akilinene
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 514
- 433
Hata Chadema mngeungana wote hamzidi hata asilimia 1 ya watanzania wote. Hiyo ndiyo sauti ya wengi?Kila kitu kinachofanyika, kutendeka au kutendwa, kinapaswa kuwa katika kiwango ambacho hakipungui sana au kuzidi sana(kiwe within reasonable limits).
Kwa msingi huo, hata viongozi wetu katika kufanya maamuzi, wanapaswa kuzingatia hilo ili wasiharubu, na pia ili wasionee watu.
Mwendazake katika kufanya maamuzi, kuna wakati ni wazi alipitiliza na alionea sana watu, na ndio maana tuliona baadhi ya aliowaondoa katika nafasi zao, baadae aliwarudisha(inaonyesha aligundua makosa yake).
Sasa huyu Mama yetu anaonekana kuwa ni kinyume cha Mwendazake kwa kuwa mzito kuchukua maamuzi kwa viwango nachosema ni cha kupitiliza(it is getting too much).
Mfano sahihi ni jinsi anavyokuwa mzito kumuondoa huyu Bosi wa Mapolisi ambae sasa anapigiwa kelele karibu kila kona ila Mama bado haoni kuwa huyu mtu ni tatizo (anapaswa kuondolewa).
Kama anapokea maagizo kutoka juu, njia mowajawapo ya kurekebisha hali hii bado itabaki kuwa ni kumuondoa tu na kumpangia kazi nyingine, na mrithi wake asiingiliwe, vinginevyo hatua ya kumuondoa itakuwa haina maana.
Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, hivyo kama Mama ataendelea kupuuza hizi sauti, basi awe tayari kukubaliana na matokeo, na sijui kama kuna binadamu wa kushindana na Mungu.
Hata Mwendazake alimlinda sana Bashite na kupuuza sauti ya walio wengi, ila mwisho wa siku yalimshinda.
Too much of everything is harmful-Mama utajionea siku si nyingi
Time will tell.