Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Hamduni-TAKUKURU, Makala-Dar, Kafulila-Arusha, Chalamila-Mwanza, Sendiga-Iringa, Makongoro...

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,789
11,931
Salaam Wakuu, Huu ndo uteuzi rais kafanya.

Rais Samia afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na Taasisi: Bw. Mwakitalu kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Hamduni Mkuu wa TAKUKURU, Amos Makala kawa mkuu wa Mkoa wa Dar, Kafulila kawa mkuu wa Mkoa Arusha, Chalamila kawa mkuu wa Mkoa Mwanza, Queen Sendiga kawa mkuu wa Mkoa Iringa(Queen alikuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Uchaguzi wa Oktoba 2020), Makongoro Nyerere kawa mkuu wa Mkoa Manyara.

Chalamila kawa mkuu wa Mkoa Mwanza(Albert Chalamila alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya), Kunenge kawa mkuu wa Mkoa wa Pwani( Aboubakar Kunenge alikuwa Mmkuu wa Mkoa wa Dar), Kagaigai kawa mkuu wa Mkoa KIlimanjaro(Stephen Kagaigai alikuwa Katibu wa Bunge), Ali Hapi kawa mkuu wa Mkoa Tabora(Hapi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa). Anna Mngwira amesitaafu alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo atapangiwa kazi nyingine.

=====

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa na watendaji wakuu wa taasisi kama ifuatavyo;

1. Amemteua Bw. Anthony John Mtaka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mtaka alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

2. Amemteua Bi. Zainab Rajab Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi. Kabla ya uteuzi huo Bi. Telack alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na anachukua nafasi ya Bw. Godfrey Zambi ambaye amestaafu.

3. Amemteua Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kabla ya uteuzi huo Bw. Luhumbi alikuwa Mkuu wa Geita.

4. Amemteua Bw. Juma Zuberi Homera kuwa Mkuu wa Mbeya. Kabla ya uteuzi huo Bw. Homera alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

5. Amemteua Bw. Martin Reuben Shigella kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Kabla ya uteuzi huo Bw. Shigella alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga na anachukua nafasi ya Bw. Loata Erasto Ole Sanare ambaye amemaliza muda wake.

6. Amemteua Brig. Jen. Marco Elisha Gaguti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara. Kabla ya uteuzi huo Brig. Jen. Gaguti alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera na anachukua nafasi ya Bw. Gelasius Gasper Byakanwa ambaye atapangiwa majukumu mengine.

7. Amemteua Bw. Albert Chalamila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Kabla ya uteuzi huo Bw. Chalamila alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

8. Amemteua Bw. Aboubakar Mussa Kunenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Kabla ya uteuzi huo Bw. Kunenge alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Mhandisi Evarist Welle Ndikilo ambaye amestaafu.

9. Amemteua Bw. Joseph Joseph Mkirikiti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mkirikiti alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara na anachukua nafasi ya Bw. Joachim Leonard Wangabo ambaye amestaafu.

10. Amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mahenge alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na anachukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amestaafu.

11. Amemteua Dkt. Philemon Rugumiliza Sengati kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Sengati alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

12. Amemteua Bw. John Vianney Mongella kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mongella alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

13. Amemteua Bw. Ally Salim Hapi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora. Kabla ya uteuzi huo Bw. Hapi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

14. Amemteua Bw. Adam Kigoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Kabla ya uteuzi huo Bw. Malima alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

15. Amemteua Bw. David Zacharia Kafulila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Bw. Kafulila anachukua nafasi ya Bw. Idd Hassan Kimanta ambaye amestaafu.

16. Amemteua Bw. Amos Gabriel Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Bw. Makalla anachukua nafasi ya Bw. Aboubakar Mussa Kunenge ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

17. Amemteua Bi. Rosemary Staki Senyamule kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita. Bi. Senyamule anachukua nafasi ya Bw. Robert Gabriel Luhumbi ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

18. Amemteua Bi. Queen Cuthbert Sendiga kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa. Bi. Sendiga anachukua nafasi ya Bw. Ali Salim Hapi ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Tabora.

19. Amemteua Mej. Jen. Charles Mbuge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Bw. Mbuge anachukua nafasi ya Mej. Jen. Marco Elisha Gaguti ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

20. Amemteua Bi. Mwanamvua Mrindoko kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi. Bi. Mrindoko anachukua nafasi ya Bw. Juma Zubeir Homera ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

21. Amemteua Bw. Stephen Kagaigai kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kabla ya uteuzi huo Bw. Kagaigai alikuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na anachukua nafasi Bi. Anna Elisha Mghwira ambaye amestaafu.

22. Amemteua Brig. Jen. Wilbert Augustine Ibuge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. Brig. Jen. Ibuge anachukua nafasi ya Bi. Christine Mndeme ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

23. Amemteua Bw. Omary Tebweta Mgumba kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Bw. Mgumba anachukua nafasi ya Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ambaye amestaafu.

24. Amemteua Bw. Makongoro Nyerere kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Bw. Makongoro Nyerere anachukua nafasi ya Bw. Mkirikiti ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

25. Amemteua Bw. Thobias Emir Andengenye kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma. Bw. Andengenye anaendelea na wadhifa huo katika Mkoa huo huo wa Kigoma.

26. Amemteua Bw. Marwa Mwita Rubirya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Bw. Rubirya anaendelea na wadhifa huo huo katika Mkoa huo huo wa Njombe.

Mhe. Rais Samia amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa taasisi zifuatazo;

1. Amemteua Mhe. Balozi Joseph Edward Sokoine kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Mhe. Balozi Sokoine anachukua nafasi ya Mej. Jen. Ibuge ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

2. Amemteua Bi. Nenelwa Mwihambi kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bi. Mwihambi anachukua nafasi ya Bw. Stephen Kagaigai ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

3. Amemteua Dkt. Edwin Paul Mhede kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART). Anachukua nafasi ya Mhandisi Ronald Muberwa Lwakatale ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

4. Amemteua Bw. Sylvester Antony Mwakitalu kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). Bw. Mwakitalu anachukua nafasi iliyoachwa na Bw. Biswalo Mganga ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

5. Amemteua Bw. Joseph Pande kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka (DDPP). Bw. Pande anachukua nafasi ya Bw. Edson Athanas Makallo ambaye atapangiwa majukumu mengine.

6. Amemteua Kamishna Msaidizi wa polisi (ACP) Salum Rashid Hamduni kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). ACP Hamduni anachukua nafasi ya Mej. Jen. John Mbungo ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Aidha, Mhe. Rais Samia amempandisha cheo ACP Hamduni kuwa Kamishna wa Polisi (CP).

7. Amemteua Bi. Neema Mpembe Mwakalyelye kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.

Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 15 Mei, 2021 na wataapishwa tarehe 18 Mei, 2021 kuanzia saa 9:00 alasiri, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
1621073914629.png

1621073856109.png

1621073891223.png
 
Chalamila yuko pale pale kama mkuu wa mkoa. Kelele za kina Maria Sarungi hazijasikilizwa.

Hamduni afanye kazi kitaalam, aachane na vitisho vya magwanda ya kijeshi kama ya aliemtangulia. Akumbuke PCCB ni law enforcement agency or investigative services hivyo afanye kazi kitaalam.
 
Back
Top Bottom