Rais Samia achana na kuikumbatia CCM, fanya kazi zenye Maslahi mapana kwa Watanzania

Watanzania bwana!!!
Wabunge bungeni hawajui wanachoDEMKIA Ndugaye akisema ndiyo nao Ndiyoooooo! akisema hapana nao hapanaaaa!!!! Haijulikani wanacho shangilia
Sasa ugonjwa umeamia kwa Wananchi

NANI KATUROGA!!!!!!!!!!
TUMTAFUTE KWANZA MCHAWI WETU KWANZA
NA SISI TUMROGE
 
Mleta uzi huna lolote, ndio nyie mkipewa nafasi hata wiki humalizi unashindwa kuongoza.
Unadhani u rais ni kazi ndogo kiasi cha wewe kumkosoa Rais?
Tafuta kazi ya kufanya utunze familia yako .
Kazi yake ndio hiyo!!!
 
Kwani jiwe alifanyaje kama sio majanga tu Nchi hii bila cccm kuondolewa zitakuwa Stori tupu

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
CCM iondolewe halafu apewe nani nchi? Tuwape wezi wabinafsishe nchi iwe ya familia zao?

Mkiambiwa watu waliupenda wizi wa Magufuli mlikuwa mnang’aka sasa subirieni ufisadi wa kutisha ambao utatangazwa wazi wazi mnamo 2025 ikiwa hamna maendeleo yoyote yaliofanyika na kuonekana na tija zaidi ya porojo tu halafu mtamtafuta mchawi!

Tunarudi kwenye Era ambayo wanasiasa watajitajirisha wao na familia zao bila mipaka na kuwasahau kabisa wapiga kura wao bila aibu!
 
😆 😆 Watu walisema JK dhaifu, akaja mwendazake dikteta, sasa mama Rais ndani ya miezi miwili naye dhaifu.
Taifa liliharibiwa sana na maneno kama Big Results Now.

Everyday is Saturday................................:cool:
Kwa dalili tu huyu wa sasa ndio atakuwa worst kuliko yule wa Ari Mpya...Kasi Mpya! Lets leave it to the hands of time.

2025 shida zitakuwa pale pale ila kuna kundi dogo tu la wenye nazo ndio litakuwa likitamba na kutanua mjini! Social services zitarudi kuwa so poor.
 
Wewe jamaa sikujua kama ni mpumbavu kiasi hiki.

Nakushauri tu, ongea na Maxence Melo awaombe mods wake huu uzi ufutwe. Huu uzi utakuchafua na kila atakae usoma atakuona wewe huna akili.

Ukute hapo una vyeti vyako vya utalii college halafu unaanza kumpangia Mheshimiwa rais. Eti hujaona mama alichokifanya mpaka sasa

Hivi nyie mijitu mengine mnajua hata kuishi tu duniani ni hasara?? Leave alone you being a Tanzanian. Yaani wewe hufai hata senti moja.
 
Hakuna wa kumfananisha mwamba, jiwe, JPM hata siku moja. Ngoja tuanze kula urojo huku chamwino ndio tutafurahi.

2025 tathmini itafanyika na ndio tutajua mwamba alikuwa jiwe kweli kweli.
Hahahahah majibu yatakuwa kama hivi:
Ufisadi vs Huduma bora. 5-0
Rushwa vs Haki. 7-1
Uwazi vs Kuminywa. 2-1

Hapo ndipo atakapokumbukwa yule ambaye anadhihakiwa na kukiri kuwa jamaa ndiye aliiweza nchi!
 
Mleta uzi huna lolote, ndio nyie mkipewa nafasi hata wiki humalizi unashindwa kuongoza.
Unadhani u rais ni kazi ndogo kiasi cha wewe kumkosoa Rais?
Tafuta kazi ya kufanya utunze familia yako .
Yaani hapo alipo ukute hata kazi maalum ya kufanya hana.

Tunaendelea kusisitiza kwamba Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu
 
Ndiyo maana kuiongoza nchi hii lazima uwe mbogo, ukisikiliza kila mmoja hautafika, Magu style ndiyo inatakiwa. Mwanadamu huwa hana shukrani, wewe fanya the Right thing period
Ndio namna pekee maana kila mtu anaongea utumbo kelele left & right ndo maana mzee akaamua azizime redio mbao zote sauti inayosikika iwe kutoka ikulu tu!
 
Hakika mimi uwa nasema ukweli bila sisi kama nchi kuacha kuishi ya Uongo uongo hakuna maendelea ambayo tutakuja kupata.

Mama Samia alionekana ni mtu atakaye kuja kufanya mageuzi makubwa lakini nasikitika hakuna kitu chochote mpaka sasa ambacho amefanya.

Kwanza alitoa ahadi ya ukaguzi maalumu BOT ambapo pesa zilichotwa kinyemela mpaka sasa kimya.

Aliagiza kufunguliwa kwa vyombo vyote vya habari mpaka sasa kimya.

Ameleta tume ya walimu wameikataa na yeye kakubali.

