Rais Samia akishiriki Makabidhiano na Uzinduzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma Kagera, leo Oktoba 13,2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Rais Samia akishiriki Makabidhiano na uzunduzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma Kagera, leo Oktoba 13,2022

eb475e9d-dbfe-4d02-9e8c-35bec06aafec.jpg

7695703a-3ae8-4e56-8c27-9965aead19c6.jpg

Muonekano wa Majengo ya Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) kilichopo, Burugo Kata ya Nyakato Bukoba ambacho kimezinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 13 Oktoba, 2022 Mkoani Kagera.

======
11:09 Rais Samia kazindua Majengo ya chuo cha VETA Kagera.

Chuo cha ufundi stadi na Huduma cha Kagera, kimekamilika kwa asilimia 100 ambapo bilioni 22 zimetumika kujenga chuo hicho. Chuo kina majengo ya madarasa, mabweni, nyumba za walimu, karakana, maktaba, jiko nk.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila
Sisi wananchi wa Mkoa huu wa Kagera tumefurahi sana na hakika ujio wako umeleta neema nyingi sana kwa mkoa huu. Na nimekuwa nikiwaambia wananchi wa hapa kuwa heshima tuliyopata kwa ujio wako na tutakayoendelea kupata haijawahi kutokea kwa mkoa huu hakika unatuletea maendeleo makubwa.

Na kwa ujenzi wa chuo hiki tumepata heshima kubwa na hakika umetuheshimisha na nilikuletea ombi la kuwa vile vyuo vilivyokuwa vimefungwa vinavyomilikiwa na kanisa vifunguliwe ukanijibu kuwa umeleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa chuo kikuu na vile vyuo vilivyofungwa vifunguliwe.

Pia kuna miradi ya maji inaendelea na mradi wa maji ambao ulikuwa kama umetelekezwa ni mradi wa Kemondo na sasa unatekelezwa.

Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

4e13b26a-ef85-46b0-93ae-ff34670e5801.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa funguo kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China, Chen Mingjian kama ishara ya makabidhiano ya Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) kilichopo, Burugo kata ya Nyakato Bukoba Mkoani Kagera tarehe 13 Oktoba, 2022.


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi iendelee

Namshukuru Mungu kwa kutukutanisha hapa, pia nashukuru serikali ya China kwa kuendelea kuwa msaada kwa nchi yetu likiwemo hili la uendelezaji ujuzi wa watu wetu.

Serikali ya watu wa China imekuwa ikitimiza ahadi zake kwa dhati na kwa uaminifu mkubwa. Walichofanya katika ujenzi wa chuo hiki ni mfano mdogo wa mambo ambayo wanafanya kwa ajili ya maendeleo ya Nchi yetu, China inaonesha kuwa rafiki wa kweli kwa maendeleo ya nchi yetu. Kazi kwenu watanzania katika kutumia majengo tuliyojengewa na vifaa tulivyowekewa. Asanteni sana Jamhuri ya watu wa China.

Kabla sijaja kwenye viwanja hivi nilitembezwa kuangalia chuo hiki, madarasa ni ya kisasa na karakana ni za kisasa kabisa, lakini pia kuna mitambo ya kisasa kabisa. Niliwaambia chuo kuwa watakaotumia mitambo hiyo wawe ni wenye weredi wa hali ya juu ili iweze kukaa kwa muda mrefu zaidi.

Kesho ni Siku ya Mwalimu Nyerere, wakati wa uhai wake alisema kuna maadui wa3, Ujinga, Umasikini na maradhi, na kila awamu inapiga na maadui hawa na hawa maadui hawawezi kuisha kwa kuwa kila siku watu wanazaliwa na wanazaliwa wakiwa na vitu hivi hivyo hii ni vita endelevu.

Ujenzi wa chuo hiki ni kuongeza weledi ili vijana wetu waweze kuajirika, na tumejenga VETA kwa kila Wilaya na sasa Tunakwend kujenga kila Mkoa.

Kwa nini tunajenga vyo hivi tunazungumzia tatizo la ajira tunasomesha watoto lakini watoto hawapi ajira, utafiti unaosha kuwa asilimi 12 ya ya vijana hawana ajira na kwa sababu asilimia kubwa ni vijana hivyo hii asilimia 12 tunaiongezea uwezo ili iweze kuajirika. Tunawajengea uwezo vjana ili waweze kukabiliana na changamoto hiyo.

Kama Alivyoongea waziri wa elimu Serikali ina mikakati ya kuhakikisha kila wilaya ina chuo ch aufundi stadi cha serikali, tunajua kuwa kuna vyuo vya binafsi lakini kwa wale watakaoshindwa kulipia vyuo vya binafsi waende kwenye vyuo vya Serikali.

Vyuo vipya na vile vya zamani vinahitaji vifaa na mitambo mipya kwa ajili ya kutoa mafunzo, tunatambua kuwa vyuo vinahitaji fedha kwa ajili ya kuweka mitambo ili viweze kutoa mafunzo stadi, Serikali inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kunua vifaa hivyo.

