Rais Samia amekataa ombi la Jeshi la Polisi kutumia nusu ya fedha za faini wanazokusanya kuendeshea Baraza la Usalama Barabarani

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,761
Rais Samia Suluhu Hassan amelikataa ombi la Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani la kutaka kutumia nusu ya fedha wanazokusanya kama faini kuendeshea Baraza la Usalama Barabarani.

Rais Samia amesema akikubali maana yake kikosi cha usalama barabarani kitajikita kwenye kukusanya faini badala ya kuzuia ajali.

Chanzo: Swahili Times

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwenye hilo, Rais Samia yupo sahihi sana. Azidi kujaliwa hekima ya nna hiyo hiyo hata kwa yale yaliyobakia.

Ushauri wowote kutoka kwa mtu mwovu, ni lazima uchukuliwe kwa tahadhari kubwa.

Kwa sasa, Polisi ni nadra sana kufikiria yaliyo mema kutokana na ile roho ya uovu inayotembea miongoni mwao.
 
Hangaya,Polisi wanapenda kupangwa Traffic na kuendesha pikipiki za misafara.
IGP mkaliangalie hilo
Kauli kauli kauli
 
Huku kwetu Dubey polisi wanatumia Lamborghini katika Doria! 😏
 
Sawa, basi atoe hilo fungu badala yake, ukisikia kutafuta umaarufu wa kitoto ndo huu, …
 
Naona makapuku polisi wanavyofura kwa hasira baada ya mtego wao wa ulaji kugonga mwamba mbele ya chuma Samia
 
Wasipewe hata senti, wao wanatakiwa kuthibiti makosa ya usalama barabarani siyo kukusanya pesa za faini ili wapate nusu ya makusanyo, kwa thinking ya namna hii nimeamini kauli ya Simbachawene, na kwa kutoa kauli isiyo na weledi kama hiyo nchi za wenzetu igp hana kazi.​
 
Rais Samia Suluhu Hassan amelikataa ombi la Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani la kutaka kutumia nusu ya fedha wanazokusanya kama faini kuendeshea Baraza la Usalama Barabarani.

Rais Samia amesema akikubali maana yake kikosi cha usalama barabarani kitajikita kwenye kukusanya faini badala ya kuzuia ajali.

Chanzo: Swahili Times

Maendeleo hayana vyama!

Kwani malengo ya kukusanya kiwango cha faini kwa siku kwa askari wa Sirro kimebadilika?
 
Back
Top Bottom