Rais Samia aambiwe ukweli hawezi kumfurahisha kila mtu nchini

mwananyaso

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
2,843
3,128
Nafahamu Rais Samia ni mpenzi sana wa mitandao ya kijamii, imani yangu anasoma kinachoandikwa na baadhi ya watanzania wenzetu nikiwemo na mimi mwenyewe tukiwa na mitazamo tofauti.

Kati yetu ,wapo ambao hushauri,huelekeza,hulaumu,husifia na wengine huponda pia.

Hali hii ilitokea hata kipindi cha mtangulizi wake hayati Magufuli,na hii ni hurka ya binadamu yoyote yule,lakini alisimama imara sana,hakutoka mchezoni .

Kwa kuzingatia nafasi ya kimamlaka aliyonayo Rais Samia ategemee yote niliyoyataja hapo juu.
Ushauri wangu kwake ni kuhakikisha anaisimamia nchi barabara kama mkuu wa nchi kwenye angles zote bila kujali atamkwaza nani .

Watanzania wanahitaji hali bora ya maisha ,huduma za kiafya zikiboreshwa ,ulinzi wa mali zao,elimu bora,huduma za miundo mbinu zikiimarishwa,bei affordable ya manunuzi kwa bidhaa na mengineyo mengi yenye tija kwa jamii.hapo ndipo pazito haswa

Nimalizie kwa kusema kazi yake itapimwa baada au kabla ya muhula wake kuisha ,hasa utekelezaji wa ilani ya chama chake, na wengi wetu kipimo chake ni namna atakavyovunja rekodi ya mtangulizi wake hayati Magufuli.
 
Back
Top Bottom