Vijana na hasa vijana wa Mkoa huu wa Kagera nawaasa kutumia fursa hii ya uwepo wa chuo hiki, jiungeni kwa ajili ya kupata mafunzo haya stadi ili muweze kuwa na ujuzi ambao utawasaidia kupata ajira lakini muweze kufungua viwanda vyenu vidogovidogo.

Lakini natoa agizo kwa Wakuu wa mkoa na Mkuu wa wilaya jipange kujua wanafunzi wangapi wanajiunga Chuoni hapa kwa kozi fupi na kozi ndefu wajulikane. Kuna asilimia 10 ya halmashauri wakute tayari halmashauri imejipanga. Wajulikane waliojiunga muweze kuwasaidia aidha kuwanunulia vifaa maana mkiwapa pesa watazitumia vibaya labda kama watasimamiwa kwa ukaribu sana lakini zuri ni kuwapa vifaa vinginevyo kutakuwa na watu wanamaliza VETA na hawana ajira, na hili ni agizo langu.

Gharama kubwa ya uendeshaji wa chuo itakuwa ya Serikali. Kutakuwa na malipo madogo kwa wanafunzi kujilipia hapa, naimani mzazi huwezi kukosa laki 2 au laki na 70 kumsimesha mtoto hapa.

Nimemsikia Waziri anasema kwenye Chuo hiki cha Veta hapa Kagera vijana 400 watakuwa wa mafunzo ya muda mrefu, kati ya vijana hao vijana 20 wanawake 10 na wavulana 10 wale ambao wanyonge hawana uwezo wa kujilipia nitawalipia mimi.

Vijana watakaomaliza chuo hiki cha ufundi waandaliwe mazingira mazuri ya kujiajiri na kuajiriwa, Mafundi stadi wengi wanahitajika katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati nchini kuna bomba la mafuta linalotoka Uganda kuja Tanzania kuna bwawa kubwa la Nyerere na kuna utekelezaji wa ujenzi wa barabara.

1665657138065.png

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amewataka walimu na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) kilichopo Burugo, Nyakato Bukoba kutunza miundo mbinu ya Chuo hicho ili iweze kuhudumia wanafunzi wengi zaidi.


0efd502a-a284-427f-92e2-504329e55a7c.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishuhudia utiaji Saini Mkataba wa Makabidhiano wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) kilichopo Burugo, Nyakato Bukoba kati ya Serikali ya China na Tanzania katika hafla iliyofanyika tarehe 13 Oktoba, 2022 Mkoani Kagera.
1665656830337.png
 
Safi Sana mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kwa kazi kubwa unayoendelea kuifanya katika kulitumikia Taifa letu, muda wote mh Rais wetu mpendwa yupo kazini kuwatumikia watanzania, muda wote mh Rais wetu mpendwa unamuona yupo kufungua miradi au kutatua kero au kutoa majibu kwa maswali ya wananchi au kutoa maelekezo, hakika Rais Samia Ni zawadi kwetu watanzania tunayopaswa kujivunia na kuiheshimu maana viongozi aina yake Hawazaliwi kila Siku na hawapatikani kila nchi.
 
Kupitia uzi huu naomba niwasilishe yafuatayo:
1. Tafadhali watu mnaoandaa sherehe za aina hii, acheni tabia ya kuleta wasanii wenu-diamond, Ali kiba, dula makabila nk, kwa nini mnashindwa kutoa nafasi ya kutumbuiza kwenye sherehe za aina hii kwa vijana wa shule za msingi na sekondari wa mahali husika? Pesa mnazowalipa hao wasanii si bora zichangie miradi ya maendeleo kwa shule za mahali sherehe zinapofanyika?Hawa wasanii wakiwemo TOT na wengine sisi wazazi wengine haturuhusu watoto wetu kusikiliza au kuangalia Sanaa zao..sababu uvaaji wao, nyimbo zao na uchezaji wao hauleti picha nzuri kwa watoto, huwezi ukahamisha mambo yanayotakiwa yafanyike kwenye kumbi za starehe yafanywe hadharani mbele ya watoto wasiotakiwa kwenda kwenye nyumba za starehe..unapomualika diamond hadharani unatoa ujumbe gani kwa watoto wa shule? Huko si kuhamasisha shauku ya wao kuanza kwenda nyumba za starehe? hizo mimba za utotoni zitapungua? nyimbo zao nyingi ni za mambo ya mapenzi na zinaa vitu ambavyo kimaadili mtoto haruhusiwi kusikiliza au kuona, Tafadhali wasaidizi wa Rais katazeni jambo hili, km kule kwenye mikutano ya ccm inafanyika, iishie huko huko..isifanyike kwenye sherehe za serikali..halafu mara zote wasanii wanaoalikwa ni wale wa kutoka Dar es salaam tu, na sherehe zikiwa Dr es salaam huoni wasanii kutoka mikoani wakitumbuiza dar es salaam..sisi wazazi hatutaki tabia hii iendelee! Bora kusiwepo muda wa kutumbuiza kuliko kuleta wasanii kutumbuiza.
 
Back
Top Bottom