Rais Samia amedhihirisha kuwa CCM imefilisika sera Kama alivyosema Mwl.JK. Nyerere

Kwa kweli huyu, kwa ile kauli kuwa wanawake wamchague yeye kwasababu ni mwanamke mwenzao, ameonekana kupwaya sana. Kwa hiyo anataka na wanaume wamchague mwanaume kwa vile ni mwanaume mwenzao?

Asiendelee na hizi hoja mfilisi. Wanaume wana uwezo wa kusahau vyama vyao ili kuhakikisha tu hatuongozwi na mwanamke mwenye hulka za ubaguzi wa kijinsia.

Hii inaweza kuwa ni sababu ya yeye kuanza kuwapachika akina mama kwenye nafasi nyeti kama Waziri wa Ulinzi. Huenda Siro akitoka, IGP atakuwa mwanamke, siyo kwa sababu ya sifa bali kwa sababu ya uwanamke wake.

Hili tulikemee kwa nguvu.
 
Wanaume lazima tuungane kuondoa umama huu wanao taka kutuchezea.
Mwanaume wa kweli hatishwi na Mwanasesere.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo uliona ni sawa kwa wafia chama waliojiunga chama hicho miaka zaidi ya kumi iliyopita kumpigia deki mtu aliejiunga chaman wiki mbili na kupewa ridhaa ya kugombea uraisi kwa masilahi ya mwenyekiti na genge lake?
Mbona huko ccm kuna wafia chama wengi tu waliokipigania chama muda mrefu lakini kina Gekul, Kitila mkumbo, katambi na wengine kibao wametojiunga toka upinzanii na kulamba uteuzi wakiwaacha wafia chama lakini hamlalamiki
 
Wangoni ni wazinzi mno bwashee, jina limetokana na neno UGONI.
Mkuu nasikia kuwa huwa wanataniwa na watani wao "Mngoni ukimpatia fedha hata ziwe mamilioni kumpelekea mtu atazifisha zote bila kuchukua hata shilingi, lakini ukimwomba au umtume akusindikizie/akupelekee mwanamke mahali, hamfikishi badala yake ANAOA
 
Unamzungumzia Lisu huyu ambae ameshindwa kuwashawishi watanzania wachague wabunge hata watatu wa chama chake au Lisu yupi? Look bro... Mwaka 2005 Chadema ilimsimamisha Mbowe agombee uraisi, japo aliangukia pua lkn ushawishi wake ulisababisha chama chake kipate wabunge zaidi ya 20. Mwaka 2010 kikampitisha dr Slaa agombee uraisi, vile vile japo alishindwa kupenya lkn alikiletea chama chake wabunge zaidi ya 50. Mwaka 2015 mkaazima mgombea wa CCM mh Lowasa na yeye alijaribu kufanya kile alichofanya kwa kuwaletea wabunge ambao hamkuwahi kupata toka chama chenu kianzishwe, ila kwa upande wa uraisi alishindwa japo kwa kura ndogo. Mwaka 2020 mkampitisha mbeleji wenu ndugu Lisu agombee matokeo yake kila mtu anajua. Ilikuwa ni aibu kwa jamaa kugalagazwa yeye na wagombea wake wa ubunge wote. Hii ikamfanya yeye mwenyew atorokee Ulaya kujificha baada ya kuona aibu kuendelea kubaki nchini. Hizo chaguzi zote ninazokwambia tume ilikuwa ni ile ile mnayosema sio huru miaka yote, wasimamizi ni wale wale na polisi ni wale wale, ila Lisu tu ndio aliangukiwa na jumba bovu kwa vile hakuwa na ushawishi wa kuwashawishi watanzania kama walivyofanya kina Mbowe, Slaa na Lowasa.
Mkuu unaandika haya kwa utanii ama kama burudani/utani tu, or you're serous. Kila mtu anajua uchaguzi ule ulichafuliwa hadi wakapatikana COVID 19, na mwenye Dunia akaleta PIGO la ugonjwa wa CORONA. Be serous kwenye hoja zako, wengine tunaendelea kujifunza humu.
 
Back
Top Bottom