Behaviourist
JF-Expert Member
- Apr 8, 2016
- 39,902
- 95,405
Kiongozi yeyote au raia yeyote anaesingizia masuala ya ukame kama chanzo cha matatizo katika sector ya umeme ikiwa ni pamoja na wewe ni binadamu mwenye akili fupi sana.Taarifa zilitoka mapema kuwa kutakuwa na ukame...tena toka mwezi wa nane!
Kwenye karne ya 21 vyanzo vya umeme vinapaswa kuwa diversified badala ya kutegemea chanzo kimoja cha umeme wa maji peke yake kwa sababu sasa hivi dunia inakumbwa na tatizo kubwa la global warming ambapo kama tulivyoshuhudia viongozi wa dunia wamekuwa wakisitasita katika kutatua tatizo hilo.
Suala la umeme katika level ya nchi linapaswa kuwa na long run solutions ikiwa ni pamoja na diversification katika vyanzo vyake.Kuna vyanzo vingi sana vya umeme kama vile gas na kadhalika.
Kusingizia ukame ni kuishiwa hoja na pumzi katika kuongoza.Dunia ya sasa hivi haipo tena kwenye zama za akili fupi kama hizo.WTF!!!
Kusingizia ukame ni akili za chekechea ambazo ndiyo naona zimejaa hapa JF pamoja na huko Serikalini.