Rais Samia aagiza wote waliotajwa kwa wizi wa Fedha za Umma kwenye Ripoti ya CAG washughulikiwe

Mwananchi Huru

JF-Expert Member
Nov 20, 2021
1,446
1,001
Rais wa Tanzania Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote Tanzania ikiwemo TAKUKURU Mhe Samia Suluhu Hassan amesema haya...

"Mkurugenzi wa TPA, Waziri na TAKUKURU mpo, naamrisha ripoti ya CAG mkaisome, halafu mchukue hatua, fedha nyingi sana imepotea watu tunachekeana tu, na bado waliotajwa kwenye ripoti bado wapo maofisini wanaendeleza wizi,"

rais samia.png

==
Ukweli ni kwamba Tanzania sasa kumekucha na Rais ni Jemedari Mkuu Mhe Samia Suluhu Hassan,

Moto kwa majizi yote ya fedha za umma ni rasmi sasa unawaka na siku zao zinahesabika kwa vidole.

Wale wote waliokuwa wanamchukulia " Mama Poa " sasa wakae mkao wa kunyolewa kwa madhambi yao,

Sasa kama ulitajwa na CAG umetafuna cha Umma kaa mguu sawa, Tutaelewana tu ngoja tuone

Ushauri wangu "Nyie wenye dhamana acheni kugusa pesa ya Umma huyu mama sio Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli aliyewachekea na kuangalia wale asiowataka tu kwani Rais Samia ni Mtu wa haki Sana na hana upendeleo"
 
Anaweza? Hili sio suala la masikhara...asipepese macho akiletewa mafaili..haya mafaili yanamajina ambayo lazima usiku ukose usingizi..

Vijana walimpima JPM walipompa faili fulani, naye akasema apigwe pingu tu hakuna namna dah wale vijana wakaona hiki kweli chuma ikabidi Mzee wa Lupaso aokoe jahazi, dah sijui ingekuaje leo hii japo naamini ungekuwa ndio mwanzo wa Tanzania waitakao wengi...ile movie mzee wa Lupaso angeicha tu mwisho wake..
 
anaweza? hili sio suala la masikhara...asipepese macho akiletewa mafaili..haya mafaili yanamajina ambayo lazima usiku ukose usingizi..

vijana walimpima JPM walipompa faili fulani, naye akasema apigwe pingu tu hakuna namna dah wale vijana wakaona hiki kweli chuma ikabidi Mzee wa Lupaso aokoe jahazi, dah sijui ingekuaje leo hii japo naamini ungekuwa ndio mwanzo wa Tanzania waitakao wengi...ile movie mzee wa Lupaso angeicha tu mwisho wake..
Mtaje tu huyo muhuni usiogope
 
Kile kilikuwa chuma haswa.
 
Mnapenda sana kum overrate JPM ila jiulize Makonda na Sabaya wakati wanafanya madudu alikua haoni? Lugola na Nchambi walifungwa? Vipi waliobeba pesa za ESCROW Kwenye masandarusi wapo jela gani? Walioingiza serikali hasara ya matrillion kwenye Tanzanite na dhahabu wapo jela gani? In fact si alimpa Mwanyika ubunge wa Njombe?

JPM alikamata watendaji tu ila hakugusa wanasiasa, otherwise kamati Kuu nzima ya CCM wangekua jela sahivi.
 
View attachment 2032484
Tanzania sasa kumekucha,Moto unawaka, Wale wote waliokuwa wanamchukulia Mama poa sasa moto umewaka kwa ghafla,

Sasa kama ulitajwa na CAG umetafuna cha Umma kaa mguu sawa, Tutaelewana tu ngoja tuone,

Ushauri wangu nyie wenye dhamana acheni kugusa pesa ya Umma huyu mama sio Hayati Dkt John John Joseph Pombe Magufuli aliyewachekea,
Sasa mama si aanze kwanza kwa kuwatumbua wale waliotajwa.

Vv
 
anaweza? hili sio suala la masikhara...asipepese macho akiletewa mafaili..haya mafaili yanamajina ambayo lazima usiku ukose usingizi..

vijana walimpima JPM walipompa faili fulani, naye akasema apigwe pingu tu hakuna namna dah wale vijana wakaona hiki kweli chuma ikabidi Mzee wa Lupaso aokoe jahazi, dah sijui ingekuaje leo hii japo naamini ungekuwa ndio mwanzo wa Tanzania waitakao wengi...ile movie mzee wa Lupaso angeicha tu mwisho wake..
Funguka jombaa mbona unatembea na codes??
 
Hongera Mh. Rais kwa kuliona....nashauri IGP pia abadilishwe. Haendani na kasi yako au bado ni mfuasi/ana uraibu na Mwendazake. Wajibisha au Pangua safu za Jeshi la Polisi na TAKUKURU hasa wale wanaozembea. Ama sivyo utatoa maagizo alafu yataishia hewani.
 
Kulikuwa na haja gani kutoa tamko hadharani?

Ripoti imewaweka wazi, yeye kama Rais angewaita kama wakuu ama wa Takukuru au Polisi, kuanza kushughulika na ukamatwaji wa wahusika...
Rais hafanyi hiyo kazi yeye, Anavyombo ndio maana anaagiza sisi wacha tuone hivyo vyombo effectiveness yao
 
Back
Top Bottom