Rais Samia aingilie kati tatizo la wazee kuwaoa mabinti wadogo; aagize sheria ya ndoa kurekebishwa

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,802
18,225
Jambo wakuu!

Sitaki kuwachosha, naingia kwenye mada moja kwa moja. Kumekuwa na wimbi baya la wazee kuwaoa mabinti wadogo ambao ni sawa na watoto au wajukuu zao na kibaya zaidi, baadhi ya wazee hao waliwahi kulitumikia taifa kwa nyadhifa kubwa.

Tofauti na matarajio ya wengi kuwa wazee hawa walipaswa kuonyesha mfano bora kwa watanzania, badala yake wamegeuka kuwa kero kwa kugeuza uharibifu wa mabinti kuwa jambo la umaarufu. Halafu wamekuwa siku zote wakitamba kabla na baada ya kufanya vitendo hivyo wakidhani kuwa wanafanya jambo zuri. Inasikitisha sana.

Baadhi ya viongozi wakubwa wa kitaifa ambao wamejitumbukiza kwenye mchezo huu mchafu wa kuwaoa mabinti wadogo ni Profesa Kapuya, Pius Ngwandu, Abrahamu Mengi na kesho tarehe 24/03/2022 mzee Augustine Lyatonga Mrema ametangaza kufunga ndoa na binti mbichi kabisa anayelingana na wajukuu zake. Namuomba Mh mama Samia uingilie kati jambo hili kwa kuagiza Wizara ya Sheria kuifanyia mabadiliko sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ili kuwasnusuru mabinti wasiolewe na wazee vikongwe.

Sheria iweke tofauti ya umri wa watu wanaofaa kuoana; ikiwa tofauti ya umri itakuwa kubwa (kwa mfano miaka kuanzia 20 na kuandelea) basi ndoa hiyo ichukuliwe kuwa ni batili na mhusika (mume) atakayekuwa ametenda kosa hilo achukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupigwa faini, kufungwa jela au vyote kwa pamoja. Watanzania wanapaswa kuiga mfano bora wa Pius Msekwa na John Malecela waliowaoa watu wazima wanaolingana nao kiumri.

Mama Samia umefanya jambo jema kuwaruhusu mabinti waliozaa kurejea shule kutimiza ndoto zao za kielimu. Hapa umeupiga mwingi mama yangu mpendwa. Adhma yako ya kutoa elimu kwa mabinti haiwezi kutimia ikiwa mabinti hao unaowapigania kurudi shule kupata elimu watakwapuliwa na wazee wenye uchu wa ngono.

Nakuomba pia ushughulikie tatizo hili la mabinti wadogo kuolewa na baba au babu zao ili kuwakoa mabinti wanaoingia kwenye mtego huu wa fisi wapenda ngono.

Watu wanaweza kuchukulia jambo hili kuwa dogo lakini ukiliangalia kwa jicho la latu, hili ni tatizo kubwa sana linaweza kuathiri maadili ya kitaifa na ukosefu wa uzalendo na utii wa sheria. Ikiwa wazee wataendelea na tabia yao hii ya kuwaoa mabinti wadogo kuna uwezekano vijana wadogo wakiume nao wakaanza kuwaoa wanawake watu wazima ili kulipiza kisasi. Ndio.

Ipo siku vijana watakosa mabinti wa kuwaoa na kuwageukia vikongwe. Endapo nchi itafikia hatua hii, maadili ya kitaifa yatamomonyoka kwa kiasi kikubwa. Kuliko kusubiri ukuta uanguke tujenge mpya, nakuomba mama Samia uingilie kati suala hili kabla hali haijwa mbaya sana.

Nawasilisha.​
 
Jambo wakuu!

Sitaki kuwachosha, naingia kwenye mada moja kwa moja. Kumekuwa na wimbi baya la wazee kuwaoa mabinti wadogo ambao ni sawa na watoto au wajukuu zao na kibaya zaidi, baadhi ya wazee hao waliwahi kulitumikia taifa kwa nyadhifa kubwa. Tofauti na matarajio ya wengi kuwa wazee hawa​
Sasa wewe kwa akili zako hilo lina athari gani kwa uchumi wetu,.....bora aboreshe elimu watu kama nyie mtakua na wide analysis en understanding on basic human rights hamtaandika ujinga kama hu
 
Jambo wakuu!

Sitaki kuwachosha, naingia kwenye mada moja kwa moja. Kumekuwa na wimbi baya la wazee kuwaoa mabinti wadogo ambao ni sawa na watoto au wajukuu zao na kibaya zaidi, baadhi ya wazee hao waliwahi kulitumikia taifa kwa nyadhifa kubwa. Tofauti na matarajio ya wengi kuwa wazee hawa​
Kwa Mujibu wa Katiba yetu miaka 18 ni mtu mzima mwenye nafasi na uhuru wa kufanya maamuzi mbali mbali..
 
Sasa wewe kwa akili zako hilo lina athari gani kwa uchumi wetu,.....bora aboreshe elimu watu kama nyie mtakua na wide analysis en understanding on basic human rights hamtaandika ujinga kama hu
Nchi ikiingia katika taharuki kwa wazee kuwaoa mabinti na vijana wa kiume kuwaoa vibibi vikongwe huo uchumi utaujengaje mkuu?
 
Kwa Mujibu wa Katiba yetu miaka 18 ni mtu mzima mwenye nafasi na uhuru wa kufanya maamuzi mbali mbali..
Kwa bahati mbaya ni kuwa baadhi ya mabinti wanaoolewa na wazee hawa ni under 18 :oops: :oops: :oops:
 
Back
Top Bottom