Rais Samia amekwepa mshale kibahatibahati wakati huu! Next??

Mimi kwa sehemu yangu kama mtanzania, nimemsamehe Spika Ndugai... Ni jukumu langu la kikristo kusamehe 7 ×70 =490

Hiyo ni misamaha mingi sana, hivyo awe ameomba kwa nia ya dhati au kinafiki...potelea mbali. Acha apunguze hapo msamaha mmoja. Japo sitaacha kujadili content ya alichokiongea.

Ukweli ni kuwa hakukua na video clip kuchakachuliwa wala kupunguzwa wala kutafsiriwa vibaya...it is what it is... ni bona-fide genuine directly kutoka kwa Ndugai.

Huu ulikuwa mkuki na ulimlenga mama directly.

Lengo lilikuwa ku-spin mjadala ambao utakuwa nje ya uwezo wa mama kuudhibiti kwa kuamini kuwa hana propaganda machinery ya kupambana na huo mjadala.

Hapa ndio napoamini mama anahitaji kujipanga kwenye propaganda! Maana ni wazi kwamba amekwepa huu mkuki 'kimishemishe' na kubwa ni kwasababu ya maadaui wengi wa Ndugai.

Hapa mama amepiganiwa na watu wote (walio wana CCM na wapinzani) na ndio maana huu mzigo ukaonekana mwepesi.

Ila kuelekea kwenye joto la uchaguzi mkuu... maadui ndani ya chama hawatajificha (kama walimwimbia JK usoni kua wana imani na Lowasa, mama ni nani wasimwimbie?)

Na wapinzani watakuwa at their best ukichukulia ukweli kuwa Lissu na Lema watakuwa ndani ya nyumba... Lissu ni mzuri sana kwenye kuanzisha mijadala inayokuwa migumu kudhibiti.

Wakati huo mama hatakuwa na wasamaria wema wa kumtetea!

Mama Samia atengeneze timu ya Propaganda sasa ili iwe tested mapema... akitumia Tiss kufanya reality check ndani ya chama atagundua makatibu wengi na hawa ni pamoja na waenezi wa ngazi zote ndani ya chama hawako upande wake.. na ni vile tu hakuna upande uliojiweka wazi ndani ya chama ndio maana wako kimya.
Wengi ni wakupiga nyundo mwaka huu wa uchaguzi ndani ya chama!!

It is now or never, mvua kubwa ikianza hakutakuwa na muda wa kutengeneza safina!
Point taken

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Inweza ikawa hivyo ila inaweza kuwa ni two-term plus. Kama unaelewa siasa weka na hiyo. Wakati mwingine binadamu tunakuwa na ugonjwa unaoitwa colour blindness.
Sio kwa Samia haina mjadala mwisho wake 2021-2025 hapo tu ifahamike hivyo.
 
Back
Top Bottom