Rais Samia akiwa Longido amlilia tena Hayati Magufuli

Huyu bila mambo ya Wuhan angeupata wapi urais? Kwamba hayashukuru ila analia? Siyo ya mamba hayo?

Huyu kwa habari zilizopo kwa kukerwa na mwendazake alishawahi kutema mzigo mara kadhaa. Kumbe alia sana kwa kuondokewa?

Angekuwa konda boy, SABAYA au ile timu pendwa wangeeleweka.

Huyu alipo kwa ajili ya 2025 atasema lolote.
Mkuu Brazaj uzalendo ni pamoja na kutumia lugha za staha kwa mh.Rais wako......
 
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu leo akiwahutubia wananchi wa Longido amemlilia tena aliyekuwa rais wa tano wa nchi yetu John Magufuli na kuwataka wananchi wasimame kumuombea roho yake ilale mahali pema peponi.

Rais Samia amewaambia wana Longido kuwa kama siyo ujasiri wa hayati Magufuli kuwapelekea jumla ya billioni 15 wasingepata maji hadi leo hii. Amesema Maji ni sadaka hivyo Magufuli alitoa sadaka kwa wana Longido hivyo wanapaswa kumuombea.


Kwahiyo hiyo sadaka imetolewa na Magufuli! Kwani ni hela zake! Kama alitaka kutoa sadaka angetoa kutoka kipato chake tena kile cha halali sio hela za watanzania (serikali) halafu eti mdai yeye ndio katoa sadaka.
 
Mkuu Brazaj uzalendo ni pamoja na kutumia lugha za staha kwa mh.Rais wako......

Wapi pako tenge mkuu?

Pamoja na machungu mengi tunaandika with "total restraint."

Wako wapi ndugu zetu hawa: Ben 8, Azory au

IMG_20211015_144814_546.jpg


Jiweke kwenye viatu vyetu kuyaelewa machungu yetu tafadhali.
 
Back
Top Bottom