Rais Samia ahsante sana, Nikki wa Pili ni uteuzi bora kabisa

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,174
27,217
Nani kama mama? Ukikutana na watu 10, basi 7 Kati yao watakuambia wanampenda sana mama kuliko baba.

Mama Samia kweli amedhmairia kuifikisha Tanzania kwenye nchi ya asali na maziwa, niseme wazi kuwa mimi sijawahi kuamini kiongozi Bora anaweza kutoka nje ya mfumo wa CCM.

Ujio wa mama Samia ni ujumbe kuwa CCM bado Ina hazina ya viongozi wenye maono na wenye uwezo mkubwa Sana
Mama Samia siku ya jana umetufurahisha sana watanzania kwa kumteua the genius NIKKI WA PILI, hakika ni furaha isiyomithirika.

Nikki wa Pili ni genius, ni kijana shupavu, hodari, mpole, mnyenyekevu na mwenye busara ya hali ya juu sana. Waswahili wanasema usiandikie mate wakati wino ungalipo. Muda utasema kuhusu Nikki wa Pili. Namuona mbali sana.

Mama umetutendea vyema sana kumleta Nikki wa Pili.

Kwa wasiomjua huyu kijana nitaeleza kwa ufupi hapa chini.

Nikki alizaliwa na kusomea Arusha, alipomaliza darasa la 7 na matokeo kutoka hakupata bahati ya kuchaguliwa (kipindi kile kufaulu kulikuwa kugumu sana) hivyo Nikki akakaa nyumbani kutokana na familia kutokuwa na uwezo wa kumsomesha shule binafsi. Hivyo akabidi ajatafute kibarua kwenye kuuza duka soko la kilombero mkoani humo.

Baada ya miezi mitatu ikatoka second selection, na hatimaye jina la Nickson Simon likatoka na hivyo kuendelea na masomo shule ya secondary Arusha.

Ilipofika form 4 Nikki akapata Division 1 na kupangiwa kwenda Kigoma Secondary kwa ajili ya masomo ya Advance(A-Level).

Mazingira ya kwenda huko hayakuwa mazuri kwa maana ilibidi aungeunge sana ili kufika Kigoma na kuanza masomo.

Na alipomaliza Form 6 akapata Div 1 na kuamua kwenda kujiunga na chuo kikuu Cha Daressalaam (UDSM).

Kipindi yupo UDSM, kaka yake Joh Makini alikuwa taayari msanii mkubwa sana Tanzania akitmaba na ngoma zake kadhaa ikiwemo chochote popote.

Hivyo Joh Makini alihitaji kufanya wimbo mwingine na siku anaenda studio pale Kama kaea records ubungo alikuwa ameongizana na Nikki wa Pili ambae yeye alikuwa anaenda zake mabibo hostel.

Joh akiwa nje anapasha sauti ili aanze kurekodi wimbo maana beat ilikuwa tayari. Ghafla Nikki wa Pili akaomba afanye kama anajaribu kwenye hiyo beat. The rest is history.

Watu wote studio walikuwa hawaamini wanachokisikia, na baadae wimbo wa "Niaje Nivipi" ulikuwa mkubwa kupita maelezo na kumtambulisha rasmi Nikki wa Pili.

Nikki wa Pili akaamua kuendeleza kutoa nyimbi zingine kama ; Good Boy, Excellent, Feelings, Higher, Kila wakati, Pea, Kiujamaa n.k

Hii story itaendelea.

AHSANTE SANA MAMA SAMIA KWA ZAWADI HII YA NIKKI WA PILI, MUNGU AKUBARIKI SANA

Screenshot_20210620-112810_1.jpg
 
Akafanyee KAZII aache porojo

Wengi wanateuliwa wakosafi Sana wakiingia uwanjan

Mkuu n mapepo sutiana yanawavaa gafla
 
Back
Top Bottom