Rais Samia achana na kuikumbatia CCM, fanya kazi zenye Maslahi mapana kwa Watanzania

Bila kusahau roho yake mbaya
Shujaa John Pombe Joseph Magufuli atabaki kuwa rais wa karne, mwamba, jasiri, mbeba maono na mtekelezaji...

Tusimlinganishe Rais Samia Suluhu Hassan na JPM. Sisi tuangalie utekelezwaji miradi na ilani ya kurasa 303

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan

Kazi iendelee
 
Sawa hatukatai Kaua uchumi lakini tunataka kuona miradi mingine mikubwa kama Ndege ,Madaraja,SGR,Nyerere project,Terminal 3,Stendi ya Mbezi,Viwanda,Barabara,madarasa,Elimu bure,Kukomesha rushwa, nidhamu kazini.... na mengineyo mengi... Tunataka kuyaona! Uchumi uliuliwa lakini hayo yalifanyika... tuone ya kwake sasa...

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Kweli mkuu, yaani wananchi wa Nchi hii inatakiwa kuwatawala kwa mkono wa Chuma, maana mijitu haina shukrani, namshauri mama hakuna kufuta sheria za hujumu uchumi wala money laundering, na asiruhusu uhuru wa vyombo vya habari, awaminye kisawasawa , hii nchi ili wakuheshimu inatakiwa uwe kiongozi katili na mwenye kutoa hotuba za kibabe,sio za kumfariji yoyote
Kweli kabisa! Vinginevyo utakuta muda umeisha na hakuna ulichofanya! Siasa tupu na maendeleo hakuna!

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Hata wakifanya ili mradi tu Kama hai affect utendaji kazi wao aachane nao...Kuna mamlaka na dola zenye nguvu dunian Kama marekani wanamuziki wanaikosoa waziwazi wanamkejeli raisi waziwazi lakini ndio taifa lenye nguvu duniani Kuna mambo sio ya msingi asifanye kosa Kama la magufuli kuanza kupambana na watu wanao ongea siku akitoka wataongea tu!! Afanye kazi tu iliompeleka ikulu
Marekani,Ujerumani na nchi zilizoendelea zimeshapita hizi hatua tuliyopo! Usijifananishe nao! Bila kuziba masikio Tanzania hauwezi kufanya maendeleo watu watafanya siasa tu na hakutakua na maendeleo

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Mleta uzi huna lolote, ndio nyie mkipewa nafasi hata wiki humalizi unashindwa kuongoza.
Unadhani u rais ni kazi ndogo kiasi cha wewe kumkosoa Rais?
Tafuta kazi ya kufanya utunze familia yako .
Nchi hii ni mali ya Watz wote bila kujali itikadi zao. Rais anapaswa kufanya kazi kwa mujibu wa Katiba alioapa kuilinda. Akifanya kazi kama Mtangulizi wake yaani Rais wa kundi fulani au kama M/Kiti wa CCM hatoboi. Na dalili zinaonyesha kuwa ameshatekwa na Kundi fulani.
 
Mama Samia alionekana ni mtu atakaye kuja kufanya mageuzi makubwa lakini nasikitika hakuna kitu chochote mpaka sasa ambacho amefanya.
Mkuu, jinyonge tu uachane na bughudha za wabongo.
Kwa jinsi ulivyokonfuzidi mtu kama wewe ukipewa nafasi ya kumshauri mama nchi inageuka kuwa kama kilabu cha pombe za kienyeji.
 
Kwa kifupi naona anajaribu kuuma na kupuliza ili amridhishe kila mtu, hii kwangu ni sawa na kupiga msamba au kuzunguka mbuyu kama hana vipaumbele vyake, atapoteza muda wote hapo.
Ndiyo maana mwendazake alichagua njia moja tu.
 
Kuna watu walipotea,kupigwa risasi,kuuwawa yeye kama Amiri Jeshi Mkuu;Mkuu wa vikoasi vya ulinzi na usalama hakuchukua hatua yeyote,hadi anaelekea Jongomeo.
Aliminya stahiki za wafanyakazi kipindi chote cha utawala wake.
Maisha ya Watanzania yamekuwa magumu sana toka kipindi cha Mwalimu Nyerere hii hali ilishuhudiwa sababu tu ya kufanya miradi ambayo hatuna uhakika wa return,huenda ni ''White Elephant''.
Ukabila na ukanda umezidi sana kipindi cha huyu mwamba.Ni kipindi ambacho Watanzania wamegawika naweza sema toka uhuru hatujawahi shuhudia hii hali.
Kuwa na roho ya visasi kwa wale wanaomkosoa hata kama ni kwa nia njema.
Hayo ni kwa uchache tu....
Kuna watu walipotea,kupigwa risasi,kuuwawa yeye kama Amiri Jeshi Mkuu;Mkuu wa vikoasi vya ulinzi na usalama hakuchukua hatua yeyote,hadi anaelekea Jongomeo.

Watu wangapi wanakufa kwa siku? Je Watoto wanaokufa kwa malaria mahospitalini kila siku sio watu? Au hao hakupaswa kupambana kuleta madawa mahospitalini kuwaokoa?Unataka kila siku aende TBC kutoa pole kwa kila kifo?


Aliminya stahiki za wafanyakazi kipindi chote cha utawala wake.
Maisha ya Watanzania yamekuwa magumu sana toka kipindi cha Mwalimu Nyerere hii hali ilishuhudiwa sababu tu ya kufanya miradi ambayo hatuna uhakika wa return,huenda ni ''White Elephant''.

Je,kuna mfanyakazi aliyenyimwa mshahara wake katika kipindi chake? Watanzania hawahawa wanaosomeshwa bure na mikopo ya chuo kuongezwa maradufu? Au watanzania wapi? Hawahawa ambao wanapita barabara nzuri au kwenye reli iliyoboreshwa? Hawahawa walioboreshewa huduma za afya? Mradi wa umeme utakaoleta MW zaidi ya 2000 haufai kwa taifa kwa kupunguza gharama za umeme? Mradi wa SGR,Terminal 3,Mbezi Stand haifai?


Ukabila na ukanda umezidi sana kipindi cha huyu mwamba.Ni kipindi ambacho Watanzania wamegawika naweza sema toka uhuru hatujawahi shuhudia hii hali.
Kuwa na roho ya visasi kwa wale wanaomkosoa hata kama ni kwa nia njema.
Hayo ni kwa uchache tu....

Unaweza kutoa ushahidi? Kwanza ukabila na ukanda wewe unakudhuru vipi as long as maendeleo yenye tija yanaonekana? Hii ni rubbish point

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Mpe muda mama yetu azoee kiti cha uraisi,tumpe baada ya mwaka mmoja.
Tusipende kumkatisha tamaa,tena tumepata Raisi msikivu.
 
CCM iondolewe halafu apewe nani nchi? Tuwape wezi wabinafsishe nchi iwe ya familia zao?

Mkiambiwa watu waliupenda wizi wa Magufuli mlikuwa mnang’aka sasa subirieni ufisadi wa kutisha ambao utatangazwa wazi wazi mnamo 2025 ikiwa hamna maendeleo yoyote yaliofanyika na kuonekana na tija zaidi ya porojo tu halafu mtamtafuta mchawi!

Tunarudi kwenye Era ambayo wanasiasa watajitajirisha wao na familia zao bila mipaka na kuwasahau kabisa wapiga kura wao bila aibu!
Nyie watu wapuuzi sana kufanya Jambo lile lile kisha utegemee matokeo tofauti ni UPUMBAVU.....eti mliupenda wizi wake simumfuate sasa huko aliko.....

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Wazanzibar ndio hamna machogo, ukumfunua maza ilo shungi utakutana na bonge la bichwa bapa la hatari.

Ah ah wala hayavutii mabichwa ya kizanzibar, midada yao tu ndio mitamu,
Maraisi wa Bara hukuwaambia hivyo unatuonea Wazenji... Na kila mwamba ngozi huvutia kwake zamu yenu machogo ishapita
 
Hakika mimi uwa nasema ukweli bila sisi kama nchi kuacha kuishi ya Uongo uongo hakuna maendelea ambayo tutakuja kupata.

Mama Samia alionekana ni mtu atakaye kuja kufanya mageuzi makubwa lakini nasikitika hakuna kitu chochote mpaka sasa ambacho amefanya.

Kwanza alitoa ahadi ya ukaguzi maalumu BOT ambapo pesa zilichotwa kinyemela mpaka sasa kimya.

Aliagiza kufunguliwa kwa vyombo vyote vya habari mpaka sasa kimya.

Ameleta tume ya walimu wameikataa na yeye kakubali.

Unamtoa mwizi hazina unampeleka viwanda na biashara kwa kuogopa nini?

Haya mambo 4 yanaonyesha kama taifa hatuna kiongozi mwenye msimamo.

Kutokana na picha hii naomba kutoa ushauri kwa mambo yafuatayo

1: Mama aombe msamaha taifa Kwa uharibifu ambao Magufuli aliufanya then.

2: Ahachane na baadhi ya elephant project kama ununzi wa ndege kwa cash uku mishahara ikikushinda kuongeza.

3: Rais aanzishe haraka mchakato wa katiba mpya lasivyo atakwama pakubwa.

4: Rais aongelee swala la Bandari ya bagamoyo ambayo inaonekana ni mradi wa kifisadi kama inawezekana initial contract iwekwe wazi ili Watanzania tuone yaliyomo.

5: Janga la covid19 nalo umepiga kimya mi nasema atakaye ichezea corona itaondoka na yeye.

Nimesikitishwa na Hotuba ya Rais leo kuongelea swala la wafanyakazi wa umma na kuacha wafanyakazi wa sector binafisi ambao ndio wengi zaidi mfano wafanyakazi wa sector binafsi.

Wamekuwa hawaunganishwi na mfuko wa taifa ya bima ya afya kwa lazima.

Wamekuwa hawaunganiswi na mfumo wa pension kwa lazima hivyo waajiri wanakiuka sheria za kazi.

Wamekuwa wanafanya kazi muda mrefu kwa malipo yaleyale yaani mtu analipwa laki 3 kwa mwezi halafu anafanya kazi kwa masaa 12 mpaka 18 kwa siku.

Tena kwa masikitiko malimbikizo ya mishahara yanakuwa makubwa mtu unakuta anadai kwa miezi 2 au 3 nyuma na kwa kulinganisha maisha ya sasa yalivyo magumu je tunawatetea.

Mikataba ya wafanyakazi wa sector binafsi imekuwa haipo wanaopewa ni chini ya 5% ya watu wote wanaofanya kazi sector binafsi hii inafanya watu wafukuzwe hovyo bila kupewa stahiki zao

Wakati yote haya yanafanyika Nchi ina Rais , Makamu, Mawaziri,Wabunge,Wakuu wa mikoa,Wakuu wa wilaya, wakurugenzi, Idara ya usalama wa taifa, polisi, Takukuru, Tume za wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi.

Nchi sasa inaonekana kama mtu anaongozewa na amewekwa Kama rubber stamp.

Usumbufu kwa wachimbaji wadogo umerudi kwa haraka sana why?

Vituo vya Mafuta baadhi hawatumii EFD tena why?

Ongezeko la madawa ya kulevya kwanini yameongezeka kwa haraka why?

Tunaongelea siku 50 tu za utawala wako mambo yamebadilika hivi je ndani ya miaka 5 hali itakuwaje?

Bila kifanya mageuzi makubwa ya kikatiba na kimfumo hakuna pahali mama samia ataenda.

Inawezekana anafanya either kwa kutokuwa na taarifa au anafanya makusudi.

Nchii hii kwanza mkubali ni yetu sote then tukiri tulikosea hapo nyuma kama nchi then hatujachelewa tuanze upya tusimike mifumo imara other wise kila rais atakuja na kuondoka maendeleo ya kweli hakuna.

Jiulize gharama za pesa zilizotumika leo kuwapeleka mwanza Rais, Makamo, waziri mkuu, Mawaziri wote, Wakuu wa mikoa kwenda kupiga polojo halafu kwenda kushusha kodi kutoka 9% kwenda 8%.

Mama samia akiendelea kukumbatia watu waovu ndani ya ccm atakwama pakubwa sana

Tunataka report ya CAG ya ukaguzi maalumu pale BOT.

Ukishindwa utakuwa Rais dhaifu zaidi kuwai kuongoza taifa hili mambo bado usilale.

Achana na kuikumbatia CCM Fanya kazi zenye Maslahi mapana kwa Watanzania.

Katika dharura nyingi:

1. Audit report BOT.
2. Covid 19.
3. Kusafisha genge la wale jamaa bila kumwacha mtu.

Haya yalikuwa ya dharura zaidi.

Mama na auvae ujasiri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom