Rais Samia ameingia katika biashara na kuwadekeza wafanyabiashara. Nchi inakufa

Nionavyo ni Wa-TZ kuhadaika kiurahisi na kelele za Bungeni. Yaani Bashe anasimulia mambo utadhani ana niya njema. Anajidai kusimulia shida za mkulima ambazo zinafahamika miaka yote na bado anasifiwa. Nyuma yake ana lake jambo. Nimeona aliamua kusimulia mambo ya bei ya mbolea lakini hasemi kwa nini analeta benki ya ushirika wakati benki ya wakulima ipo. ni mpotopshaji tu!
Je Bashe anajua kuwa huko nyuma tuliwahi kuwa na benki ya ushirika hapa nchini? Hatima yake ilikuwa nini?
Kabla ya kuridhia kuanzisha hiyo benki Ijulikane tu kuwa benki ya wakulima inaweza kuwahudumia wana ushirika kwani ni hao hao wakulima!
Bashe asome historia ya benki ya ushirika nchini kabla ya kuleta duplication ya institutions just to achieve personal gain , that will be misallocation of resources.
 
naomba kutoa ushuhuda. mimi nimeishi na watu waliondelea. huko uzunguni miaka kumi huko hakuna ushirika wa serikali na wafanyabiashara katika kujenga miundombinu ya nchi bali reli ikishajengwa ni 100% mali ya serikali na uzalishaji umeme ni 100% mali ya serikali. ushirika ni kwenye kodi tu mfanyabiashara anaelipa kodi kubwa anafikiriwa punguzo.

serikali kama haina pesa inakopa kwenye mashirika ya fedha au benki kujenga miundombinu sio kuchukua pesa za wafanyabiashara maana ukishachukua pesa zao huwezi kuwaendesha nchi inakuwa mali yao wanaifanya serikali wanavyotaka na kodi hawalipi.

hiyo model ya serikali eti wafanyabiashara walete mabehewa kwangu mimi ni traditional au classical sio modern theory of economic development na nina hakika tutafeli.
Tuwalaumu sana wachumi wanaomshauri Mama.

Anaejua kitabu kilichoandika huo ushirika wa kuanzia kujenga miundombinu ya nchi kwa ushirika wa serikali na wafanyabiashara atutajie tukisome

kitabu namba moja wanachotumia wazungu wote duniani kujifunza kuhusu uchumi kinaitwa Wealth of Nation by Adam Smith (1776) ambapo raia wanafundishwa namna ya kuwa matajiri na serikali kuwawekea miundombinu mizuri ya uwekezaji.
Mama ana tabu kwakweli kila mtu mshauri
 
Umeandika mengi kama husia zako au chuki binafsi kwa private sector hujaonyesha hatari iliopo wakishirkiana na sector binfsi.....kwa information yako serikali yoyote ya maana haiwezi kufanikiwa bila private sector
Binafsi sina mfano wowote wa mafanikio ya ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi afrika hii. Unao mfano unaoujua? Tuelimishane, tafadhali!
 
Baba yenu alijidekeza kufanya kila kitu mwenyewe, kafa na hakuna aichokikamilisha.
Biashara na ajira nyingi zilikufa, wafanyabiashara waliporwa mchana kweupe na serikali(Task Force za TRA).

Nyie manundu mlifurahia ama hamna akili nzuri, sasa tuna mtu mweye akili Chamwino.
Mnafikiri maisha ni lelemama kwa kutaka kutukuzwa "unyonge", na ninyi kutaka kupewa vya bure.
Humpendi JPM lakini kimoyomoyo unamuwaza namna alivyokuwa na dira ya wapi nchi iende, mama Yako sidhani kama anamuda hata wa kusoma mafaili yeye alikiri Hana kichwa Cha kukalili mambo Wala kuyafuatilia
 
