Rais Samia aambiwe Makamu wa Rais ni Mkubwa kwa Rais wa Zanzibar, au anafanya makusudi!?

Lakasa chika7

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
454
1,263
Nimesikiliza hotuba zake nyingi sana! Kubwa ile ya bungeni juzi.

Mama nadhani kwa makusudi anataka kulazimisha Rais wa Zanzibar ni mkubwa kiutawala kwa Makamu wa Rais.

Kwenye hotuba zake nyingi.

Anaanza kumuaddress Rais Zanzibar kabla ya Makamu wa Rais wa Tanzania. Hii siyo sawa hata kidogo. Huwezi kutambua uwepo wa Rais wa Zanzibar kabla ya Makamu wa Rais wa Tanzania. Ni dharau na fedhea kwa Muungano.

Rais wa Zanzibar ni mjumbe tu Baraza la Mawaziri hana nguvu yeyote.

Leo unataka pesa za Sherehe za Muungano ziende kwa usawa Zanzibar na Tanganyika.
Hivi hizo pesa zimetoka Bara leo ziende Zanzibar.
Zanzibar yenye watu million 1 ipate sawa na Tanganyika yenye watu million 60.

Watanganyika tuwe makini na mwendo wa Mama.
Yupo kwa ajili ya Zanzibar zaidi kuliko Tanzania.
Sisi Tanganyika hatuna agenda ya pamoja tupo tu hatujui tunataka nini.
Leo mimi mbara siruhusiwi kwenda Zanzibar kununua kiwanja wala kufanya kazi kwenye serikali yao.
Wazanzibar kibao wapo serikalini kwenye ofisi hata zisizo za Muungano na free wao kununua ardhi.

Watanganyika mmelala ngojeni mambo ndio yanaanza.

Kiprotoko hutakiwi kutambua uwepo wa Rais wa Zanzibar kabla ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Tanganyika hatuna agenda kila siku Zanzibar wanalalamika kuhusu mambo kadhaa kwenye Muungano Bara kimya.

Mimi nilitaka kununua kiwanja Zanzibar nikaambiwa nioneshe kitambulisho cha Zanzibar mkazi.
Mama ana asili ya wapemba alizaliwa huko baba ake alihamia Unguja.

Watanganyika tupo na akili chache sana.. Agenda zetu wabunge wa covid 19..utopolo tu

Tunadhani Mwinyi ni mwenzetu.. Mwinyi siyo mwenzetu.

Mama umekua Rais kwa muujibu wa katiba bila katiba usingepata Urais wa dezo Tafadhali heshimu katiba.

Rais wa Zanzibar kiprotoko ni mdogo kuliko hata Waziri Mkuu.

Siku ya mashindano ya kusoma Quran eti Rais wa Zanzibar anaondoka uwanjani kabla ya Waziri Mkuu. Ndani ya eneo la Tanganyika Rais wa Zanzibar hana nguvu ni km mm tu.

Mama acha uzanzibar tunajua nyie wapemba wabaguzi sana.

Kipindi flani walikuzushia unataka Rais unataka kugombea Urais Zanzibar ulikataa ukasema Urais Zanzibar ni mdogo kuliko cheo chako cha Makamu Rais naona leo umesahau..! Maliza miaka 4 iloyobaki tuachie Nchi yetu.

Its Zanzibar time BARA IMELALA FOFO... LINI MBUNGE WA BARA ALIWAHI KUHOJI WHY WABARA HAWARUHUSIWI KUNUNUA ARDHI ZANZIBAR.

Tumepigwa Bara huyu Mama Mzanzbar zaidi kuhusu mtanzania.

Akiwa na Safari za nje ataenda yeye asipoenda ataenda Mwinyi.
 
Nimesikiliza hotuba zake nyingi sana! Kubwa ile ya bungeni juzi.
Mama nadhani kwa makusudi anataka kulazimisha Rais wa Zanzibar ni mkubwa kiutawala kwa Makamu wa Rais.
Kwenye hotuba zake nyingi
Anaanza kumuaddress Rais Zanzibar kabla ya Makamu wa Rais wa Tanzania. Hii siyo sawa hata kidogo.

Rais wa Zanzibar ni sa
Kwani yeye mwenyewe anasemaje?
 
Nimesikiliza hotuba zake nyingi sana! Kubwa ile ya bungeni juzi.
Mama nadhani kwa makusudi anataka kulazimisha Rais wa Zanzibar ni mkubwa kiutawala kwa Makamu wa Rais.
Kwenye hotuba zake nyingi
Anaanza kumuaddress Rais Zanzibar kabla ya Makamu wa Rais wa Tanzania. Hii siyo sawa hata kidogo.

Rais wa Zanzibar ni sa
Ni sawa
 
Hakufanya sawa

Ki protocal, Hussein hana title yoyote kwa sasa kwny Jamhuri zaid ya kuwa Mjumbe tu wa Baraza la Mawaziri

Title ya Rais wa Znz kuwa Makamu wa Rais ilishaondolewa tangu 1994 kwa Ushauri wa Nyerere

Watu wa Protocal na hasa Waandishi wa Hotuba waiondoe hii sintofahamu!
 
Rais Samia
Rais Mwinyi
Makamu wa Rais Mpango
Makamu wa kwanza wa Rais
Makamu wa Pili wa Rais
Jaji Mkuu to
Jaji mkuu zanzibar
Spika wa bunge to
Spika wa balaza la Mapinduzi
Manaibu Spika
Viongozi wa ulinzi na Usalama
Viongozi wa dini
Mabalozi
Wakuu wa mashirika
Itifaki imezingatiwa
 
Back
Top Bottom