Rais Samia aanza kurekodi kipindi cha kutangaza utalii

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Rais Samia Suluhu Hassan amenza kurekodi kipindi maarufu cha ‘Royal Tour’ chenye lengo la kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia vivutio vya utalii.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 29, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Jaffar Haniu imesema, Rais Samia atatembelea na kuonesha kwa wageni hao vivutio mbalimbali vya utalii, uwekezaji, sanaa na utamaduni vilivyopo nchini.

Taarifa hiyo inayomnukuu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utramaduni, Wasanii na Michezo, Dk Hassan Abbas, imesema Rais Samia na wageni wa Royal Tour wameanza kazi ya kurekodi maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii na uwekezaji Agosti 28/2021 katika maeneo ya visiwa vya Zanzibar.
 
Back
Top Bottom