MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,009
- 2,169
Ni vigumu kuamini lakini ndio ukweli kwamba rais wetu naye sasa ni mfanyabiashara mashuhuri nchini na anamiliki magari mengi ya usafirishaji. Sasa aamini nchi itaendelea kwa ushirika na wafanyabiashara. Haiwezekani!
Wafanyabiashara wetu ni misheni tauni. Wapigaji wa serikali kama ilivyokuwa IPTL. Kwa kuwapa nguvu wafanyabiashara sasa wako kwenye mashirika ya uma kama ilivyo bodi ya TANESCO.
Wafanyabiashara sasa wanasafiri na Rais kusaini mikataba kama tulivyoona Rostam akifanya. Sasa wafanyabiashara hawagusiki tena.
Bahati mbaya wafanyabiashara sasa wanaingiza vijana wao ktk siasa na kuwasimamia kupata uwaziri. Ilikuwa hivyo kwa akina Ngereja na Rostam wake, sasa kamchukuwa Bashe, wamo akina makamba, nk.
Tatizo linaanza kujitokeza kwenye bwawa la umeme la Mwl. Nyerere na reli ya SGR. Tunamuona rais akianza kuzungumza lugha kwamba watashirikiana na sekta binafsi. Watu binafsi waingie kuzalisha umeme kwa bwawa liliojengwa na serikali!
SGR nayo inajengwa na serikali, eti na wafanyabiashara wanunue mabehewa binafsi kama shares zao, kama Ndugai alivyowahi ropoka Bungeni. Nchi inakufa!!
Uhusiano wa wafanyabiashara na serikali siyo wa aina hii. Wao walipe kodi tu! Mfanyabishara makini hahitaji safari ya rais ili akasaini bishara zake, huo ni mtego wa kuingiza mkono Ikulu kama ilivyo sasa hivi. Huu ni wizi na ufisadi unaoanzia Ikulu na rais naye akionesha tamaa ya kufanya biashara.
Ndio maana tunaona lugha za kusema TRA wazungumze na wafanyabiashara, mazungumzo yapi badala ya kufuata sharia za miaka yote? Ktk kilimo Bashe anakuja na hadithi za ruzuku ya mbolea tena ambayo ilitumika kupiga pesa ya serikali.
Waagizaji tayari wapo wanasubili GO! Waziri Mkenda alipolinda viwanda vya sukari akaambiwa na rais hiyo ni nonsense! What a hell president is this?