Rais Samia achana na kuikumbatia CCM, fanya kazi zenye Maslahi mapana kwa Watanzania

Kipindi flani hapa Watu wamenyanyaswa sana mateso na makesi kibao ya ajabu ajabu.Leo hii mnaanza kumsema mama ambae hana hata miezi 5 ofisini.Muacheni.
 
Pamoja na udhaifu wote aliyonayo bora huyu kuliko yule MwenyeKwenda zake,Yeye na matendo yake mwache aende tu.
Kwa mfano ukiulizwa JPM alikufanyia nini kibaya utatoa jawabu gani...

Tusipende kutoa lawama kwa kusikia fulani kafanyiwa hivi au vile kwani ni vigumu kuelewa ukweli halisi wa jambo ikiwa halijakutokea wewe. Aidha unapaswa kukumbuka kuwa uongo husambaa kwa kasi sana ikilinganishwa na ukweli.

Sipo hapa kumtetea mtu yeyote, ninachojaribu kufanya ni kuwataka watz tusiwe wepesi wa kutoa lawama au sifa kwa mtu ikiwa hujajitafutia usahihi wa jambo alilolifanya. Kiongozi mmoja aliwahi kusema "usirithi adui, tengeneza wa kwako", nadhani hakukosea.....

Wahenga waliwahi sana " Amani haiji ila kwa ncha ya upanga"... Ukifuatilia historia ya nchi zote zilizoendelea utagundua kwamba bila kufunga mkanda na kukaza kiatu sawasawa, maendeleo utayasikia kwao wayafanyayo hayo na si kwako.

Inapaswa kama taifa tujiulize tunahitaji nini, kisha tupange nini tufanye ili kukipata au kukifikia tunachokihitaji. Ili kufikia lengo unalolihitaji ni vizuri kupanga kutoka mwisho kuja mwanzo kwani kwa kufanya hivyo kutakuwezesha kujua matokeo ya kila hatua utakayokuwa unapiga na kama matokeo ni hasi, ni rahisi kujisahihisha mapema.

Kitu kingine ningeshauri tusiwe wepesi wa kusahau au kuweka matumaini yetu yote kwa viongozi kwani wao pia ni wanadamu kama tulivyo sisi. Ikumbukwe kabla ya uchaguzi mwa 2015 sisi watu tulikuwa msitari wa mbele kubeza na kulaumu uongozi uliokuwepo madarakani, na kupitia wawakilishi wetu tuliweza kusema kila aina ya maneno nisingependa kuyarudia hapa maana nadhani sote twayafahamu. Na katika kusahihisha makosa, tulitoa mawazo kupitia wawakilishi wetu kwamba nchi yetu inahitaji Rais mkali mwenye kuongoza kwa mkono wa chuma ili kuikomboa nchi yetu.

Jambo hilo ndilo lililowalazimu CCM kumpitisha Magufuli kugombea na niwaambie tu kuwa halikuwa jambo jepesi hata ndani ya chama chenyewe. Sote twajua nini kilitokea wakati wa mchakato wa kumpata mgombea huyo. Ni kwamba hata ndani ya chama hawakuwa wanamhitaji ila kulingana na hali ilivyokuwa kwa wakati huo, hawakuwa na namna yoyote ya kufanya isipokuwa kumweka yeye ili chama kiweze kushinda. Chaguo lolote tofauti na yeye lingelikuwa ni msumari wa mwisho kwenye jeneza la CCM katika siasa za Tanzania kwani hakukuwa na mgombea yeyote mwingine ambaye angeliweza kusimama mbele ya Chadema ya Dr. Slaa.

Mambo muhimu ya kukumbuka ni kwamba... serikali haiwezi ikaleta kila jambo, serikali haiwezi ikaajiri wahitimu wote, nchi haiwezi kuendelea ikiwa hatuwapimi wawakilishi wetu na kuchukua hatua, hatuwezi tukaendelea kwa kutegemea misaada, si kila jambo lifanywalo au lianzishwalo na wenye ngozi nyeupe latufaa kwa matumizi yetu (ikumbukwe hawataki tupige hatua kutoka hapa tulipo, tafuta vielelezo thabiti utaviapata) na mwisho japo si kwa umuhimu, "tuwe na moyo wa kushukuru".

Jpili njema!
 
Naomba namba yako ya voda nikutumie hela ya soda au kama uko karibu na kwa mangi nenda hapo mwambie akupe pepsi baridi sana ntakuja kulipa
 
Kwani jiwe alifanyaje kama sio majanga tu Nchi hii bila cccm kuondolewa zitakuwa Stori tupu

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
CCM haiwezi kuondolewa madarakani sahau hiyo kitu.

Ina watanzania waligeuzwa mandondocha kitambo tu.

Hawashangai, hawahoji wala kushtuka.

Upinzani nao ni CCM B
 
Kwa mfano ukiulizwa JPM alikufanyia nini kibaya utatoa jawabu gani..
Kuna watu walipotea,kupigwa risasi,kuuwawa yeye kama Amiri Jeshi Mkuu;Mkuu wa vikoasi vya ulinzi na usalama hakuchukua hatua yeyote,hadi anaelekea Jongomeo.
Aliminya stahiki za wafanyakazi kipindi chote cha utawala wake.
Maisha ya Watanzania yamekuwa magumu sana toka kipindi cha Mwalimu Nyerere hii hali ilishuhudiwa sababu tu ya kufanya miradi ambayo hatuna uhakika wa return,huenda ni ''White Elephant''.
Ukabila na ukanda umezidi sana kipindi cha huyu mwamba.Ni kipindi ambacho Watanzania wamegawika naweza sema toka uhuru hatujawahi shuhudia hii hali.
Kuwa na roho ya visasi kwa wale wanaomkosoa hata kama ni kwa nia njema.
Hayo ni kwa uchache tu....
 
1. Tunataka katiba mpya nzuri

2. Tunataka mabadilio ya sheria mbovu siyo maagizo ya rais tu, maagizo ni easily reversible

3. Tunataka Ukandamizaji wa kuwa na online Channel youtube uondolewe, kwa nini niilipe serikali hela kwa mimi kuwa na Channel yangu youtube?

4. Tunataka uhuru wa vyombo vya habari
Upuuzi mtupu! Utakula online TV?
Tunahitaji "Maendeleo" uchumi ukue ufike juu tuondokane na umasikini! Sio hizo TAKATAKA zako!

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Tunahitaji miradi yote ya kimkakati SGR,Mradi wa umeme,daraja la busisi n.k yakamilike na miradi mipya iletwe.Shirika la ndege lisife elimu iendelee kuwa bure! Vituo vya afya,Shule na madarasa viendelee kujengwa.HAYO TU!

Hivyo unavyovisema ameshaahidi kuvifanyia kazi hatuna shaka navyo, tunazungumzia ambavyo mpaka sasa amemute!
 
Hakika mimi uwa nasema ukweli bila sisi kama nchi kuacha kuishi ya Uongo uongo hakuna maendelea ambayo tutakuja kupata.

Mama Samia alionekana ni mtu atakaye kuja kufanya mageuzi makubwa lakini nasikitika hakuna kitu chochote mpaka sasa ambacho amefanya.

Kwanza alitoa ahadi ya ukaguzi maalumu BOT ambapo pesa zilichotwa kinyemela mpaka sasa kimya.

Aliagiza kufunguliwa kwa vyombo vyote vya habari mpaka sasa kimya.

Ameleta tume ya walimu wameikataa na yeye kakubali.

Unamtoa mwizi hazina unampeleka viwanda na biashara kwa kuogopa nini?

Haya mambo 4 yanaonyesha kama taifa hatuna kiongozi mwenye msimamo.

Kutokana na picha hii naomba kutoa ushauri kwa mambo yafuatayo

1: Mama aombe msamaha taifa Kwa uharibifu ambao Magufuli aliufanya then.

2: Ahachane na baadhi ya elephant project kama ununzi wa ndege kwa cash uku mishahara ikikushinda kuongeza.

3: Rais aanzishe haraka mchakato wa katiba mpya lasivyo atakwama pakubwa.

4: Rais aongelee swala la Bandari ya bagamoyo ambayo inaonekana ni mradi wa kifisadi kama inawezekana initial contract iwekwe wazi ili Watanzania tuone yaliyomo.

5: Janga la covid19 nalo umepiga kimya mi nasema atakaye ichezea corona itaondoka na yeye.

Nimesikitishwa na Hotuba ya Rais leo kuongelea swala la wafanyakazi wa umma na kuacha wafanyakazi wa sector binafisi ambao ndio wengi zaidi mfano wafanyakazi wa sector binafsi.

Wamekuwa hawaunganishwi na mfuko wa taifa ya bima ya afya kwa lazima.

Wamekuwa hawaunganiswi na mfumo wa pension kwa lazima hivyo waajiri wanakiuka sheria za kazi.

Wamekuwa wanafanya kazi muda mrefu kwa malipo yaleyale yaani mtu analipwa laki 3 kwa mwezi halafu anafanya kazi kwa masaa 12 mpaka 18 kwa siku.

Tena kwa masikitiko malimbikizo ya mishahara yanakuwa makubwa mtu unakuta anadai kwa miezi 2 au 3 nyuma na kwa kulinganisha maisha ya sasa yalivyo magumu je tunawatetea.

Mikataba ya wafanyakazi wa sector binafsi imekuwa haipo wanaopewa ni chini ya 5% ya watu wote wanaofanya kazi sector binafsi hii inafanya watu wafukuzwe hovyo bila kupewa stahiki zao

Wakati yote haya yanafanyika Nchi ina Rais , Makamu, Mawaziri,Wabunge,Wakuu wa mikoa,Wakuu wa wilaya, wakurugenzi, Idara ya usalama wa taifa, polisi, Takukuru, Tume za wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi.

Nchi sasa inaonekana kama mtu anaongozewa na amewekwa Kama rubber stamp.

Usumbufu kwa wachimbaji wadogo umerudi kwa haraka sana why?

Vituo vya Mafuta baadhi hawatumii EFD tena why?

Ongezeko la madawa ya kulevya kwanini yameongezeka kwa haraka why?

Tunaongelea siku 50 tu za utawala wako mambo yamebadilika hivi je ndani ya miaka 5 hali itakuwaje?

Bila kifanya mageuzi makubwa ya kikatiba na kimfumo hakuna pahali mama samia ataenda.

Inawezekana anafanya either kwa kutokuwa na taarifa au anafanya makusudi.

Nchii hii kwanza mkubali ni yetu sote then tukiri tulikosea hapo nyuma kama nchi then hatujachelewa tuanze upya tusimike mifumo imara other wise kila rais atakuja na kuondoka maendeleo ya kweli hakuna.

Jiulize gharama za pesa zilizotumika leo kuwapeleka mwanza Rais, Makamo, waziri mkuu, Mawaziri wote, Wakuu wa mikoa kwenda kupiga polojo halafu kwenda kushusha kodi kutoka 9% kwenda 8%.

Mama samia akiendelea kukumbatia watu waovu ndani ya ccm atakwama pakubwa sana

Tunataka report ya CAG ya ukaguzi maalumu pale BOT.

Ukishindwa utakuwa Rais dhaifu zaidi kuwai kuongoza taifa hili mambo bado usilale.

Achana na kuikumbatia ccm Fanya kazi zenye Maslahi mapana kwa Watanzania.
Story ndeeeefuuu ila ni upuuzi tu na makorokocho ndani yake
 
Wengi wao hao ni wale MATAGA FC!!yaani siku 50, tu ndio ushushe lawama zote hizo?, si bora hata huyu anakubali madhaifu, na kuwa tayari kuyarekebisha??yule aliyekuwa kila kitu anajua yeye miaka 5 amefanya nini?kubwa?hata leo hajaongeza mishahara lakini watu amewapa matumaini, sasa meko, unaulizia haki yako, UNATISHIWA??
Unauliza amefanya nini wewe una akili kweli? Au huna macho? Ndege huzioni,Madaraja,SGR,Nyerere project,Terminal 3,Stendi ya Mbezi,Viwanda,Barabara,madarasa,Elimu bure,Kukomesha rushwa, nidhamu kazini.... na mengineyo mengi kwamba huyaoni au jeuri tu??

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Mimi naamini katika swala la muda. Ndio kwanza ana mwezi mmoja tu. Najua watanzania tuliumizwa sana kwa kipindi cha miaka mitano. Lakini je huyu rais ana nguvu kiasi gani kubadilisha maovu ya mtangulizi wake ya miaka mitano ndani ya mwezi mmoja? Tuwe wakweli.
Usiseme watanzania sema wewe uliumizwa!

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Shujaa John Pombe Joseph Magufuli atabaki kuwa rais wa karne, mwamba, jasiri, mbeba maono na mtekelezaji...

Tusimlinganishe Rais Samia Suluhu Hassan na JPM. Sisi tuangalie utekelezwaji miradi na ilani ya kurasa 303

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais wetu Samia Suluhu Hassan

Kazi iendelee
Kweli kabisa.Huu ni ukweli mchungu!

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom