Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,784
- 12,226
Eneo la kwanza ni kuheshimu katiba na sheria, hili ni eneo ambalo kama nchi tunataka kudumisha upendo na amani ni la kuzingatia kwa nguvu zote. Samia ameapa kulinda katiba asipofanya hivyo ni uhaini na lazima atakuja kuchukuliwa hatua bila kujali kinga za Urais. Mila na utamaduni wa Taifa lo lote hudumisha na kuimarishwa na katiba yake.
Eneo la pili na uhuru na haki ya wananchi wote bila kujali cheo cha mtu au nafasi yake katika jamii. Hivi sasa kuna watu wanajiona wana haki zaidi ya wengine na hivyo kufanya vitendo vya uonevu na dhuluma dhidi ya wengine. Kuna watu wanasota magerezani bila kuhukumiwa na wengine wamehukumiwa kwa uonezi na husda. Hii si sawa kabisa, Rais Samia anapaswa kuchukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na kuunda tume huru ya kijaji kuchunguza haki za wote waliopo mahabusu na gerezani.
Eneo la tatu ni kusikilizwa kwa maoni na vilio vya wananchi bila kujali itikadi zao za kisiasa. Pamoja na kuwa na katiba na sheria zilizopo lakini watu wengi wamekuwa wakiathirika na baadhi ya vifungu vya sheria hizo kwa sababu ni za uonevu na zimetungwa kulinda maslahi ya baadhi ya watu.
Aidha kuna sheria zimetungwa kudhibiti baadhi ya watu na vyama vya siasa bila kuzingatia haki zao za msingi za kikatiba. Kwa hiyo kilio cha kupata katiba mpya ambayo itaendana na wakati wa sasa ni muhimu kusikilizwa na pia kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi ambayo itatoa haki sawa kwa kila mtu na vyama vyote vya siasa.