Rais Samia aduwaza wachumi nchini

#Nakupenda Tanzania
IMG_20211116_120145.jpg
 
Mkuu si ulisema nchi haina Mungu ndio maana mvua hazinyeshi ghafla unakubali kuwa SSH amefanikiwa??

CCM bila unafki
Mjinga wewe mazao yaliyouzwa kuingiza pesa za kigeni yalipandwa kipindi Cha magufuli unanichokoza au!.hayo mauzo ya mazao nje yalipandwa na kukomaa kipindi Cha mama Samia? Nikisifu serikali niache ukiingia ndani nitakwambia tunasubiri mazao tlyatakayopandwa kwenye huu ukama na yeye avune ajidai mauzo ya nje

Haya majidai Ni ya kipindi Cha magufuli
 
Kazi kubwa na nzuri anazozifanya Rais Samia Suluhu Hassan zimewaduwaza wachumi,

Hii ni baada ya akiba ya fedha za kigeni ( Gross official foreign reserves ) kuongezeka zaidi ndani ya miezi miwili tu nakufikia $6.7BL sawa na TZS 15.41 kutoka $5.9BL sawa na TZS 13.57 mwezi Septemba,

Ongezeko hili ni karibu TZS 2 trilioni linalomfanya Rais Samia ndani ya kipindi chake hiki kifupi kuongeza Jumla ya TZS 4Trilion kwenye hifadhi ya fedha za kigeni,rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na Rais yeyote wa awamu yeyote,

Ongezeko hili linachangizwa zaidi na uuzaji nje ( Exports ) wa bidhaa pamoja na huduma hasa mazao ya Chakula kama mchele, Mahindi, maharagwe na mboga mboga,

Kwamsiojua,ongezeko hili ni mbali ya ongezeko la gharama za uagizaji mafuta nje zilizokua kwa 18.3% nakufikia $1.7BL

Jambo la Pili ni Uwekezaji mkubwa kutoka inje Foreign Direct Investments ( FDIs ) uliofikia $2.9BL sawa na TZS 6.7Trilioni,

Ukuaji huu wa uwekezaji ni sawa na mara sita zaidi ya uwekezaji wote uliofanywa mwaka uliopita katika kipindi kama hicho cha kati ya Mwezi Machi na Agosti,

Ongezeko hili linaweza kuagiza bidhaa na huduma nje kwa kipindi kisichopungua karibu miezi saba rekodi ambayo haijawahi kufikiwa tangu kuwako wa Taifa hili miaka sitini ( 60 ) iliyopita,

Tanzania kwa sasa ndio nchi inayokuza hifadhi yake kwa kasi Ukanda mzima wa Africa Mashariki na Tumevuka lengo la EAC lakuwa na akiba ya kuagiza bidhaa na huduma nje kwa kipindi kisichopungua miezi 4.5

View attachment 2018173
Rubbish
 
Hilo jarida limeongelea kuhusu umeme? Ama maji?

Kuongeza reserve huku hakuna maji wala umeme kuna faida gani kwa watanzania?

Juzi wamewgiza ndege nne za zaidi ya Bilioni 780 wakati watu hawana maji wala umeme, hii nchi ina vituko.

Huyu mama uwezo wa kuongoza nchi hana.

Faida ya hiyo reserve ni kua na shule kama hizi.

Usishangae wakikwambia hiyo shule iko Somalia au Iraq maana maccm hawachelewi kuhamisha magoli bila kutazama waliposimama
 
Mkuu si ulisema nchi haina Mungu ndio maana mvua hazinyeshi ghafla unakubali kuwa SSH amefanikiwa??

CCM bila unafki
Hayo.mazao yameuzwa nje Sana kuingiza pesa za kigeni yalipandwa kipindi Cha mcha Mungu Magufuli yamevunwa kipindi Cha Samia


Tunasubiri ya kwake yatakayopandwa kipindi chake ndio uje na hoja Kama yeye mcha Mungu au kafiri

Mavuno yaliyopaisha uchumi yalipandwa kipindi Cha Uraisi wa Magufuli sio Uraisi wa Samia
 
Hayo.mazao yameuzwa nje Sana kuingiza pesa za kigeni yalipandwa kipindi Cha mcha Mungu Magufuli yamevunwa kipindi Cha Samia


Tunasubiri ya kwake yatakayopandwa kipindi chake ndio uje na hoja Kama yeye mcha Mungu au kafiri

Mavuno yaliyopaisha uchumi yalipandwa kipindi Cha Uraisi wa Magufuli sio Uraisi wa Samia
Mungu Magifuli!!
 
uchumi gani ambao hauna refection yeyote kwa watanzania!?, bidhaa Bei znapanda,zingine hazpatkani kiurahisi,umeme umekuwa shaka na hofu ,miradi ya kimkakati haiendi !!??, Ni ujinga kutuletea porojo hapa!!
 
pesa za mikopo unasema pesa imeongezeka. yaani wewe una shiling elfu 50 uede kwa paulo umkope akakupa milion ukaenda kwa john ukakopa ukapewa milion 2 zikafika milion 3 na elfu hamsini yako ufike nyumbani watoto waanze kujitapa baba yetu ni tajiri kwa wiki tu kaingiza milion 3 hawajui hizo pesa ni mkopo unatakiwa urudishwe tena zaidi
 
Angalia utaambiwa umetumwa na Makamba
Sisemi waiuze TANESCO wakae nayo tuu kama wanataka ila waachie private sector wafanye hiyo biashara bila kuipendelea TANESCO, sheria za sasa haziruhusu mtu binafsi kuzalisha na kuuza umeme, sheria ya sasa unaweza kuzalisha umeme lakini lazima uwauzie TANESCO kwa bei watakayokupangia kusambaza huruhusiwi, matatizo ya umeme na maji nchi nyingi zimeshasahau na sio luxury tena, monopoly ya TANESCO ndio matatizo yote yanapoanzia, tubadili sheria tuachane na huu ujinga wa kututia umaskini
 
Upo sawa ila hili pendekezo lina hatari zake pia.

Labda umeme wa majumbani na biashara ndogo ndogo ndo watu binafsi wapewe halafu mambo mengine yote yanayohusu nchi kama jeshi, miradi mikubwa, viwanda nk umeme uwe wa serikali.
Sijui huo uwoga unatoka wapi, hata China ambao tunafikiri ni communist, serikali yao haifanyi hizo biashara tena wanachofanya ni kuwapa pesa au kuwahakikishia mikopo sector binafsi ili wafanye vitu vyao, umeme ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi na bila umeme umaskini hautoisha Tanzania
 
Unapokuwa unaongelea mambo ya uchumi hebu jiongelee mwenyewe sio kutujumlisha sote.
 
Yeye ni Mungu wa kuzuia ukame? Kwa akili zake sasa ndio unaona anakomaa na gas Ili hata ukame ukija usipate Mgao.

Samia anawanyima usingizi,go Samia go hadi nyongo ziwatokee puani 👇

View attachment 2018239

View attachment 2018240

View attachment 2018241

View attachment 2018242

View attachment 2018243

View attachment 2018244

View attachment 2018245

View attachment 2018246

View attachment 2018247
Mkuu wewe ni msaada kwa CCM na Taifa kwa ujumla wake,

Hongera Sana Pacha We proud on you
 
Back
Top Bottom