Unamtoa mwizi hazina unampeleka viwanda na biashara kwa kuogopa nini?

Haya mambo 4 yanaonyesha kama taifa hatuna kiongozi mwenye msimamo.

Kutokana na picha hii naomba kutoa ushauri kwa mambo yafuatayo

1: Mama aombe msamaha taifa Kwa uharibifu ambao Magufuli aliufanya then.

2: Ahachane na baadhi ya elephant project kama ununzi wa ndege kwa cash uku mishahara ikikushinda kuongeza.

3: Rais aanzishe haraka mchakato wa katiba mpya lasivyo atakwama pakubwa.

4: Rais aongelee swala la Bandari ya bagamoyo ambayo inaonekana ni mradi wa kifisadi kama inawezekana initial contract iwekwe wazi ili Watanzania tuone yaliyomo.

5: Janga la covid19 nalo umepiga kimya mi nasema atakaye ichezea corona itaondoka na yeye.

Nimesikitishwa na Hotuba ya Rais leo kuongelea swala la wafanyakazi wa umma na kuacha wafanyakazi wa sector binafisi ambao ndio wengi zaidi mfano wafanyakazi wa sector binafsi

Wamekuwa hawaunganishwi na mfuko wa taifa ya bima ya afya kwa lazima.

Wamekuwa hawaunganiswi na mfumo wa pension kwa lazima hivyo waajiri wanakiuka sheria za kazi.

Wamekuwa wanafanya kazi muda mrefu kwa malipo yaleyale yaani mtu analipwa laki 3 kwa mwezi halafu anafanya kazi kwa masaa 12 mpaka 18 kwa siku

Tena kwa masikitiko malimbikizo ya mishahara yanakuwa makubwa mtu unakuta anadai kwa miezi 2 au 3 nyuma na kwa kulinganisha maisha ya sasa yalivyo magumu je tunawatetea.

Mikataba ya wafanyakazi wa sector binafsi imekuwa haipo wanaopewa ni chini ya 5% ya watu wote wanaofanya kazi sector binafsi hii inafanya watu wafukuzwe hovyo bila kupewa stahiki zao

Wakati yote haya yanafanyika Nchi ina Rais , Makamu, Mawaziri,Wabunge,Wakuu wa mikoa,Wakuu wa wilaya, wakurugenzi, Idara ya usalama wa taifa, polisi, Takukuru, Tume za wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi.

Nchi sasa inaonekana kama mtu anaongozewa na amewekwa Kama rubber stamp.

Usumbufu kwa wachimbaji wadogo umerudi kwa haraka sana why?

Vituo vya Mafuta baadhi hawatumii EFD tena why?

Ongezeko la madawa ya kulevya kwanini yameongezeka kwa haraka why?

Tunaongelea siku 50 tu za utawala wako mambo yamebadilika hivi je ndani ya miaka 5 hali itakuwaje?

Bila kifanya mageuzi makubwa ya kikatiba na kimfumo hakuna pahali mama samia ataenda.

Inawezekana anafanya either kwa kutokuwa na taarifa au anafanya makusudi.

Nchii hii kwanza mkubali ni yetu sote then tukiri tulikosea hapo nyuma kama nchi then hatujachelewa tuanze upya tusimike mifumo imara other wise kila rais atakuja na kuondoka maendeleo ya kweli hakuna.

Jiulize gharama za pesa zilizotumika leo kuwapeleka mwanza Rais, Makamo, waziri mkuu, Mawaziri wote, Wakuu wa mikoa kwenda kupiga polojo halafu kwenda kushusha kodi kutoka 9% kwenda 8%.

Mama samia akiendelea kukumbatia watu waovu ndani ya ccm atakwama pakubwa sana

Tunataka report ya CAG ya ukaguzi maalumu pale BOT.

Ukishindwa utakuwa Rais dhaifu zaidi kuwai kuongoza taifa hili mambo bado usilale.

Achana na kuikumbatia ccm Fanya kazi zenye Maslahi mapana kwa Watanzania.
Haya ni matusi kwa rais.
 
Hata mimi nimeona huyu mama hamna kitu kabisa, yaani hii nchi itaharibika mikononi mwake.
Isitoshe hana confidence ya kuwa kiongozi imara, mfano, kila mara utamsikia akirudia rudia kusema mimi ni Rais, mimi ni Rais,.. Kauli hii ameirudia zaidi ya mara tatu tokea aapishwe kama Rais.
Sisi "wanasaikolojia" tunasema kwamba ukimsikia mtu anajitangaza kuwa yeye ndiye "Bossi" mbele ya wale anaowaongoza basi fahamu kwamba mtu huyo hatoshi kwenye nafasi ya Ubossi.

Kiongozi mzuri huwa hajitangazi mara mbili mbili kuwa yeye ni kiongozi, bali kazi zake, vitendo vyake na maono yake ya humtangaza.
Rais wa kwanza mwanamke na ukumbuke kuwa Hayati JPM alikuwa na uwezo wa kumchukua Mwinyi kama mgombea mwenza mwaka 2015.

