Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,191
- 4,104
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akifungua barabara ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass) km 42.4 Ngaramtoni Arusha, leo Tarehe 22 Julai, 2022
=======
Hotuba ya Rais Samia, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania
Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mungu na pia kwa viongozi wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kujumiaka nasi kwenye ufunguzi wa barabara hii muhimu pamoja na wakandarasi na wananchi wote na wote waliohusika katika kukamilisha mradi huu. Na kwa dhati kabisa nitoe shukrani zangu kwa bank ya maendeleo Afrika waliowezesha ujenzi wa barabara hii.
Kukamilika kwa barabara hii italeta faida za kukuza uchumi na shughuli nyingine katika jumuiya ya Afrika Mashariki. Pamoja na barabara hii sisi Tanzania tunaendela na mradi wa barabara za kutuungunisha na nchi jirani kwa barabara, reli anga na majini ili usafiri na usafirisha uweze kufanyika kwa urahisi ndani ya Afrika Mashariki.
Napenda kutoa Rai kwa watu wote wanaoishi maeneo yote ambayo miradi hii inapita waweze kuchukua fursa za kujinufaisha kiuchumi ili waweze kupata fedha za kujikimu na kufanya maendleo.
Lakini barabara hizi zinatumia gharama kubwa na kumeanza kutokea uhalifu kwa watu kuharibu miondombinu, kwa watu kumwaga mafuta barabarani ambayo yanaharibu barabara lakini pia watu wanatupa takata kwenye madaraja na wengine wanaharibu miundombinu na kusababishia hasara Serikali.