Rais Samia afanya mazungumzo na Rais Paul Kagame, wakubaliana kukuza uhusiano

Tanzania itatuchukua miaka mingi kujitambua.kweli Rwanda Ni mahala pa kwenda kujifunza.

..wakati mwingine huwa hawana cha kusema hivyo inabidi waongeze na UONGO.

..Kwa mfano, kuna wakati Waziri Mkuu wa Ethiopia alikuja Tanzania halafu Magufuli akadanganya eti wamekubaliana Ethiopia itaanza kutumia bandari ya Dar Es Salaam.
 
IT sio tu kukaa kwenye computer, mfano rwanda wanatengeneza simu zao wenyewe wanauza ndan ya nchi
Kwani sisi tunashindwa nini kutengeneza simu?
Tatizo ujuzi na uwezo wetu havithaminiwi na wenye mamlaka kwa sababu wanazozijua wao.
 
sasa wewe unachukua engine ya pikipiki, feni ya rejeta alafu unaunda ndege nndo unamaanisha hizi? rwanda wanatengeneza chips from 0 dogo
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema mazungumzo kati yake na Rais Paul Kagame yamejikita zaidi katika kuimarisha na kukuza uhusiano wa kiuchumi.

Amesema, "Kubwa tulilokubaliana ni kukuza ushirikiano zaidi. Tanzania na Rwanda tuko kwenye Biashara na Uwekezaji, bado tuna fursa nyingi tunazoweza kutumia".

Ameongeza, "Leo tumesaini makubaliano kwamba tunaendelea kuweka uhusiano mkubwa kwenye matumizi ya TEHAMA. Rwanda mpo mbele yetu na tupo tayari kuja kujifunza kwenu".

Rais Paul Kagame amesema Taifa hilo lipo tayari kufanya kazi kwa karibu na Tanzania ili kuharakisha kufufua Mataifa hayo na Ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla kufuatia mlipuko wa janga la COVID-19

Kagame amesema changamoto zinazoukabili Ukanda wa Afrika Mashariki zinaweza kutatuliwa kwa mshikamano na fursa zinazonufaisha pande zote

Rais Samia Suluhu Hassan yupo Nchini Rwanda kwa ziara ya siku mbili

Subiri yaje yamkute yaliyowakuta Uganda. Mwisho ni kudukua simu za watu wake
 
Madikteta wakutane kigali
 
Back
Top Bottom