Presha aliyonayo huyu Mama ni kubwa kutoka humo humo CCM hivyo kauli zake za kuitetea jinsia yake zina msingi wake.
 
Hakika mimi uwa nasema ukweli bila sisi kama nchi kuacha kuishi ya Uongo uongo hakuna maendelea ambayo tutakuja kupata.

Mama Samia alionekana ni mtu atakaye kuja kufanya mageuzi makubwa lakini nasikitika hakuna kitu chochote mpaka sasa ambacho amefanya.

Kwanza alitoa ahadi ya ukaguzi maalumu BOT ambapo pesa zilichotwa kinyemela mpaka sasa kimya.

Aliagiza kufunguliwa kwa vyombo vyote vya habari mpaka sasa kimya.

Ameleta tume ya walimu wameikataa na yeye kakubali.

Unamtoa mwizi hazina unampeleka viwanda na biashara kwa kuogopa nini?

Haya mambo 4 yanaonyesha kama taifa hatuna kiongozi mwenye msimamo.

Kutokana na picha hii naomba kutoa ushauri kwa mambo yafuatayo

1: Mama aombe msamaha taifa Kwa uharibifu ambao Magufuli aliufanya then.

2: Ahachane na baadhi ya elephant project kama ununzi wa ndege kwa cash uku mishahara ikikushinda kuongeza.

3: Rais aanzishe haraka mchakato wa katiba mpya lasivyo atakwama pakubwa.

4: Rais aongelee swala la Bandari ya bagamoyo ambayo inaonekana ni mradi wa kifisadi kama inawezekana initial contract iwekwe wazi ili Watanzania tuone yaliyomo.

5: Janga la covid19 nalo umepiga kimya mi nasema atakaye ichezea corona itaondoka na yeye.

Nimesikitishwa na Hotuba ya Rais leo kuongelea swala la wafanyakazi wa umma na kuacha wafanyakazi wa sector binafisi ambao ndio wengi zaidi mfano wafanyakazi wa sector binafsi

Wamekuwa hawaunganishwi na mfuko wa taifa ya bima ya afya kwa lazima.

Wamekuwa hawaunganiswi na mfumo wa pension kwa lazima hivyo waajiri wanakiuka sheria za kazi.

Wamekuwa wanafanya kazi muda mrefu kwa malipo yaleyale yaani mtu analipwa laki 3 kwa mwezi halafu anafanya kazi kwa masaa 12 mpaka 18 kwa siku

Tena kwa masikitiko malimbikizo ya mishahara yanakuwa makubwa mtu unakuta anadai kwa miezi 2 au 3 nyuma na kwa kulinganisha maisha ya sasa yalivyo magumu je tunawatetea.

Mikataba ya wafanyakazi wa sector binafsi imekuwa haipo wanaopewa ni chini ya 5% ya watu wote wanaofanya kazi sector binafsi hii inafanya watu wafukuzwe hovyo bila kupewa stahiki zao

Wakati yote haya yanafanyika Nchi ina Rais , Makamu, Mawaziri,Wabunge,Wakuu wa mikoa,Wakuu wa wilaya, wakurugenzi, Idara ya usalama wa taifa, polisi, Takukuru, Tume za wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi.

Nchi sasa inaonekana kama mtu anaongozewa na amewekwa Kama rubber stamp.

Usumbufu kwa wachimbaji wadogo umerudi kwa haraka sana why?

Vituo vya Mafuta baadhi hawatumii EFD tena why?

Ongezeko la madawa ya kulevya kwanini yameongezeka kwa haraka why?

Tunaongelea siku 50 tu za utawala wako mambo yamebadilika hivi je ndani ya miaka 5 hali itakuwaje?

Bila kifanya mageuzi makubwa ya kikatiba na kimfumo hakuna pahali mama samia ataenda.

Inawezekana anafanya either kwa kutokuwa na taarifa au anafanya makusudi.

Nchii hii kwanza mkubali ni yetu sote then tukiri tulikosea hapo nyuma kama nchi then hatujachelewa tuanze upya tusimike mifumo imara other wise kila rais atakuja na kuondoka maendeleo ya kweli hakuna.

Jiulize gharama za pesa zilizotumika leo kuwapeleka mwanza Rais, Makamo, waziri mkuu, Mawaziri wote, Wakuu wa mikoa kwenda kupiga polojo halafu kwenda kushusha kodi kutoka 9% kwenda 8%.

Mama samia akiendelea kukumbatia watu waovu ndani ya ccm atakwama pakubwa sana

Tunataka report ya CAG ya ukaguzi maalumu pale BOT.

Ukishindwa utakuwa Rais dhaifu zaidi kuwai kuongoza taifa hili mambo bado usilale.

Achana na kuikumbatia ccm Fanya kazi zenye Maslahi mapana kwa Watanzania.
una mpangia Rais cha kufanya hahahaaa akili finyu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom