Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,105
- 35,046
Tangu Rais Samia ashike madaraka amekuwa busy sana kuzing'ang'ania na kuzipigia debe siasa za kuwaenzi na kuuenzi utamaduni wa machifu na watemi hapa Tanzania. Hapa nitaweka kweli kadhaa kuhusu ubaya wa siasa hizo kwa nchi yetu na vizazi vijavyo.
1. Utamaduni wa watemi na machifu ni utamaduni wa kikabila na kikoo kwa 100%. Hawa hawafanani, hawakubaliani na hawakai chungu kimoja. Unalenga kuwagawa watanzania kuliko kuwaunganisha.
2. Utamaduni wa watemi na machifu umezungukwa na mfumo dume kwa karibu 100%. Kadri unavyopaliliwa ndivyo ambavyo mfumo dume unakuzwa na kuota mizizi kwenye jamii.
3. Kwa sehemu kubwa sana tamaduni za watemi na machifu zimejikita kwenye ubagani, matambiko, ushirikina na mambo ya kale. Sioni mantiki yoyote kwa serikali kuukumbatia sasa kwenye karne ya 21.
4. Kwa sehemu kubwa utamaduni wa tawala za machifu unakinzana na mifumo ya tawala rasmi za kiserikali na kisheria. Huwa ni vitu visivyoweza kwenda sambamba. Kuimarika kwa tawala rasmi za kiserikali automatically kuliua tawala za machifu na watemi, kuzifufua upya hizo tawala za machifu sasa ni kuhatarisha uwepo wa tawala rasmi za kisheria na kiserikali.
5. Utamaduni wa tawala za watemi na machifu kwa sehemu kubwa umedhoofika, kufifia, kuparaganyika au ulishakufa kwa jamii nyingi sana hapa Tanzania. Wengi watakaoibuka sasa na kuitwa watemi au machifu huenda watakuwa waganga wa kienyeji, wazee wa kikoo, matapeli (wazee wa fursa), wajumbe wa CCM wa nyumba kumi kumi (wazee wazee). Kiuhalisia utakuta sio watu halisi wa kuwakilisha watemi na machifu wa zama zile. Kuwakumbatia watu wa namna hiyo ni kupoteza muda na rasimali.