Rais Samia amefanikiwa kupambana na adui watatu wa Mtanzania

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Ni maadui watatu waliotajwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere tangu tunapata uhuru – ujinga, umaskini na maradhi. Hadi anazikwa kijijini kwake Butiama Oktoba, 1999, maadui wa Taifa walibaki ni walewale watatu.

Na kuna viongozi wengi waliopita walijitahidi kupambana na hawa maadui zetu watatu lakini hawakufanikiwa ni miaka zaidi ya 60 sasa toka Tanzania ipate uhuru kulikua hakuna miundombinu bora kuna sehemu huduma za afya zilikua hazijafika, kilimo kilionekana kama cha watu masikini, lakini sasa Rais Samia Suluhu amekuja na mikakati mbali mbali ya kupambana na hawa maadui zetu UJINGA, UMASIKINI, na MARADHI

UJINGA; Rais Samia Suluhu amepambana na ujinga kwa kuboresha sekta ya elimu amefanikisha ujenzi wa madarasa mpaka vijijini sehemu ambazo zilisahaulika lakini pia amewezesha elimu bure kutoka awali mpaka kidato cha sita, madawati ya kutosha na ameajiri walimu wa kutosha .

Vile vile 2023 kuna ajira zaidi ya elfu 42 za walimu zimepitishwa pia ataongezea ujenzi wa madarasa 8000 nchi nzima maana mwaka huu wahitimu wa darasa la saba wameongezeka kwa 22% ukilinganisha na mwaka jana
Lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bure iliyo bora katika mazingira rafiki

UMASIKINI; Rais Samia Suluhu amefanikiwa kupigana na adui yetu mkuu umasikini na sasa amefanikiwa kwa kuhakikisha ametoa ajira, ameongeza mishara kwa kima chini kwa asilimia 23.3 pia kwa wale ambao hawajaajiliwa, amehakikisha vijana wanqpata mikopo yenye mashart nafuu na ili kuondokana kabisa na umasikini Tanzania Rais Samia Suluhu ameamua kuwekeza katika kilimo maana kilimo ni biashara pia ni ajira

MARADHI Rais Samia sasa anaendelea kuhakikisha anapambana na maradhi kwa kuhakikisha upatikanaji wa vituo vya afya mpaka vijijini na amehakikisha anapunguza gharama za matibabu kupitia bima ya afya kwa wote.

Rais Samia Suluhu anahakikisha tunafaulu kwa asilimia 100 kuondokana na ujinga, umasikini na maradhi
 
Wajinga wanazidi kuongezeka, maradhi ndo balaa. Kwenye umaskini ndo usiseme. Hata wewe unaweza kuwa shahidi.

Unalipwa shingapi?
Mama amejitahidi sana kwa kiasi kikubwa kupamabana na hawa maadui zetu na amefanikiwa, hata kaya masikini saizi wanasaidiwa kupitia mfuko wa TASAF
 
Yeye mwenyewe ni wale wale
Mama kajitahidi sana jamani katikauongozi wake ametoa ajira nyingi na ameboresha miundombinu wawekezaji wanakuja kila siku Tanzania na fursa za ajira zimeongezeka kwaiyo Rais Samia Suluhu amefanya mapinduzi makubwa ukilinganisha na mtangulizi wake hakutoa nafasi za ajira kabisa
 
Back
Top Bottom