Kampuni kubwa zaidi za Treni marekani za BNSF na Union Pacific hazimilikiwi na serikali na wala serikali haina mkono wake huko. BNSF inamilikiwa na Berkshire Hathaway ya Warren Buffet na UP inamilikiwa na wanahisa mbalimbali.
naomba kutoa ushuhuda. mimi nimeishi na watu waliondelea. huko uzunguni hakuna ushirika wa serikali na wafanyabiashara katika kujenga miundombinu ya nchi bali reli ikishajengwa ni 100% mali ya serikali na uzalishaji umeme ni 100% mali ya serikali. ushirika ni kwenye kodi tu mfanyabiashara anaelipa kodi kubwa anafikiriwa punguzo. hiyo model ya serikali eti wafanyabiashara walete mabehewa kwangu mimi ni traditional au classical sio modern theory of economic development na tutafeli. Tuwalaumu sana wanaomshauri Mama. Anaejua kitabu kilichoandika huo ushirika wa kuanzia kujenga miundombinu ya nchi kwa atutajie tukisome
 
Utakuwa bwege basi! Tunajadili hali ya TZ wewe unaleta mifano ya nchi unazoita kubwa. Hapa TZ unao mfano wowote wa mafanikio uliotokana na wafanyabiashara binafsi kushirikiana na serikali? Hawa akina Rostam ndo unasema ni wafanyabiashara? Hawa akina Kikwete na GSM yao ndo wafanyabiashara? Hawa ni wezi tu! Hwana lolote. Faida wanaitegemea itokane na wizi, basi!

OLIGARCHS . Hawa washirika wa Kikwete Utajiri wao unatokana na kuiibia Serikali through overpricing in the services they render to the government!! Ndio Maana huwa wanafanya juhudi kuweka vijana wao kama Bashe, January, Ngelleja kwenye nafasi ambako watafanikisha kufanya biashara kubwa kubwa na serikali!!

Hivi sasa wamemuingia Samia through Kikwete na kutumia ignorance ya huyu mama kuihujumu nchi na kumdanganya kuwa watamsaidia kumpatia resources za kuendelea kuwa Rais post 2025!
 
Kikwete alileta fursa nyingi sana.
Tatizo la watu wengi wanapenda kujazwa manoti mfukoni badala ya kujifanyia kazi na kujijaza manoti mfukoni.
Hakuna darasa la kuziona fursa, hiyo ni akili yako mwenyewe.
Hapana mkuu mie sipo huko kwenye kujaza manoti mfukoni sikumaanisha mafanikio yangu au maendeleo yangu binafsi.
 
Kwa nini Watanzania wengi hawataki kujifunza kwenye historia ya hii nchi? Sera za kuwabana wafanyabiashara na kuwaita wahujumu uchumi zilishafanywa na Nyerere tangu enzi za Azimio la Arusha. Mwisho wake nchi ilifilisika na umaskini kuongezeka.

"Those Who Do Not Learn History Are Doomed To Repeat It" - George Santayana
 
OLIGARCHS . Hawa washirika wa Kikwete Utajiri wao unatokana na kuiibia Serikali through overpricing in the services they render to the government!! Ndio Maana huwa wanafanya juhudi kuweka vijana wao kama Bashe, January, Ngelleja kwenye nafasi ambako watafanikisha kufanya biashara kubwa kubwa na serikali!!

Hivi sasa wamemuingia Samia through Kikwete na kutumia ignorance ya huyu mama kuihujumu nchi na kumdanganya kuwa watamsaidia kumpatia resources za kuendelea kuwa Rais post 2025!

Oligarchs ndiyo waliojenga uchumi wa Urusi baada ya wakomunisti kuifilisi nchi na Soviet Union kusambaratika. Tofauti, Urusi wanajua kuwatumia oligarchs wao kuleta maendeleo ya uchumi wao, wabongo mnawapiga vita. Ndiyo maana uchumi wetu unakwama.
 
Baba yenu alijidekeza kufanya kila kitu mwenyewe, kafa na hakuna aichokikamilisha.
Biashara na ajira nyingi zilikufa, wafanyabiashara waliporwa mchana kweupe na serikali(Task Force za TRA).

Nyie manundu mlifurahia ama hamna akili nzuri, sasa tuna mtu mweye akili Chamwino.
Mnafikiri maisha ni lelemama kwa kutaka kutukuzwa "unyonge", na ninyi kutaka kupewa vya bure.
Mwenye akili kwa kuacha bora liende? bidhaa zinapanda bei kiholela yupo tu? Kiufupi anakumbatia wachache na kuacha kundi kubwa likiteseka
 
Oligarchs ndiyo waliojenga uchumi wa Urusi baada ya wakomunisti kuifilisi nchi na Soviet Union kusambaratika. Tofauti, Urusi wanajua kuwatumia oligarchs wao kuleta maendeleo ya uchumi wao, wabongo mnawapiga vita. Ndiyo maana uchumi wetu unakwama.

Oligarchs wameficha fedha zao nje ya RUSSIA na ndio maana wanahangaika sasa wakati account na mali zao kushikiliwa. Huwezi kuwatumia watu kama ROSTAM kuendeleza nchi wakati fedha zao nyingi wanaficha nje ya nchi na kuwadanganya nyie mazuzu wanaleta kidogo na kuwekeza kwenye sehemu ndogo na zingine kuwagawia ENABLERS wao wakina KIKWETE and their conspirators.
 
naomba kutoa ushuhuda. mimi nimeishi na watu waliondelea. huko uzunguni hakuna ushirika wa serikali na wafanyabiashara katika kujenga miundombinu ya nchi bali reli ikishajengwa ni 100% mali ya serikali na uzalishaji umeme ni 100% mali ya serikali. ushirika ni kwenye kodi tu mfanyabiashara anaelipa kodi kubwa anafikiriwa punguzo. hiyo model ya serikali eti wafanyabiashara walete mabehewa kwangu mimi ni traditional au classical sio modern theory of economic development na tutafeli. Tuwalaumu sana wanaomshauri Mama. Anaejua kitabu kilichoandika huo ushirika wa kuanzia kujenga miundombinu ya nchi kwa atutajie tukisome
Mwisho wa siku hiyo SGR itakuja Kususua. Kama matajiri ndo watanunua mabehewa na kufanya biashara
 
Umeandika mengi kama husia zako au chuki binafsi kwa private sector hujaonyesha hatari iliopo wakishirkiana na sector binfsi.....kwa information yako serikali yoyote ya maana haiwezi kufanikiwa bila private sector
Rudia kusoma utaelewa. Usikurupuke kujibu.
 
Oligarchs wameficha fedha zao nje ya RUSSIA na ndio maana wanahangaika sasa wakati account na mali zao kushikiliwa. Huwezi kuwatumia watu kama ROSTAM kuendeleza nchi wakati fedha zao nyingi wanaficha nje ya nchi na kuwadanganya nyie mazuzu wanaleta kidogo na kuwekeza kwenye sehemu ndogo na zingine kuwagawia ENABLERS wao wakina KIKWETE and their conspirators.
Walizificha baada ya mwendawazimu Putin kuchukua nchi. Enzi za Yelstin walikuwa wanapeta tuu na ndiyo walioiyokoa Urusi kiuchumi. Putin huwa anawakamua Oligarchs hela zao kimafia ili ajitajirishe yeye binafsi na familia yake na kufanya siasa zake. Utajiri wa Putin aliupata kinyama na hela za kuvamia nchi jirani alizipata kinyama.

Jiulize kwa nini oligarchs wetu wanaficha hela nje? Wanajua kuna wanasiasa mafisi wanataka kuwapora ili wafanye siasa haramu na kutajirisha familia zao.
 
Sijazingumzia udhaifu ila nimezungumzia ujanja na ushamba, Mwendazake alikuwa mshamba watu wakalalamika ila kaja mjanja tena kazungukwa na watoto wa mjini ila bado watu wanalalamika.

Kila mmoja lawama na sifa zinaenda kwa angle yake.
 
Back
Top Bottom