahili kuombewa Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania.

Amepambana Sana Rais wetu,amepigana Sana mama yetu, Amepigana na kupambana bila kuchoka,Bila kupumzika,bila kukata Tamaa,Bila kupata muda wa kukaa na familia yake, bila kinyongo Wala hasira ,bila kuwafokea au kuwalaumu watanzania,amelibeba Taifa letu katika mabega yake na kuishikiria Bendera yetu katika kifua chake na ramani ya nchi yetu katika macho yake na kuitazama Tanzania na watanzania kwa upendo,huruma ,unyenyekevu na ukarimu wa Hali ya juu Sana,amefanya kwa maslahi ya watanzania na siyo yake binafsi.

Pole Sana mh Rais kwa kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu, watanzania tuna kuunga mkono na tupo na wewe bega kwa bega,usichoke Wala kukata Tamaa,Tunakutegemea Sana Kuendelea kupata utumishi wako,yawezekana wapo uliokuwa na matarajio nao makubwa lakini wakakukatisha Tamaa ,napenda kukwambia kuwa songa mbele kwa ujasiri maana walio upande wako Ni wengi Sana,Ni Taifa lote lipo na wewe na Lina kuunga mkono, mitaani kwote sauti za watu zinakuombea heri Sana wewe binafsi na serikali yako.watanzania hatutakuacha mpweke Bali tutapigana kimaombi ili mwenyezi Mungu akujalie Afya na nguvu za kututumikia,Tupo na wewe na tutaendelea kuwa na wewe,tutasimama na wewe na tutasonga na wewe.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
All in all, nikiwekewa ccm hapa, na maandazi pale! Aisee nitachagua maandazi. Maana hakuna namna nyingine.
CCM ni chama kilichoonyesha uwezo mkubwa Sana wa kiuongozi katika Taifa letu ,ndio maana watanzania Tunaendelea kuwa wenye umoja na mshikamano,tofauti na majirani zetu ambao vyama vyao ni kwa ajili ya uchaguzi na kusaka madaraka,lakini kwa CCM Ni Taifa na maslahi ya Taifa kwanza
 
Utaacha lini kumsifia sifia mwanamke mwenzio mtandaoni kila siku? Hunaga contents nyingine zaidi ya hizi za kumwabudu binadamu mwenzio? Hujajifunza kwa Musiba tu? Usimtegemee binadamu mwenzio kama ngazi ya kukwea kwenye mafanikio. Kama ipo ipo tu
Acha dharau zako wewe
 
CCM ni chama kilichoonyesha uwezo mkubwa Sana wa kiuongozi katika Taifa letu ,ndio maana watanzania Tunaendelea kuwa wenye umoja na mshikamano,tofauti na majirani zetu ambao vyama vyao ni kwa ajili ya uchaguzi na kusaka madaraka,lakini kwa CCM Ni Taifa na maslahi ya Taifa kwanza
Kwenye eneo la kuwadhulumu wananchi wake. Kingine nini?

Fedha ya serikali iwe mapato ya ndani au ya mikopo na misaada, inafujwa ovyo na hakuna hatua ya kuiokoa.

Robo tu hutumika kuwasaidia wananchi na kiasi kinachobaki huliwa na wenye mamlaka.

Bado jitu linakuja humu kusema Rais Samia kafanya. Kafanya nini zaidi ya kutalii na kula kodi zetu na washirika wake?
 
Wewe andika yote! Ila mwisho wa siku niwekee ccm na maandazi sehemu moja, halafu uoe kama sitachagua maandazi.
 
Umeandika vingi ila ni ujinga mtupu
 
CCM ni chama kilichoonyesha uwezo mkubwa Sana wa kiuongozi katika Taifa letu ,ndio maana watanzania Tunaendelea kuwa wenye umoja na mshikamano,tofauti na majirani zetu ambao vyama vyao ni kwa ajili ya uchaguzi na kusaka madaraka,lakini kwa CCM Ni Taifa na maslahi ya Taifa kwanza
Mbona sasa kwenye Uchaguzi,CCM kinatumia nguvu nyingi sana kuingia madarakani?
Polisi,TISS,Jeshi na Tume ya Taifa ya uchaguzi wanalazimika kuchakachua matokeo ya kura ili CCM ibaki madarakani.
 
Kwenye eneo la kuwadhulumu wananchi wake. Kingine nini?

Fedha ya serikali iwe mapato ya ndani au ya mikopo na misaada, inafujwa ovyo na hakuna hatua ya kuiokoa.

Robo tu hutumika kuwasaidia wananchi na kiasi kinachobaki huliwa na wenye mamlaka.

Bado jitu linakuja humu kusema Rais Samia kafanya. Kafanya nini zaidi ya kutalii na kula kodi zetu na washirika wake?
Ngoja nikwambie na kukueleza tu kwa kifupi japo naona akili yako bado haijakomaa na huna uelewa na ufahamu wa Mambo mengi Sana.

Ziara za mh Rais nje ya nchi zimekuwa na manufaa makubwa Sana na kuzaa matunda kwa Taifa letu, mfano Ni ziara ya mh Rais nchini China iliyoleta matunda ya kusamehewa Deni la billion 31 fedha zitakazotumika kuweza katika maeneo mengine Kama vile Afya , Elimu, Miundombinu ,maji ,kilimo, n.k.

Ziara y mh Rais wetu nchini Kenya iliimarisha mahusiano yetu na Kenya na kupelekea Tanzania kunufaika na soko la Kenya kwa Bidhaa kutoka Tanzania ikiwepo mazao n.k, Nafikiri unaona hata Gas yetu kupitia wafanyabiashara wetu Kama Rostam azizi inauzwa katika soko la Kenya kwa wingi Sana,

Ziara ya mh Rais nchini marekani nayo ilijenga na kuyapa uhai mahusiano yetu na marekani mpaka kufikia makamu wa Rais wa marekani kuitembelea Tanzania hivi karibuni ,ambapo faida yake Ni kuwa Tanzania inaendelea kunufaika na fursa za kiuwekezaji,kibiashara n.k kutokana marekani na pia kupata mabillioni ya pesa .

Ziara hizo za mh Rais katika kuitangaza nchi yetu na vivutio vyake kupitia wazo lake la kibunifu la Royal Tour imepelekea watalii mbalimbali kumiminika hapa nchini,

Ziara za mh Rais katika mataifa mbalimbali zimekuwa na matunda Sana kwa Taifa letu,zimeleta fursa za kiuchumi,kuitangaza nchi yetu, kuvutia wawekezaji wengi Sana, kuliheshimisha Taifa letu kimataifa,

Naomba niishie hapa maana nikiandika mengi nitauchanganya ubongo wako ambao nimeona Ni mdogo Sana na hauna kitu kichwani mwako Zaid ya ulimbukeni na ujianga tu Kama mtoto aliyekosa malezi Bora ya wazazi wake
 
CCM ni chama kilichoonyesha uwezo mkubwa Sana wa kiuongozi katika Taifa letu ,ndio maana watanzania Tunaendelea kuwa wenye umoja na mshikamano,tofauti na majirani zetu ambao vyama vyao ni kwa ajili ya uchaguzi na kusaka madaraka,lakini kwa CCM Ni Taifa na maslahi ya Taifa kwanza
Watanzania gani? Acha bangi wewe!
 
Mbona sasa kwenye Uchaguzi,CCM kinatumia nguvu nyingi sana kuingia madarakani?
Polisi,TISS,Jeshi na Tume ya Taifa ya uchaguzi wanalazimika kuchakachua matokeo ya kura ili CCM ibaki madarakani.
CCM imeshinda na Itaendelea kushinda katika chaguzi zote kutokana na kuaminiwa na kukubalika na watanzania,kunakotokana na kuwa na Sera na ajenda zinazogusa maisha ya watu,kujari na kuwa na uchungu na maisha ya watu,kujibu kero na changamoto za watu,kuwa na ilani inayoendana na mahitaji ya watu na wakati,kuwa karibu ya wananchi na kuwasikiliza kero zao, kubadilika kulingana na wakati,kuwa na viongozi na wagombea wanaokubalika na watu na wakati wote kuzungumza ajenda za watu zinazo gusa maisha Yao.

Hata ije tume ya uchaguzi kutoka marekani bado CCM itashinda kwa kishindo Tuuuuuuuuuuu ,kwa kuwa mamilioni ya watanzania Wana Iman na CCM na wanaipenda na kuikubali Sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom